Liahona
Mungu Atatusaidia na Kutulinda
Agosti 2024


“Mungu Atatusaidia na Kutulinda,” Liahona, Agosti. 2024.

Ujumbe wa Kila Mwezi wa Jarida Liahona, Agosti 2024

Mungu Atatusaidia na Kutulinda

Kama Kapteni Moroni, tunaweza kupokea msaada wa kiungu na nguvu kwa ajili ya mapambano tunayokabiliana nayo katika maisha.

Kapteni Moroni anashikilia bendera ya uhuru

Vielelezo na Eric Chow

Niliposoma Kitabu cha Mormoni kwa mara ya kwanza, nilifurahia historia ya vita kati ya Wanefi na Walamani. Nilivutiwa na imani, ujuzi, na mbinu zilizotumiwa na Kapteni Moroni, kamanda wa jeshi ambaye aliteuliwa kuwa kiongozi wa majeshi yote ya Wanefi alipokuwa na umri wa miaka 25 tu. Alikuwa mwenye hekima, mwenye nguvu, na mwerevu. Alikuwa amejitolea kabisa kwa uhuru na ustawi wa watu wake. (Ona Alma 48:11–12.)

Badala ya kusifia mafanikio ya kijeshi kwake mwenyewe, Moroni alielezea sifa ya mafanikio kwa Mungu na kwa msaada mtakatifu majeshi yake yaliyopokea kutoka kwa wanawake na watoto wasio wanajeshi. Alimwambia kiongozi wa adui aliyeshindwa: “Bwana … amekukabidhi mikononi mwetu. Na sasa nataka wewe ujue kwamba hii ni … kwa sababu ya dini yetu na imani katika Kristo.” Moroni kisha alishiriki umaizi huu wa kinabii: “Mungu atatusaidia, na kututunzai, na kutulinda, ilimradi tukiwa waaminifu kwake, na kwa imani yetu, na dini yetu” (Alma 44:3, 4).

Baada ya muda, nimekuja kutambua kwamba Moroni alionyesha kanuni ambazo tunaweza kuzitumia ili kutusaidia kukabiliana na changamoto za maisha yetu ya kisasa. Tunapofanya imani katika Yesu Kristo, Mwokozi wa ulimwengu, Yeye atatubariki kwa nguvu Zake. Lakini kwake Yeye kufanya hivyo na kwetu sisi kutambua baraka Zake, tunahitaji kuelewa dhumuni letu, kuweka mkakati wa mafanikio, na kujiandaa kwa mapambano ya kiisitiari tunayokabiliana nayo, kama vile Moroni alivyojiandaa kwa ajili ya na kukabiliana na mapambano halisi katika maisha yake. Tunapofanya hivyo, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo watatusaidia na kutulinda.

Kuelewa Dhumuni Letu

Moroni mara kwa mara aliwakumbusha wale watu kwamba wao walikuwa nani (warithi wa agano la Ibrahimu), ambao walikuwa (watoto wapendwa wa Mungu), na zile sababu ambazo wao walipigania (familia, imani, na uhuru). Moroni aliwafundisha watu wake kwamba walikuwa wanapigania kunusurika kwao hasa na kwa uhuru kutokana na ukandamizaji na kifungo. Kinyume chake, maadui zao walipigania kujiongezea mamlaka binafsi na nguvu kwa kuwatumikisha wengine.

Wakati baadhi ya Wanefi walipotafuta kujitwalia mamlaka bila haki kwa faida binafsi, Moroni alirarua koti lake na kuandika kwenye kipande cha koti hilo vipengele vya msingi vya ujumbe wake: “Kwa ukumbusho wa Mungu wetu, dini yetu, na uhuru wetu, na amani yetu, wake zetu, na watoto wetu.” Aliinua bendera hii, ambayo aliiita “bendera ya uhuru,” iliyofungwa juu ya ncha ya upodo na kuitumia kuwakumbusha watu kile kuhusu mapigano hayo yalihusu na kuwakusanya kwenye kusudi hilo. (Ona Alma 46:12–13, 19–20.)

