Mafundisho na Maagano 2021
Juni 13. Ninawezaje Kuepuka Ponografia? Mafundisho na Maagano 63


“Juni 13. Ninawezaje Kuepuka Ponografia? Mafundisho na Maagano 63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Juni 13. Ninawezaje Kuepuka Ponografia?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

msichana akiwa ameshikilia simu

Juni 13

Ninawezaje Kuepuka Ponografia?

Mafundisho na Maagano 63

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, ni shughuli gani tumeshafanya hivi karibuni? Je, zilifanikiwa? Ni nini kilifanyika vizuri, na ni jinsi gani tunaweza kuziboresha?

  • Wajibu wetu au majukumu. Ni nani anahitaji usaidizi wetu? Tunawezaje kuwasaidia?

  • Maisha yetu. Ni malengo gani tunayashughulikia kibinafsi? Ni uzoefu gani tunaweza kuushiriki? Ni baraka zipi tumezipokea?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuwa wamejifunza Mafundisho na Maagano 63 wiki hii na kusoma kuhusu onyo la Bwana kwa Watakatifu wa mwanzo kuhusu hatari za tamaa—onyo Alilolitoa mara kwa mara (ona Mafundisho na Maagano 63:13–16; Mathayo 5:27–28; 3 Nefi 12:27–30). Wakati maonyo haya yametumika kwa watu wote katika nyakati zote, yanatumika kwa msisitizo sana katika siku yetu, wakati ponografia ni janga lililosambaa kote. Ni hatari gani na mashinikizo yahusianayo na ponografia ambayo washiriki wa akidi yako au darasa lako wanaweza kukutana nayo? Ni kanuni zipi za injili na njia zipi za kujikinga zinaweza kuwasaidia kuweka mawazo yao na matendo yao kuwa safi?

Unapojiandaa kufundisha, fikiria kurejea “Burudani na Vyombo vya Habari” na “Usafi wa Kijinsia” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ([2011], 11–13, 35–37) na Wema Uyapambe mawazo Yako (kijitabu, 2006).

wavulana wakiwa darasani

Washiriki wa akidi na darasa wanaweza kuimarishana katika kuepuka ponografia.

Jifunzeni Pamoja

Kuanza mjadala kuhusu ponografia, unaweza kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kusoma Mafundisho na Maagano 63:13–16 na kujadili mawazo yanayopatikana katika mistari hii ambayo huwasaidia wao kuelewa kwa nini ponografia ni hatarishi sana. Ili kuwasaidia washiriki wa akidi yako au darasa lako kuelewa jinsi ya kuepuka ponografia, tumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo. Kwenye hitimisho la mjadala wako, unaweza kuhisi kupokea msukumo wa kujadili jinsi askofu anavyoweza kuwasaidia wale waliojihusisha na ponografia (ona Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, 12, 37).

  • Washiriki wa akidi yako au darasa lako wanaweza kuwa na maswali kuhusu kuepuka ponografia. Ili kuwasaidia wao kuweza kupata majibu, unaweza kuandika maswali yafuatayo ubaoni: Ponografia ni nini? Kwa nini ni hatarishi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuepukana na kishawishi cha ponografia? Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kupata majibu kwa maswali mawili ya mwanzo, waombe warejee “ponography” katika True to the Faith (kurasa 117–18) na “Burudani na Vyombo vya Habari” na “Usafi wa Kijinsia” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (kurasa 11–13, 35–37). Ili kuwasaidia kupata majibu kwa swali la tatu, waombe warejee Mwanzo 39:1–12; Warumi 12:21; 2 Timotheo 2:22; Alma 39:3–9; Moroni 10:30; Mafundisho na Maagano 27:15–18; 121:45–46. Waalike kushiriki majibu waliyoyapata.

  • Ili kuisaidia akidi yako au darasa lako kugundua njia za kuepuka ponografia, unaweza kuwataka wapitie ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Hakuna Nafasi Tena kwa ajili ya Adui wa Nafsi Yangu” (Liahona, Mei 2010, 44–46) na ujumbe wa Dada Linda S. Reeves “Ulinzi kutokana na Ponografia—Nyumba Inayofokasi kwa Kristo” (Liahona, Mei 2014, 15–17). Wanaweza wakapiga taswira kwamba wanafanya mahojiano na kijana au binti yao ajaye kuhusu kwa nini ponografia ni haribifu sana na jinsi ya kuiepuka. Ni taarifa ipi wanaweza kuishiriki kutoka kwenye ujumbe wa mkutano waliourejea? Waalike kuwa katika jozi na kushiriki majibu waliyoyapata. Pia waombe waandike watafanya nini kuepuka ponografia.

  • Waalike wale unaowafundisha wasome 1 Wakorintho 10:13 na Alma 13:28. Waulize jinsi wanavyodhani maandiko haya yanahusiana na changamoto zetu za kuepuka ponografia leo. Unaweza pia kuwaomba kupiga taswira kwamba wanaye rafiki ambaye amehangaika na ponografia na anataka kutubu. Ni nini wanapata kwenye maandiko ambacho kitamsaidia rafiki yao kwenye “Nyenzo Saidizi” na kwenye kurasa 1–4 za kijitabu Let Virtue Garnish Thy Thoughts? Ni nini kinaweza kumsaidia rafiki yao kuelewa kwamba askofu anaweza kumsaidia? (Ona Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, 12, 37).

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Unapofundisha kama Mwokozi alivyofundisha, washiriki wa akidi au darasa watatoa nafasi kwenye mioyo yao kwa ajili ya mbegu ya injili kupandwa, kuvimba na kukua. Unaweza kufanya nini ili kuwasaidia kutumia maandiko kuelewa nguvu na uzuri wa kuishi maisha ya wema?