“Julai 11. Kujua Kuhusu Mpango wa Wokovu Kunaathiri Vipi Maisha Yangu? Mafundisho na Maagano 76,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Julai 11. Je, Kujua Kuhusu Mpango wa Wokovu Kunaathiri Vipi Maisha Yangu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Julai 11
Kujua Kuhusu Mpango wa Wokovu Kunaathiri Vipi Maisha Yangu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):
-
Akidi au darasa letu. Je, ni nani anahitaji usaidizi wetu na sala zetu? Je, ni kipi tunaweza kufanya ili kuwasaidia? Je, ni nani tumualike katika shughuli ijayo?
-
Wajibu wetu au majukumu. Je, ni majukumu gani tumeshayatimiza? Je, ni majukumu gani tunahitaji kuyatoa? Je, ni kwa namna gani tumewaalika wengine kuja kwa Kristo, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaalika wengine hivi sasa?
-
Maisha yetu. Je, ni uzoefu gani wa hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu? Je, ni nini kinatokea katika maisha yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Baba yetu wa Mbinguni ameandaa mpango ambao unatusaidia sisi kupokea baraka za milele na kuwa kama Yeye. Anataka watoto Wake wote kujua kuhusu mpango huo, kwa hiyo Ameufunua mpango huo kupitia manabii katika miaka yote. Washiriki wa akidi au darasa walipokuwa wakisoma Mafundisho na Maagano 76 wiki hii, walijifunza kile Mungu alichofunua kuhusu mpango Wake kwa Joseph Smith na Sidney Rigdon, ikiwa ni pamoja na lengo kuu la Mwokozi katika mpango na utukufu tunaoweza kupokea katika maisha yajayo. Kama tu waaminifu, tunaweza kufanywa wakamilifu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, kupokea shangwe timilifu, na kuishi pamoja na Mungu daima.
Ni kwa jinsi gani kujua kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni kumeshawishi mtazamo wako juu ya maisha? Unawezaje kuisaidia akidi yako au darasa lako kuelewa ni baraka iliyoje kujua kuhusu mpango wa wokovu? Ili kujiandaa kufundisha, unaweza kusoma “Plan of Salvation” katika True to the Faith ([2004], 115–17) au ujumbe wa Mzee Dieter F. Uchtdorf “Tukio Lako Kuu” (Liahona, Nov. 2019, 86–90).
Jifunzeni Pamoja
Njia mojawapo ya kuanzisha mjadala na akidi yako au darasa lako kuhusu mpango wa wakovu ni kwa kumualika mtu kuandika ubaoni vichwa vya habari vifuatavyo, pamoja na mistari kutoka Mafundisho na Maagano 76: Maisha Kabla ya Kuja Hapa Duniani (Mistari 22–27), Maisha ya Hapa Duniani (Mistari 40–43), na Maisha Baada ya Kifo (Mistari 50–53, 59–62). Wape washiriki wa akidi au darasa dakika chache ili wapitie mistari hii kutafuta jukumu la Mwokozi katika kukamilisha mpango wa Baba wa Mbinguni. Waombe waandike chini ya kila kichwa cha habari kile walichokipata. Shughuli hapa chini zinaweza kuwasaidia kuelewa vyema jinsi mpango wa Baba wa Mbinguni unavyobariki maisha yao.
-
kufanya mapitio ya baadhi ya majina ya mpango wa Baba wa Mbinguni kunaweza kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuuelewa mpango vyema. Wanaweza kupitia maandiko katika doti ya kwanza kwenye “Nyenzo Saidizi” na kuandaa orodha ya baadhi ya majina ya mpango wa Mungu. Je, majina haya hutufundisha nini kuhusu mpango? Kwa mfano, ni kwa jinsi gani mpango huu hutupatia furaha, sasa na milele zote? Vifungu hivi vinatufundisha nini kuhusu jukumu la Mwokozi katika mpango? Unaweza kuonyesha video “Our Eternal Life” au “Men’s Hearts Shall Fail Them” (ChurchofJesusChrist.org) na waalike wale unaowafundisha kuongelea kuhusu nyakati ambazo walihisi shukrani kwa ajili ya mpango wa Baba wa Mbinguni.
-
Fikiria kuwaalika wale unaowafundisha kujadili jinsi watakavyomjibu rafiki aliyeuliza maswali yafuatayo kuhusu mpango wa wokovu: Tulitoka wapi? Kwa nini tuko hapa? Tunaenda wapi baada ya maisha haya? Waalike watumie taarifa kwenye “Plan of Salvation” katika True to the Faith (kurasa 115–17) na nyenzo kwenye “Nyenzo Saidizi” kuandaa jibu kwa ajili ya mojawapo ya maswali. Ni kwa namna gani tumeimarishwa kwa kujua majibu ya maswali haya?
-
Washiriki wa akidi au darasa wanajifunza kweli za injili kwa undani zaidi wanapopewa fursa za kufundisha. Kabla ya kukutana, waombe washiriki kadhaa wa akidi au darasa kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki muhtasari mfupi wa kile wanachokijua kuhusu kipengele cha mpango wa wokovu. Wanaweza kutumia mihutasari inayopatikana kwenye “The Plan of Salvation,” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel ([2019], 48–53). Inaleta tofauti gani kujua kuhusu mpango wa wokovu?
Tenda kwa Imani
Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.
Nyenzo Saidizi
-
2 Nefi 11:5; Alma 12:30; 34:9; 41:2; 42:8, 13–15; Musa 6:59–62 (Majina ya mpango wa Baba wa Mbinguni)
-
Mafundisho na Maagano 38:1–3; 138:53–56; Musa 4:1–4; Ibrahimu 3:21–24 (Maisha kabla ya kuja duniani)
-
2 Nefi 2:19–21, 25; Alma 5:15–16; 34:32; Ibrahimu 3:25–26 (Maisha ya hapa duniani)
-
Yohana 14:1–2; Alma 11:42–45; Mafundisho na Maagano 76:39–43, 89–93 (Maisha baada ya kifo)