Njoo, Unifuate
Kuhudumu kwa Wasafiri wenzetu
Julai 19–25
“Wasaidie walio dhaifu, inyooshe mikono iliyolegea, na yaimarishe magoti yaliyo dhaifu” (Mafundisho na Maagano 81:5).
Rais Thomas S. Monson: Mfano wa Kuhudumia
Umri wa kuitwa kama askofu: 22
Nambari ya waumini katika kata: zaidi ya 1,000
Idadi ya wajane katika kata yake: 85
Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishiriki jinsi Askofu Monson alivyowatunza wajane: “Wengi wanaweza kujua kwamba kijana Askofu Monson alichukuwa muda wa wiki moja ya mapunziko yake binafsi kila msimu wa Krismasi kuwatembelea wale wajane wote themanini na tano katika kata yake. Wengi wanaweza kutojua kwamba kwa miaka kadha ya kwanza zawadi ambayo angewapelekea ilikuwa … kuku aliowafuga na kuwatayarisha yeye mwenyewe katika vibanda vyake vya kuku,”1
Askofu Monson anakumbuka jinsi alivyowasaidia vikongwe mume na mke ambao walihitaji kupaka rangi nyumba yao: “Katika muda wa msukumo sikuita, akidi ya wazee au watu wa kujitolea kutwaa brashi za rangi, lakini badala yake, nikifuata mwongozo wa kijitabu cha ustawi, niliwageukia wanafamilia ambao waliishi katika maeneo mengine. Wakwe wanne na mabinti wanne walichukuwa brashi katika mikono yao na walishiriki katika mradi huo.”2 Msukumo huu ulisaidia familia kuungana upya na kutunzana vizuri wao kwa wao.
“Hakika hatuwezi kumpenda Mungu kama hatuwapendi wasafiri wenzetu katika safari hii ya hapa duniani.”3 —Rais Thomas S. Monson