Mafundisho na Maagano 2021
Juni 27. Ninawezaje Kujiandaa Sasa Kujenga Nyumba Inayolenga kwa Kristo? Mafundisho na Maagano 67–70


“Juni 27. Ninawezaje Kujiandaa Sasa Kujenga Nyumba Inayolenga kwa Kristo? Mafundisho na Maagano 67–70,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Juni 27. Ninawezaje Kujiandaa Sasa Kujenga Nyumba Inayolenga kwa Kristo?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
Yesu Kristo

Bwana Yesu Kristo, na Del Parson

Juni 27

Ninawezaje Kujiandaa Sasa Kujenga Nyumba Inayolenga kwa Kristo?

Mafundisho na Maagano 67–70

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, ni nani mgeni katika kata yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia kuhisi wamekaribishwa? Ni nini tunafanya ili kufanya muda wetu katika mikutano ya akidi au darasa kuwa wa maana?

  • Wajibu wetu au majukumu. Ni yapi baadhi ya majukumu na wajibu tulionao kama wavulana au wasichana? Tunawezaje kuyatimiza vyema?

  • Maisha yetu. Ni nini tunafanya ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo na kupokea nguvu Yake katika maisha yetu? Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja Kwake?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Mafundisho na Maagano 68 inahusisha ushauri kwa wazazi ambao kwa haraka haraka unaweza usionekane kuwafaa washiriki wa akidi au darasa (ona mistari 25–28). Hata hivyo, kwa sababu wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa familia zao za sasa na za baadaye, ushauri huu unaweza kuwasaidia sasa. Njia bora ya wao kujiandaa kuwa na nyumba inayolenga kwa Kristo ni “kusimama wima mbele za Bwana” (Mstari wa 28).

Je, ni baraka zipi zimekuja kwa familia yako kwa sababu umefuata mafundisho ya Mwokozi? Ni kwa jinsi gani washiriki wa akidi au darasa wanaweza kuzisaidia familia zao kujenga nyumba inayolenga kwa Kristo? Ili kujiandaa kufundisha, unaweza kurejea ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Nyumbani Ambapo Roho wa Bwana Anakaa” (Liahona, Mei 2019, 22–25) na “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org).

Picha
msichana akipiga piano

Tunaweza kuhisi upendo mkubwa katika familia zetu wakati tunapolenga nyumba zetu kwa Kristo.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia washiriki wa akidi yako au darasa lako kuona jinsi Mafundisho na Maagano 68:25–28 inavyotumika kwao, unaweza kuwaomba waandike maelezo mafupi ya jinsi wanavyotaka maisha ya familia zao za baadae yawe. Unaweza kuwaomba kushiriki kile walichokiandika kama watapenda. Kisha wanaweza kusoma Mafundisho na Maagano 68:25–28 na kutafuta mafundisho ya injili na kanuni ambazo zinaweza kuwasaidia kujenga familia adilifu sasa na baadaye. Shughuli hapa chini zinaweza kuwasaidia kuelewa jinsi ya kumfanya Kristo awe kitovu cha familia zao.

  • Aya ya saba ya “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” inazo kweli ambazo huweza kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuzilenga nyumba zao kwa mwokozi. Waalike wasome aya hii na kutambua mafundisho na kanuni ambazo zitasaidia familia kuwa yenye furaha. Unaweza kutaka kuandika haya ubaoni na kuwaomba wale unaowafundisha kujadili ni kwa nini kila mmoja ataisaidia familia kuwa yenye furaha. Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kutaka kushiriki jinsi walivyoona mafundisho haya na kanuni hizi zikitumika katika familia zao au za wengine. Wahimize kutafakari jinsi wanavyoweza kutumia angalau mojawapo ya kanuni hizi katika maisha yao sasa. Wahakikishie tena kwamba wanaweza kumfanya Yesu kristo kitovu cha maisha yao, bila kujali hali ya familia wanayotokea.

  • Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kujadili vitu vinavyomuweka Mwokozi kitovu cha nyumba zetu na vitu vinavyomzuia Yeye kuwa kitovu cha nyumba zetu. Unaweza kumuomba mtu mmoja mmoja au makundi madogo kupitia sehemu mojawapo ya ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Nyumbani Ambapo Roho wa Bwana Anakaa” (Liahona, Mei 2019, 22–25) ili kutafuta kanuni ambazo zinaweza kusaidia kufanya nyumba zetu ziwe zilizolenga zaidi kwa Kristo. Waalike washiriki wa akidi au darasa kushiriki kile walichojifunza na kuchagua kitu kimoja watakachokifanya ndani ya wiki ijayo ili kufanya nyumba zao zilenge zaidi kwa Yesu Kristo na mafundisho Yake.

  • Na labda unaweza kumuomba mshiriki mmoja au zaidi wa akidi au darasa kuimba au kusoma wimbo kuhusu nyumba na familia, kama vile “Home Can Be a Heaven on Earth” (Nyimbo za Kanisa, na. 298) au “Love Is Spoken Here” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 190). Wengine wanaweza kusikiliza kile kinachofundishwa na wimbo kuhusu kufanya nyumbani kuwa sehemu ya furaha. Waalike kushiriki uzoefu wakati walipohisi furaha kwa sababu walionyeshwa upendo au wakati waliposaidia kuongeza upendo katika nyumba zao.

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

  • Mosia 4:14–16; Mafundisho na Maagano 88:119; 121:41–46 (Jinsi ya kujenga nyumba yenye maadili)

  • Video “What Can I Do to Help Ease Family Tension?” kutoka kwenye Uso kwa Uso na Mzee Rasband, Dada Oscarson, na Kaka Owen (matangazo ya ulimwengu ya vijana, Jan. 20, 2016), “Two Brothers Apart,” “Through Small Things,” “More Diligent and Concerned at Home” ChurchofJesusChrist.org

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi alionyesha Upendo Wake kwa wengine kwa kutoa huduma. Watu waliongoka na maisha yalibadilishwa kupitia kazi Yake njema. Kama Kiongozi, ni kwa jinsi gani unaweza kuifuata sifa hii? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia vijana kutamani kufuata mfano wa Mwokozi wa huduma katika familia zao wenyewe?

Chapisha