Mwenzi Wetu Daima
Dondoo
Tunahitaji, na wewe utahitaji, wenzi wa daima wa Roho Mtakatifu. Sasa, tunautamani, lakini tunajua kutokana na uzoefu kwamba si rahisi kuupata. Sisi kila mmoja tunafikiria na kusema na kufanya vitu katika maisha yetu ya kila siku ambavyo vinaweza kumuudhi Roho.
Hilo linapotokea, kadiri litakavyotokea, tunaweza kuhisi kutokubaliwa na Bwana. Na tunaweza kujaribiwa kuhisi tuko peke yetu. …
Ukijikuta unapata shida katika kumhisi Roho Mtakatifu, unaweza kutafakari ikiwa kuna kitu chochote ambacho kwacho unahitaji kutubu na kupokea msamaha. Unaweza kuomba kwa imani ili kujua nini cha kufanya ili utakaswe na hivyo ukaribie zaidi kustahili wenzi wa daima wa Roho Mtakatifu.
Ikiwa unataka kupokea wenzi wa Roho Mtakatifu, lazima utake kumpokea kwa sababu sahihi. Kusudi lako lazima liwe kusudi la Bwana. Ikiwa nia zako ni za ubinafsi sana, utapata ugumu kupokea na kuhisi minong’ono ya Roho.
Muhimu kwangu na kwako ni kutaka kile ambacho Mwokozi anakitaka. Nia zetu zinahitaji kuongozwa na upendo safi wa Kristo. …
… Roho Mtakatifu anatumwa kwa waumini waaminifu wa agano wa Kanisa la Yesu Kristo. Sasa, uzoefu wako utakuwa wa kipekee, na Roho ataongoza kwa njia inayofaa zaidi kwa imani yako na uwezo wa kupokea ufunuo kwa ajili yako na kwa wale unaowapenda na kuwahudumia. Ninaomba kwa moyo wangu wote kwamba ujasiri wako uweze kukua.