Katika mapambano ya maisha ya kiroho, “hatupigani mieleka dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya … watawala wa giza … [na] dhidi ya uovu wa kiroho” (Waefeso 6:12). Sisi, pia, tunahitaji kukumbushwa juu ya kile ambacho mapambano yanahusu. Mzee Neal A. Maxwell (1926–2004), mshiriki wa zamani wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alielezea wazo hili kwa ufasaha, ingawa mazungumzo, kwa ufupi.

Mwaka 2004, nilimtembelea Mzee Maxwell katika chumba chake cha hospitali sio muda mrefu kabla ya kufariki. Alikuwa mkarimu sana kwa kila mtu aliyemtembelea au kumsaidia. Wahudumu wa afya waliingia chumbani kwake na kutoka nje wakilia. Nilimwambia, “Mzee Maxwell, hii ni vigumu sana.” Alijichekea chini chini na kusema, “Ee, Dale, sisi ni viumbe wa milele tunaoishi katika ulimwengu wenye kufa. Sisi tuko nje ya kipengele chetu, kama samaki nje ya maji. Ni wakati tu tunapokuwa na taswira ya milele kwamba yo yote kati ya haya yataleta maana yoyote.

Hatupaswi kamwe kupoteza mtazamo wa utunzi mkubwa wa asili yetu ya kiungu na hatima ya milele na nguvu za kishetani ambazo zinatupinga. Kuelewa mpango wa Baba wa Mbinguni kwa usahihi kutatutia motisha kuendelea kupigania wokovu wetu wa milele na kwa ajili ya uhuru wetu kutokana na kifungo cha kiroho.

watu wakiandaa ngome

Kupanga mkakati kwa ajili ya Mafanikio

Wakati wote wa mapambano majeshi yake yalipigana, Moroni aliweka mikakati ya kuhakikisha mafanikio. Alitumia wapelelezi kugundua shughuli na nia ya maadui zake. Alitafuta maelekezo kutoka kwa nabii, Alma. Moroni kisha alitumia mawazo hayo yenye mwongozo katika njia yake ya mapambano. Alipeleka rasilimali kulingana na mahitaji, akiweka askari zaidi katika miji ambayo ilikuwa na ngome dhaifu. Yeye kimkakati aliweka mipango ya uendeshaji kulingana na taarifa zilizo sasishwa.

Kwa hiyo alipata ushindi dhidi ya majeshi ya adui. Hakuwahi kuridhika na ushindi uliopita; badala yake, aliendelea kuboresha uwezo wake na wa majeshi yake ili kukabiliana na changamoto za siku zijazo.

Tunaweza kutumia mbinu sawa na hizo ili kukabiliana na maadui wa kiroho. Tunaweza kuanza kwa kutambua kile Shetani anachojaribu kufanya katika maisha yetu. Anajaribu kutuvuruga kutoka kwenye dhumuni letu. Tunapokabiliwa na majaribu, tunapaswa kujiuliza wenyewe:

  • Ni kwa jinsi gani kitendo hiki kwa upande wangu kinasimama dhidi ya neno lililofunuliwa la Mungu?

  • Nini matokeo ya kuchukua hatua hii?

  • Je, kitendo hiki kitanisaidia kutimiza dhumuni langu duniani?

Tunapaswa pia kutambua matokeo ya mwisho ya kukubali hata majaribu madogo. Tunapokubali majaribu, tunakula “sumu kidogo kidogo” (Alma 47:18), mkakati wenye ufanisi zaidi unaotumiwa na nguvu za uovu ambao unaweza kusababisha matokeo mabaya ya kiroho.

Tunaweza kujiimarisha wenyewe dhidi ya majaribu ya Shetani kwa kufuata maelekezo tunayopokea kutoka kwa nabii wetu wa siku za mwisho. Kufanya hivyo kunatusaidia kutunza mtazamo wa milele ambao kupitia huo kutathmini matendo yetu. Kufanya mikakati jya jinsi tutakavyokabiliana na majaribu yanayotokea katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu kutatusaidia kufanya chaguzi sahihi zaidi kwa wakati huo. Mikakati na mbinu zilizoandaliwa mapema zitatusaidia kujilinda dhidi ya vivuta mawazo kutokana na dhumunii letu la milele.

