“Gethsemane,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Aprili 2023
Maeneo kutoka katika Maandiko
Gethsemane
Jifunze zaidi kuhusu mahali ambapo mateso ya Mwokozi kwa niaba yetu yalianza.
Kiko wapi?
Kwenye miteremko ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu (kulia katika kielelezo, imewekewa alama ya miti mirefu kuliko kawaida).
Nini Kilikuwa Hapo?
Kijisitu cha miti ya mizeituni na pengine kinu cha kukamulia mafuta kutokana na mizeituni
Je, Ni nini Kilitokea Hapa?
Baada ya Karamu ya Mwisho, Yesu Kristo pamoja na Mitume Wake kumi na mmoja walikwenda Gethsemane. Kisha alienda kando kusali na akawachukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye.
“Akaanza kufadhaika sana, na kuhangaika.” Akasema, “Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa” (Marko 14:33–34).
“Akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki: walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
“Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.
“Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki akazidi sana kuomba: hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini” (Luka 22:42–44).
Baada ya mateso haya makali ya Mwokozi, alisalitiwa na Yuda na kukamatwa na maafisa wa Kiyahudi na kikosi cha askari wa Kirumi.
© 2023 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa. Limepigwa chapa Marekani. Idhini ya Kingereza: 6/19. Idhini ya kutafsiri: 6/19. Tafsiri ya Monthly For the Strength of Youth Message, Juni 2023. Language. 19026 743