Mafundisho na Maagano 2021
Mei 23. Ninawezaje Kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu? Mafundisho na Maagano 51–57


“Mei 23. Ninawezaje Kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu? Mafundisho na Maagano 51–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Mei 23. Ninawezaje Kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
msichana akisimikwa

Mei 23

Ninawezaje Kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu?

Mafundisho na Maagano 51–57

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Tunaweza kufanya nini ili kujenga umoja miongoni mwa washiriki wa akidi au darasa? Je, ni malengo gani tunahitaji kuyashughulikia kwa pamoja?

  • Wajibu wetu au majukumu. Tunafanya nini ili kushiriki injili? Ni uzoefu upi tumeupata kwa kufanya kazi ya hekalu na historia ya familia?

  • Maisha yetu. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu? Ni nini kimetutia moyo katika kujifunza kwetu maandiko wiki hii?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Baada ya kuwa tumebatizwa, wenye ukuhani huweka mikono yao juu ya vichwa vyetu kutupatia kipawa cha Roho Mtakatifu. Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuwa wamekumbushwa hili walipokuwa wakijifunza Mafundisho na Maagano 51–57 wiki hii. Hata hivyo, kupokea Roho Mtakatifu huhitaji zaidi ya hilo. Ili kupokea Roho Mtakatifu kama mwenza wetu wa muda wote, lazima tutamani uwepo Wake, tumualike Yeye katika maisha yetu, na kwa uaminifu kutii amri. Ni baraka zipi zitakuja katika maisha ya wale unaowafundisha kadiri wanavyotafuta ushawishi Wake?

Ili kukusaidia unapojiandaa kufundisha, unaweza kurejea “The Gift of the Holy Ghost” katika True to the Faith ([2004], 83–84) au ujumbe wa Mzee Henry B. Eyring “Roho Wake Awe Nanyi” (Liahona, Nov. 2018, 86–89).

Picha
wavulana na wasichana wakiwa darasani

Ili kupokea mwongozo wa Roho Mtakatifu, tunapaswa kutafuta ushawishi Wake kila siku.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuelewa vyema kipawa cha Roho Mtakatifu, unaweza kuanza kwa kuongelea ni kwa jinsi gani kipawa cha Roho Mtakatifu hutolewa. Wanaweza kusoma Mafundisho na Maagano 52:10; 53:3; 55:1–3 na kujadili kile walichojifunza. Sisitiza kwamba mwenye ukuhani hatoi Roho Mtakatifu lakini anamualika muumini kupokea Roho Mtakatifu. Je, kuna tofauti gani? Shughuli hapa chini zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema jinsi ya kupokea kipawa hiki kisicho na kifani.

  • Kile Lehi na familia yake walichokifanya ili waongozwe na Liahona ni sawa sawa na kile tunachotakiwa kufanya ili kupokea ushawishi wa kuongoza wa Roho Mtakatifu. Unaweza kuonyesha picha ya Lehi na Liahona (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, [2009], na. 68), na waombe washiriki wa akidi au darasa kushiriki kile wanachokijua kuhusu Liahona. Kisha, unaweza kuwaalika nusu yao kusoma 1 Nefi 16:14–29 na nusu nyingine kusoma 1 Nefi 18:8–22, wakitafuta njia ambazo Liahona ni sawa na Roho Mtakatifu. Tunajifunza nini kutoka kwenye mfano wa familia ya Lehi ambacho kinaweza kutusaidia sisi kupokea Roho Mtakatifu kwa ukamilifu zaidi?

  • Kila kipengele katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana kimebeba ushauri kuhusu kuishi viwango na amri za Bwana. Kuishi amri hizi hualika nguvu ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Fikiria kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kila mmoja kuchagua sehemu mojawapo katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, waisome, na kuweka alama kwenye vitu ambavyo wanapaswa kufanya au kutofanya ili kuwasaidia wao kupokea Roho Mtakatifu. Kisha wanaweza kushiriki kile walichojifunza kwa wenzao wa akidi au darasa. Waalike waweke lengo litakalowasaidia wao kupokea Roho Mtakatifu kwa ukamilifu zaidi. Je, Kwa nini tunataka Roho Mtakatifu awe pamoja nasi? (ona Yohana 14:26–27; 15:26; 16:13; 2 Nefi 32:3).

  • Katika ujumbe wake “Roho Wake Awe Nanyi” (Liahona, Mei 2018, 86–89), Rais Henry B. Eyring alisema, “Tumaini langu leo ni kuongeza hamu yenu na uwezo wenu wa kupokea Roho Mtakatifu” (ukurasa wa 86). Waombe washiriki wa akidi au darasa kusoma aya tisa katika ujumbe wake wakianzia na “Uzoefu wa Nabii Joseph Smith” (ukurasa wa 88). Waalike kutafuta kile ambacho Joseph Smith alifanya ili kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu. Wanaweza kuorodhesha ubaoni majibu wanayoyapata. Kama inafaa, unaweza kuwaalika kushiriki uzoefu wao wa kupokea mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Walikuwa wanafanya nini wakati wa uzoefu huu uliopelekea kupokea mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu? Unaweza kushiriki uzoefu wako pamoja nao pia.

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Katika matayarisho Yake ya huduma ya duniani, Mwokozi “aliongozwa na Roho kwenda nyikani” kufunga, kusali, na “kuwa pamoja na Mungu” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:1 [katika Mathayo 4:1, tanbihi b]). Ufundishaji injili wenye nguvu haumaanishi tu kutayarisha somo bali pia kujiandaa sisi wenyewe. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 12.)

Chapisha