2021
Kuamini katika Bwana
Julai 2021


Wanawake wa Mwanzoni mwa Urejesho

Kuamini katika Bwana

Kwa sababu alimjua Bwana kupitia maandiko, imani ya kina ya Mary Ann Young iliweka hisia zake “shwari kabisa kwenye dhoruba yote.”1

Mary Ann Angell Young in her garden

Kielelezo na Toni Oka

Mary Ann Angell alikuwa na bahati ya kukulia katika nyumba ambayo iliwekea kipaumbele usomaji wa maandiko. Alikuwa hususani anapenda mafundisho ya Mwokozi.2 Alijifunza mapema katika maisha yake kwamba angeweza kusikia sauti ya Bwana kupitia maandiko na kupata faraja katika mafundisho Yake.

Alisikia injili ya urejesho ya Yesu Kristo ikihubiriwa katika Kisiwa cha Rhode, MAREKANI, mnamo mwaka 1831, na baada ya kusoma Kitabu cha Mormoni, Mary Ann aliongoka kwenye injili.

Alihamia Kirtland, Ohio, karibia mwaka 1833, ambako alikutana na Brigham Young, ambaye alifunga naye ndoa mnamo mapema ya mwaka 1834. Kwa miaka 48 iliyofuata, kupitia kuhama mara nyingi na majaribu, Mary Ann Angell Young aliendelea kumsikiliza Bwana kupitia maandiko na kuweka imani yake isiyoyumba Kwake.

Kwa mfano, mumewe aliondoka kwa ajili ya misheni kwenda Uingereza mnamo mwaka 1839 siku 10 tu baada ya kujifungua binti yao Alice. Kwa miezi 20 ambayo ilifuata,Mary Ann na watoto wao sita walisumbuka. Waliteseka kutokana na magonjwa na walijikimu hasa kwa mkate wa mahindi, maziwa, na mboga mboga chache za bustanini.3 Mary Ann alifanikiwa kupata kazi ndogo kusaidia familia yake na kujikimu mwenyewe na watoto wake wagonjwa. Bado Bwana aliwasaidia katika majaribu haya. “Hicho ni kitu kikubwa,” aliandika kwa mume wake, “kuamini katika Bwana.”4

Akitegemea maarifa yake ya kiroho, Mary Ann alikuwa na uthibitisho wa kina kwamba Bwana alikuwa siku zote pamoja naye, alimpenda, na alimwelewa, hususani katika masumbuko yake mengi. “Na Bwana atuekeze katika vitu vyote na aseme faraja katika masaa yenye giza nene na majaribu” ilikuwa sala yake.5

Muhtasari

  1. Barua ya Mary Ann Angell Young kwa Brigham Young, Juni. 30, 1844, Brigham Young Office Files, 1832–1878, Church History Library, Salt Lake City (CHL).

  2. Ona “Biography of Mrs. Mary Ann Young,” Woman’s Exponent, Sept. 1, 1887, 53–54; Emmeline B. Wells, “In Memoriam,” Woman’s Exponent, July 15, 1882,28–29.

  3. Ona Matthew C. Godfrey, “‘You Had Better Let Mrs Young Have Any Thing She Wants’: What a Joseph Smith Pay Order Teaches about the Plight of Missionary Wives in the Early Church,” BYU Studies, vol. 58, no. 2 (2019), 63–64.

  4. Barua ya Mary Ann Angell kwa Brigham Young, Apr. 15, 1841, Brigham Young Office Files, 1832–1878, CHL.

  5. Barua ya Mary Ann Angell kwa Brigham Young, Machi. 21, 1840, George W. Thatcher Blair Collection, 1837-1988, CHL.