“Mfumo kwa ajili ya Ufunuo Binafsi—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.
Mfumo kwa ajili ya Ufunuo Binafsi
Dondoo
Tunahitaji kuelewa mfumo ambao ndani yake Roho Mtakatifu hufanya kazi kutoa ufunuo binafsi. …
Maandiko huunda kipengele cha kwanza cha mfumo huu kwa ajili ya ufunuo binafsi. Kusherehekea katika maneno ya Kristo, kama yanavyopatikana katika maandiko, huchochea ufunuo binafsi. …
Kipengele cha pili cha mfumo ni kwamba tunapokea ufunuo binafsi kulingana na utambuzi wetu pekee na si katika ridhaa za wengine. …
… Mafundisho, amri na mafunuo kwa ajili ya Kanisa ni haki ya nabii aliye hai, anayeyapokea kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. …
… Ni nabii pekee anaweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa. …
Ufunuo binafsi hakika ni wa mtu mmoja mmoja. Unaweza kupokea ufunuo, kwa mfano, kuhusu wapi pa kuishi, kazi ipi ya kufanya au nani wa kufunga naye ndoa. …
Kipengele cha tatu cha mfumo ni kwamba ufunuo binafsi utaenda sambamba na amri za Mungu na maagano tuliyofanya na Yeye. …
Tunapoomba ufunuo kuhusu kitu fulani ambacho Mungu tayari ameshakitolea mwongozo wa wazi, tunajiingiza katika kutafsiri hisia zetu kimakosa na kusikia yale tunayotaka kusikia. …
Kipengele cha nne cha mfumo ni kutambua kile ambacho Mungu tayari amekifunua kwako binafsi, wakati ukiwa tayari kwa ufunuo zaidi kutoka Kwake. …
… Ninajua kwamba Roho Mtakatifu anaweza na atakuonyesha mambo yote unayopaswa kufanya.