Liahona
Vijana Askari Mashujaa
Agosti 2024


“Vijana Askari Mashujaa,” Rafiki, Agosti 2024, 26-27.

Ujumbe wa Kila Mweziwa Jarida la Rafiki la Agosti 2024

Vijana Askari Mashujaa

Picha
Watu wakizika silaha zao shimoni

Vielelezo na Andrew Bosley

Watu ambao Amoni na kaka zake waliwafundisha walitaka kumfuata Yesu Kristo. Walizika silaha zao na kumuahidi Mungu kwamba kamwe hawatapigana tena.

Picha
Kundi la wavulana linakaribia nyumba ambapo watu wazima wakubwa wanazungumza

Lakini punde walihitaji kulinda familia zao. Akina baba waliozika silaha zao hawakutaka kuvunja ahadi yao na Mungu. Hivyo wana wao walijiandaa kupigana badala yao. Waliitwa wale askari vijana elfu mbili. Mvulana humaanisha “kijana.”

Picha
Mvulana akisali pamoja na mama yake wakati wavulana wengine wakikusanyika wakiwa na silaha

Vijana askari hawakuwahi kupigana vita hapo awali. Lakini mama zao walisaidia kuwaandaa na kuwafundisha kumtumaini Mungu.

Picha
Helamani akiongoza vijana askari mashujaa kwa mwendo; mvulana anamsaidia kutembea mvulana mwingine aliyejeruhiwa

Walimchagua Helamani kuwa kiongozi wao. Walikuwa jasiri, na Mungu aliwasaidia. Wote waliumizwa, lakini walisaidiana. Mungu aliheshimu imani yao, na wote waliishi!

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Maandiko Yanaweza Kunisaidia Mimi Kila Siku.

Picha
Ukurasa wa kupaka rangi wa maumbo ya Kitabu cha Mormoni yakitoka nje ya kurasa za kitabu kilicho wazi

Kielelezo na Adam Koford

Ni hadithi gani ya maandiko unayoipenda?

Chapisha