Mafundisho na Maagano 2021
Mei 9. Ninawezaje Kubarikiwa na Roho Mtakatifu Kila Siku? Mafundisho na Maagano 46–48


“Mei 9. Ninawezaje Kubarikiwa na Roho Mtakatifu Kila Siku? Mafundisho na Maagano 46–48,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Mei 9. Ninawezaje Kubarikiwa na Roho Mtakatifu Kila Siku?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
msichana akisali

Mei 9

Ninawezaje Kubarikiwa na Roho Mtakatifu Kila Siku?

Mafundisho na Maagano 46–48

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, ni nani anahitaji usaidizi wetu na sala zetu? Je, ni kipi tunaweza kufanya ili kuwasaidia? Je, nani tumualike katika shughuli ijayo?

  • Wajibu wetu au majukumu. Je, ni majukumu gani tumeshayatimiza? Je, ni majukumu gani tunahitaji kuyatoa? Je, ni kwa jinsi gani tumewaalika wengine kuja kwa Kristo, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaalika wengine hivi sasa?

  • Maisha yetu. Je, ni uzoefu gani wa hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu? Je, ni nini kinatokea katika maisha yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Waumini wengi wa mwanzo wa Kanisa lililorejeshwa walikuwa wamesoma katika maandiko kuhusu kujidhihirisha kiroho kwa Roho Mtakatifu (ona Matendo ya Mitume 2:1–4; 13:52; 1 Wakorintho 12:4–11; 3 Nefi 19). Washiriki wa akidi au darasa waliposoma Mafundisho na Maagano 46–48 wiki hii, wanaweza kuwa walijifunza kuwa Bwana alikuwa na hamu ya kuwafundisha Watakatifu hawa kuhusu baraka ambazo Roho Mtakatifu anaweza kuzileta katika maisha yao. Ni uzoefu gani umekufundisha wewe kuhusu jinsi Roho Mtakatifu anavyokubariki? Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu huwasaidia katika kila kipengele cha maisha yao wale unaowafundisha?

Ili kukusaidia kujiandaa kuihamasisha akidi yako au darasa lako kutafuta ushawishi wa Roho Mtakatifu, unaweza kurejea “Roles of the Holy Ghost” katika True to the Faith ([2004], 82) na ujumbe wa Mzee Gary E. Stevenson “Ni kwa Jinsi Gani Roho Mtakatifu Hukusaidia?” (Liahona, Mei 2017, 117–20).

Picha
msichana akisoma maandiko darasani

Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kuelewa na kufundisha kweli za injili.

Jifunzeni Pamoja

Maandiko hutoa mifano mingi ya vipawa vya roho. Unawezaje kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa lako kuongeza imani yao kwamba vipawa hivi vinaweza kuonekana katika maisha yetu leo? Unaweza kuanza kwa kuwaalika wao waandike ubaoni kipawa cha roho kilichoelezewa katika Mafundisho na Maagano 46:7–33 na kujadili jinsi walivyokiona kikidhihirishwa katika maisha yao au kwenye maisha ya mtu wanayemjua.

Kwa kuongezea kwenye vipawa vya Roho, Roho Mtakatifu pia hutubariki katika njia mbalimbali. Unaweza kutumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo hapa chini kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuelewa hili vyema.

  • Wakati mwingine tunadhani kwamba tunamhitaji Roho Mtakatifu kwa maamuzi au matukio maalum tu katika maisha yetu. Unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kutambua ni mambo mengi kiasi gani Roho Mtakatifu anaweza kuwafanyia? Unaweza kuigawa akidi au darasa katika makundi madogo madogo na kuliomba kila kundi kusoma andiko moja au zaidi kutoka kwenye “Nyenzo Saidizi.” Mtu mmoja kutoka kila kundi anaweza kushiriki kile walichojifunza. Kisha mwalike kila mshiriki wa akidi au darasa kuandaa orodha ya njia ambazo Roho Mtakatifu huweza kubariki maisha yao ya kila siku. Wanaposhiriki orodha zao, wanaweza kuongelea jambo wanaloweza kufanya ili kuwa na Roho Mtakatifu pamoja nao kila siku.

  • Njia nyingine ya kuwasaidia wale unaowafundisha waweze kuelewa jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kuwasaidia ni kuandika maswali yafuatayo ubaoni: Ni nini tunakijua kuhusu Roho Mtakatifu? Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kutusadia? Kisha washiriki wa akidi au darasa wanaweza kutafuta majibu katika ujumbe wa Mzee Gary E. Stevenson “Ni kwa Jinsi Gani Roho Mtakatifu Hukusaidia?” (Liahona, Nov. 2017, 117–20). Pia wanaweza kutafuta majibu kwa kurejea “Roles of the Holy Ghost” katika True to the Faith (ukurasa wa 82). Kama inafaa, shiriki uzoefu uliowahi kuupata wa Roho Mtakatifu, na waalike vijana kushiriki uzoefu waliowahi kuupata.

  • Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kusoma “Personal Revelation” au “Learn to Recognize the Promptings of the Spirit” katika sura ya 4 ya Preach My Gospel ([2019], 95–96, 102–3). Kisha wanaweza kujifanya kwamba wao ni wamisionari wakimfundisha mtu ambaye hajawahi kusikia kabisa kuhusu jinsi Roho Mtakatifu anavyoweza kubariki maisha yetu. Ni nini wangesema kwao?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi alishiriki hadithi rahisi, mafumbo, na mifano halisi ya maisha ili kufundisha katika njia iliyoleta maana kwa wanafunzi Wake. Ni uzoefu gani binafsi unaoweza kuushiriki na vijana ili kuwasaidia wao waelewe majukumu ya Roho Mtakatifu na kuhisi hamu ya kutafuta uzoefu sawa na huo? (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 22.)

Chapisha