2022
Fokasi kwenye Hekalu—Dondoo
Novemba 2022


Fokasi kwenye Hekalu

Dondoo

Picha
Nukuu ya Nelson kwenye bango

Pakua PDF

Akina kaka na akina dada wapendwa, wakati wa vikao hivi vitano vya kuvutia vya mkutano mkuu, tumepata uzoefu tena kwamba mbingu zi wazi! Natumaini kwamba mmerekodi misukumo yenu na mtaendelea kuifuata misukumo hiyo. Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa, Yesu Krito, wako tayari kukusaidia. Ninawasihi kuongeza jitihada zenu za kutafuta msaada Wao.

Hivi karibuni, Mimi pamoja na Dada Nelson tulikuwa na fursa ya kupitia toleo jipya la 4 la mwendelezo wa Video za Kitabu cha Mormoni. Tulipendezwa nazo! …

Ni muhimu kwamba Mwokozi alichagua kuwatokea watu kwenye hekalu. Ni nyumba Yake. Imejawa nguvu Zake. Hebu tusipoteze mwelekeo wa kile Bwana anachotutendea. Anafanya mahekalu yake yafikike zaidi. Yeye anaongeza kasi ya sisi kujenga mahekalu. Anaongeza uwezo wetu wa kusaidia kukusanya Israeli. Pia anafanya iwe rahisi kwa kila mmoja wetu kutakaswa kiroho. Ninaahidi kwamba kutumia muda mwingi katika hekalu kutabariki maisha yako katika njia ambazo hakuna chochote kingine kinachoweza.

Wapendwa akina kaka na dada zangu, muendelee kufokasi kwenye hekalu katika njia ambazo hamjawahi kufanya hivyo kabla. Ninawabariki ili msonge karibu na Mugu na Yesu Kristo kila siku. Ninawapenda. Mungu awe nanyi mpaka tutakapokutana tena, ninaomba katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Chapisha