“Aprili 11. Ninawezaje Kuwaalika Wote Kuja kwa Kristo? Mafundisho na Maagano 30–36,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Aprili 11. Ninawezaje Kuwaalika Wote Kuja kwa Kristo?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Aprili 11
Ninawezaje Kuwaalika Wote Kuja kwa Kristo?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha, pamoja na kushauriana pamoja kuhusu shughuli maalum za akidi au darasa, mnaweza kutaka kujadili misukumo na dhima kutoka mkutano mkuu. Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia.
-
Ni dhima au jumbe zipi zimejitokeza bayana kwetu?
-
Tumehisi kushawishika kufanya nini kwa sababu ya kile tulichojifunza au kuhisi?
-
Je, tunahitajika kufanya nini kama akidi au darasa ili kutendea kazi ushauri tuliousikia katika mkutano mkuu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Miezi kadhaa baada ya Kanisa lililorejeshwa kuanzishwa mnamo Aprili 6, 1830, huko Fayette, New York, Bwana alianza kuwaita wamisionari ili kuwakusanya “wateule kutoka pande nne za dunia” (Mafundisho na Maagano 33:6). Kile kilichoanza kama juhudi za waongofu wapya wachache katika eneo finyu kimekua hadi kufikia jeshi la wamisionari wakitangaza injili ulimwenguni kote. Lakini kazi ya umisionari haijajikita kwa wale tu wanaotumikia kama wamisionari wa muda wote. Bwana anahitaji kila mmoja wetu kuwaalika wale wanaotunzunguka kuja Kwake.
Ni uzoefu gani umeupata kwa kuwaalika wengine ili kujifunza kuhusu injili ya Mwokozi? Unaweza kufanya nini kuwahimiza washiriki wa akidi au darasa kutekeleza majukumu yao ya kuzileta nafsi kwa Yesu Kristo? Unapojiandaa kufundisha, fikiria kurejea “What Is My Purpose as a Missionary?” katika Preach My Gospel ([2019] 1–16) na ujumbe wa Mzee Dieter F. Uchtdorf “Kazi ya Umisionari: Shiriki Kile Kilichopo Moyoni Mwako,” Liahona, Mei 2019, 15–18).
Jifunzeni Pamoja
Mafundisho na Maagano 30–36 inataja majina ya watu kadhaa ambao waliitwa misheni katika siku za mwanzo za Kanisa. Siku chache kabla ya mkutano wenu, unaweza kumpatia kila mshiriki wa akidi au darasa mojawapo ya haya majina (Ona Vichwa vya habari vya sehemu za 30–36) na kumualika mshiriki kujifunza ni ushauri gani Bwana aliutoa kumsaidia mtu huyo kushiriki injili. Je, tunawezaje kuutumia ushauri huo kwetu sisi wenyewe? Mawazo hapa chini yanaweza kuwahamasisha wale unaowafundisha kuwaalika wale wanaowazunguka kuja kwa Kristo.
-
Je, wale unaowafundisha wanaelewa kuja kwa Kristo kuna maana gani? Unaweza kuwaomba washiriki mawazo yao. Kama inaweza kuwa yenye msaada, unaweza kushiriki maelezo haya: “Kuja kwa Mwokozi, lazima watu wawe na imani Kwake ya kuongoza kwenye toba—wakifanya marekebisho muhimu ya kubadili maisha yao ili yaendane na mafundisho Yake” (Preach My Gospel, 2). Washiriki wa akidi au darasa pia wanaweza kusoma maandiko yanayohusisha vifungu vya maneno kama “njooni kwangu” au “njooni kwa Kristo” ili kuwasaidia kujibu swali hili—kwa mfano, Mathayo 11:28–30; Omni 1:26; Moroni 10:32; Mafundisho na Maagano 20:59. Kwa nini tunahitaji watu waje kwa Kristo? Je, ni baadhi ya mambo gani ya kawaida tunayoweza kufanya kuwasaidia? Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuweka mipango ya kumualika yeyote wanayemjua ili kuja karibu na Kristo.
-
Kujifunza kuhusu jinsi ambavyo wengine wameshiriki injili ni njia kuu ya kuwahamasisha wale unaowafundisha. Unaweza kuonyesha video moja au zaidi zinazopatikana katika “Nyenzo Saidizi” au waalike washiriki wa akidi au darasa kusoma ushauri na mifano inayopatikana katika ujumbe wa Dada Cristina B. Franco “Kupata Shangwe kwa Kushiriki Injili” (Liahona, Nov. 2019, 83–86). Tunajifunza nini kutoka katika mifano hii? Jadilianeni kwa pamoja nini akidi au darasa lako linaweza kufanya ili kuwaalika wengine kuja kwa Kristo.
-
Unapokuja wakati wa kushiriki injili, Mzee Dieter F. Uchtdorf alisema kwamba baadhi yetu tunaweza “kuhisi kutokujua nini cha kufanya. Au tunaweza kuhisi woga kwenda nje ya mipaka yetu tuliyoizoea” (“Kazi ya Umisionari: Kushiriki Kile Kilichopo Moyoni Mwako,” Liahona, Mei 2019, 16). Kama washiriki wa akidi au darasa wanahisi hivi, mapendekezo matano rahisi yaliyotolewa na Mzee Uchtdorf katika ujumbe wake yanaweza kuwasaidia. Unaweza kumualika kila mshiriki wa darasa kusoma kuhusu mojawapo ya mapendekezo yake na kushiriki kile walichojifunza.
Tenda kwa Imani
Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.
Nyenzo Saidizi
-
1 Timotheo 4:12 (Uwe kielelezo kwao waaminio)
-
Alma 17:2–4 (Wana wa Mosia walijiandaa kushiriki injili)
-
Mafundisho na Maagano 42:6–7 (Hubiri injili kwa nguvu ya Roho)
-
Russell M. Nelson na Wendy Nelson, “Tumaini la Israeli” (ibada ya vijana duniani kote, Juni 3, 2018), nyongeza kwenye New Era na Ensign, HopeofIsrael.ChurchofJesusChrist.org
-
(Video) “Inviting All to Come unto Christ: Sharing the Gospel,” “Inviting Others to ‘Come and See,’” “Inviting Others to ‘Come and Help,’” “Inviting Others to ‘Come and Stay’”, ChurchofJesusChrist.org