Mfano ni ule wa teknolojia. Teknolojia inaweza kuwa upanga wenye makali pande mbili, vyote muhimu na yenye madhara, kulingana na jinsi tunavyoutumia. Ili kutusaidia kufanya chaguzi za busara kuhusu vifaa vyetu, vijana na wazee tunaweza kurejelea “Kuchukua Jukumu la Teknolojia” na Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi. Haya yanatukumbusha dhumuni letu, linatuelekeza kwa Yesu Kristo, na linatusaidia kumwalika Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Kupanga jinsi gani, lini, na wapi tutatumia teknolojia kutatuimarisha dhidi ya mbinu ovu, za kidunia.

Walamani wakishambulia ngome za Wanefi

Kujiandaa kwa ajili ya Mapambano ya Kisitiari

Akitarajia vita vijavyo, Moroni aliwatandaa watu wake kibinafsi kwa dirii, ngao, chepeo, na mavazi mazito. Aliwaandaa watu wake kwa pamoja kwa kuzungushia miji kwa ngome, akijenga kuta ndefu za udongo kuwazunguka.

Kiroho, tunajiandaa kibinafsi kwa kutii amri za Mungu. Tunafanya na kushika maagano na Mungu ambayo yanavuta nguvu ya Yesu Kristo katika maisha yetu. Tunajishughulisha na vitendo binafsi, vya ibada ya faragha, kama vile kusali, kufunga, na kupekua maandiko. Sisi pia tutende katika imani, tukijibu mwongozo wa kiroho tunaoupata. Kwa dhamira tunajiandaa kwa ajili ya na kupokea sakramenti kwa kustahili. Tunapofanya hivyo, Mwokozi anakuwa halisi zaidi katika maisha yetu, kama vile alivyokuwa halisi kwa Moroni, ambaye alikuwa imara katika imani yake katika Yesu Kristo. Moroni alijua angeweza kumtegemea Mwokozi kwa ajili ya maelekezo na ukombozi (ona Alma 48:16). Sisi, pia, tunaweza kumtegemea Yesu Kristo kwa ajili ya mwelekeo na ukombozi.

Tunaweza kujiandaa zaidi kwa kuimarisha familia zetu. Baba yetu wa Mbinguni alitupanga katika familia ili kutusaidia kuwa na furaha na kujifunza jinsi ya kurudi Kwake. Familia zetu zinaweza kuwa chanzo cha msaada kwetu. Sote tunaweza kuhisi shangwe na upendo kwa kukumbuka kwamba sisi ni sehemu ya familia kubwa ya Mungu, bila kujali hali binafsi za familia zetu.

Tunaweza kwa pamoja kupata nguvu na kujiandaa kwa ajili ya mapambano yetu ya kiroho tunapojiunga katika jumuiya za Watakatifu. Vigingi vyetu na wilaya zetu hutoa sehemu kama hiyo ya kimbilio na ulinzi. Tunaweza kulishana kiroho, kusaidiana kutii amri za Mungu, na kuhimizana kumtegemea Kristo, daima na hasa katika nyakati za changamoto. Tunapokusanyika, tunatambua kwamba hatupigani mapambano yetu peke yetu. Tuna marafiki, walimu, na viongozi ambao wanaweza kutusaidia na kutulinda. Tunakuwa imara zaidi pale tunapojiandaa pamoja.

Cha kushangaza, Moroni alielezea furaha yote ya watu wake kuwa wakweli kwa imani yao katika Mungu wao na dini yao. Kama Moroni, tunapaswa kutambua kwamba shangwe huja kwa sababu ya Baba wa Mbinguni na mpango Wake na kwa sababu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Tunapokuja kuelewa dhumuni letu, tuweke mkakati kwa ajili ya mafanikio, na kujiandaa kwa ajili ya mapambano ya kisitiari, tunapokea msaada na nguvu ya kiungu.

Kama Moroni, ninajua kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo mwishowe ndio wanaoleta uhuru kutoka kifungoni—uhuru kutokana na kifo na dhambi. Wanatubariki kwa nguvu Zao wakati tunapowatazamia Wao katika mambo yote.

Muhtasari

  1. Kuchukua Jukumu la Teknolojia,” Maktaba ya Injili.

  2. Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (2022), Maktaba ya Injili.

  3. Ona Russell M. Nelson, “Shangwe na Kunusurika Kiroho,” Liahona,, Nov. 2016, 82.