Vijana
Kushiriki Furaha ya Milele
Mojawapo wa vitu bora kuhusu injili ni ufahamu wa mpango wa wokovu. Tunayo fursa maalum ya kuwa na familia yetu milele. Huu ufahamu hutusaidia kuwa na tumaini wakati wowote tunapohisi kuzidiwa na ulimwengu. Rais Eyring anafundisha, “Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo anajua mioyo yetu. Kusudi lake ni kutupa furaha (ona 2 Nefi2:25). Na kwa hivyo alitoa kipawa cha Mwanawe ili kuwezesha furaha ya miungano ya familia inayoendelea milele. … Ni toleo ambalo kila mtoto wa Mungu ambaye uja ulimwenguni anaweza kudai.”
Baraka hiyo inatumika kwa wale kati yetu wanaoishi vyema sasa na kwa wale washaaga dunia—lakini ni tu kupitia msaada wetu. Mababu zetu wako katika ulimwengu wa roho sasa, wakitusubiria sisi tuandae majina yao kwa ibada za hekalu zifanywe kwa niaba yao. Lakini wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kufanya kazi hiyo kwa niaba yao. Tunaweza kuwa na shughuli nyingi, ama tunaweza kuwa mbali sana na hekalu tusiweze kwenda kila mara.
Kwa bahati nzuri, kuna njia zingine tunaweza kuwasaidia wahenga wetu, kama vile kufanya kazi ya historia ya familia, kuingiza majina, ama kuwashikia watoto wazazi wetu wakati wanaenda hekaluni. Kwa kusaidia, tunamtumikia Bwana na kuleta tumaini la familia za milele kwa wale walio kwenye upande mwingine wa pazia.