Mafundisho na Maagano 2021
Aprili 25. Ninawezaje Kuwa Zaidi Kama Kristo katika Huduma Yangu kwa Wengine? Mafundisho na Maagano 41–44


“Aprili 25. Ninawezaje Kuwa Zaidi Kama Kristo katika Huduma Yangu kwa Wengine? Mafundisho na Maagano 41–44,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Aprili 25. Ninawezaje Kuwa Zaidi Kama Kristo katika Huduma Yangu kwa Wengine?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
Yesu Kristo akiosha miguu ya Mitume

Yesu Akiosha Miguu ya Mitume, na Del Parson

Aprili 25

Ninawezaje Kuwa Zaidi Kama Kristo katika Huduma Yangu kwa Wengine?

Mafundisho na Maagano 41–44

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, ni nani mgeni katika kata yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia kuhisi wamekaribishwa? Ni nini tunafanya ili kufanya muda wetu katika mikutano ya akidi au darasa kuwa wa maana?

  • Wajibu wetu au majukumu. Ni yapi baadhi ya majukumu na wajibu tulionao kama wavulana na wasichana? Tunawezaje kuyatimiza vyema?

  • Maisha yetu. Ni nini tunafanya ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo na kupokea nguvu Zake katika maisha yetu? Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja Kwake?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Wakati Bwana alipowaamuru Watakatifu kukusanyika Kirtland, Ohio, watu wengi kwa uaminifu waliacha nyumba zao na kusafiri kuelekea huko. Lakini kuhama huku hakukuwa tu kuhusu kuishi katika sehemu mpya—ilikuwa pia kuhusu kuishi katika njia mpya. Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuwa wamesoma Mafundisho na Maagano 41–44 wiki hii na kujifunza kuhusu kuhamia kwa Watakatifu huko Kirtland na sheria ambayo Bwana aliifunua kwao wakiwa huko. Miongoni mwa mambo mengine, Bwana alitarajia Watakatifu kuwa wamoja kadiri walivyopendana na kutumikiana (ona Mafundisho na Maagano 42:30–31, 38–39, 45; 44:6). Ni uzoefu gani unaweza kuushiriki ambao unaweza kusaidia akidi yako au darasa lako kuhisi umuhimu wa huduma kama ya Kristo?

Ili kukusaidia kujiandaa kufundisha kuhusu huduma kama ya Mwokozi, unaweza kurejea “Huduma” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ([2011], 32–33) na ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Amri Kuu ya Pili” (Liahona, Nov. 2019, 96–100).

Picha
mvulana na mwanamke wa makamo wakicheka pamoja

Tunaweza kuwatumikia wengine kama Mwokozi alivyofanya.

Jifunzeni Pamoja

Kwa kuanza mjadala kuhusu huduma kama ya Kristo, unaweza kuandika ubaoni “Kuishi pamoja katika upendo” (Mafundisho na Maagano 42:45). Waalike washiriki wa akidi yako au darasa lako kusoma Mafundisho na Maagano 42:30–31, 38–39, 45; 44:6 na waorodheshe njia ambazo Bwana aliwahitaji Watakatifu kutumia ili kutumikiana wao kwa wao. Ni fursa gani tunazo, kote ndani ya nyumba zetu na nje ya nyumba zetu, za kuwatumikia wale walio na mahitaji ya kimwili, kihisia, au kiroho? Chagua kutoka kwenye mawazo yaliyo hapa chini ili kuhamasisha akidi yako au darasa lako kutoa huduma kama ya Kristo kwa wengine.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kujifunza kutoka katika mfano wa huduma wa Mwokozi, unaweza kumpa kila mtu jukumu la kusoma kifungu cha andiko linalohusu Mwokozi akimtumikia mtu (ona “Nyenzo Saidizi”). Kila mtu anaweza kufupisha kifungu cha andiko na kuelezea kile ambacho Mwokozi alikifanya ili kuwatumikia wengine. Je, mifano hii inafundisha nini kuhusu kutumikia kama Mwokozi alivyotumikia? Kuna tofauti gani kati ya kutumikia katika njia ya Mwokozi na njia nyinginezo za kutumikia? Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki uzoefu wakati walipojaribu kutumikia kama Mwokozi alivyotumikia au wakati wengine walipowatumikia wao katika njia hii.

  • Inaweza kuwa yenye msaada zaidi kwa akidi yako au darasa lako kurejea kile ambacho Mwokozi na manabii Wake wamekifundisha kuhusu huduma. Haya ni baadhi ya mafungu ya maandiko wanayoweza kuyasoma pamoja: Mathayo 25:31–46; Luka 10:25–37; Yohana 13:34–35; Yakobo 1:27; Mosia 2:17; 18:8–10. Wahimize waandike kile ambacho wamejifunza kuhusu kuwatumikia wengine na kushiriki mawazo na uzoefu unaohusiana na kile walichojifunza. Kisha wanaweza kupanga njia za kutoa huduma kama ya Mwokozi. (Wanaweza kupata mawazo kwa kuangalia moja au zaidi ya video katika “Nyenzo Saidizi” au watembelee JustServe.org.)

  • Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa katika juhudi zao za kuwahudumia wengine, fikirieni kurejea pamoja ujumbe wa Dada Bonnie H. Cordon “Kuwa Mchungaji” (Liahona, Nov. 2018, 74–76). Unaweza kuanza kwa kuonyesha baadhi ya picha za Mwokozi akitumikia (Dada Cordon alionyesha baadhi wakati wa ujumbe wake). Picha hizi zinafundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kuhudumu katika njia ya Mwokozi? Kisha fikiria kuwaalika washiriki wa akidi au darasa wasome katika jozi mojawapo ya vipengele vya ujumbe na kushiriki kile walichojifunza kuhusu jinsi ya kutumikia kama Mwokozi. Pia, wanaweza kushiriki kile wanachojifunza kuhusu huduma kama ya Kristo pale wanapowahudumia wengine.

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Wakati wa huduma yake hapa duniani, Yesu Kristo alitumia muda Wake akiwatumikia na kuwasaidia wale waliokuwa wanamzunguka. Wafuasi wa kweli wa Kristo hufanya kama alivyofanya (ona Yohana 13:35). Tafuta fursa za kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kushiriki jinsi walivyowatumikia wengine na nini kiliwahamasisha wao kutoa huduma. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 4–5.)

Chapisha