2022
Mfuate Yesu Kristo kwa Hatua za Imani—Dondoo
Novemba 2022


“Mfuate Yesu Kristo kwa Hatua za Imani—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Mfuate Yesu Kristo kwa Hatua za Imani

Dondoo

Picha
Nukuu ya Ballard kwenye bango

Pakua PDF

Akina kaka na akina dada, ninashuhudia kwamba tunapomfuata Yesu Kristo kwa hatua za imani, kuna matumaini. Kuna matumaini katika Yesu Kristo. Kuna matumaini kwa ajili ya wote katika maisha haya. Kuna matumaini ya kushinda makosa yetu, huzuni yetu, mapambano yetu, majaribu yetu na matatizo yetu. Kuna matumaini katika toba na kusamehewa na katika kuwasamehe wengine. Ninashuhudia kwamba kuna matumaini na amani katika Kristo. Yeye anaweza kutusaidia leo kuweza kupita nyakati zetu ngumu. Yeye alifanya hivyo kwa wale waanzilishi wa mwanzoni, na atafanya hivyo sasa kwa kila mmoja wetu. …

Ninapofikiria kuhusu waanzilishi ambao wametayarisha njia kwa ajili ya wengine, kwanza ninamfikiria Nabii Joseph Smith. …

Wamisionari wetu wa leo ni waanzilishi wa siku za sasa kwa sababu wao wanashiriki ujumbe huu mtukufu [wa urejesho] kwa watu kote ulimwenguni, hivyo wakifungua njia kwa ajili ya watoto wa Baba yetu wa Mbinguni kumjua Yeye na Mwanawe Yesu Kristo. …

Rais Nelson amekuwa mwanzilishi katika Kanisa. …

Anatufundisha sisi jinsi ya kuwa wenye kujitegemea zaidi kiroho. …

Mwokozi wetu, Yesu Kristo ndiye mwanzilishi mkuu katika kuandaa njia. Ndiyo, Yeye ni “njia” [Yohana14:6]kwa ajili ya kukamilisha mpango wa wokovu ili tuweze kutubu na, kupitia imani katika Yeye, turudi kwa Baba Yetu wa Mbinguni. …

Na daima tufuate katika hatua za Yesu Kristo na, kwa imani katika kila hatua, fokasi yetu iwe Kwake, tukiendelea kuweka miguu yetu thabiti kwenye njia ya agano.

Chapisha