Karibu kwenye Toleo Hili
Tunaweza Kuweka Uhusiano na Watakatifu wa Siku za Mwisho wa awali
Kama mwana historia wa Mradi wa Karatasi za Joseph Smith, ninapenda kutoa mahubiri ya kiibada na kuchangamana na waumini wa Kanisa kuhusu historia ya Kanisa. Kwa kufanya hivi, nimegundua kwamba baadhi ya watu wana muda mgumu wa kuweka uhusiano na watakatifu wa kale. Fafanuzi za watu hawa mara nyingi zinalenga kwenye tabia zao za kishujaa, na kufanya zionekane kama kamwe hawakusumbuliwa na shaka, maradhi, au kukata tamaa.
Lakini waumini wa Kanisa walioishi katika miaka ya 1800 walikuwa sawa na wewe na mimi tulivyo leo. Walipitia furaha na shangwe, maumivu na mateso—na mara kwa mara kama kawaida tu, walipitia siku zisizo na matukio yoyote. Nimejifunza mengi kutokana na uzoefu wao kuhusu jinsi ya kupambana na hali ya maisha ya kibinadamu.
Ninatumaini kujifunza kwako Mafundisho na Maagano mwaka huu kunakusaidia kujifunza kuhusu njia ambayo Watakatifu hapo kale walishughulikia changamoto za maisha. Pia ninatumaini makala juu ya jinsi Mary Ann Young, mke wa Brigham Young, alivyopambana na majaribu kutajenga imani yako na kukusaidia kuona kwamba tunaweza kufananisha changamoto ambazo yeye na wengine walizipitia (ona ukurasa wa 32). Hata katikati ya jitihada na huzuni, imani ya Mary Ann ilimruhusu kubaki, kama alivyomwandikia mumewe, “ni shwari kabisa kupita dhoruba zote.”
Kuna mengi tunayoweza kujifunza kutoka kwa wale waliotutangulia—sio tuu kutoka uzoefu wao wa kimiujiza bali pia kutoka kwenye kujitoa kwao bila kutangaza.
Matthew C. Godfrey
Idara ya Historia ya Kanisa