“Machi 28. Kwa nini Ninahitaji Upatanisho wa Yesu Kristo? Mafundisho na Maagano 29,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Machi 28. Kwa nini Ninahitaji Upatanisho wa Yesu Kristo?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Machi 28
Kwa nini Ninahitaji Upatanisho wa Yesu Kristo?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):
-
Akidi au darasa letu. Tunaweza kufanya nini ili kujenga umoja miongoni mwa washiriki wa akidi au darasa? Je, ni malengo gani tunahitaji kuyashughulikia pamoja?
-
Wajibu wetu au majukumu. Tunafanya nini ili kushiriki injili? Ni uzoefu upi tumeupata wakati tunafanya kazi ya hekalu na historia ya familia?
-
Maisha yetu. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu? Ni nini kimetutia moyo katika kujifunza kwetu maandiko wiki hii?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Rais Ezra Taft Benson alifundisha: “Kama vile mtu hawezi kuwa na hamu ya chakula mpaka awe na njaa, vivyo hivyo hawezi kutamani wokovu wa Kristo mpaka ajue kwa nini anamhitaji Kristo. Hakuna anayejua kikamilifu na ipasavyo kwa nini anamhitaji Kristo mpaka atakapoelewa na kukubali mafundisho ya Anguko na matokeo yake juu ya watu wote” (“The Book of Mormon and the Doctrine and Covenants,” Ensign, Mei 1987, 85). Uliposoma Mafundisho na Maagano 29 wiki hii, unaweza kuwa umetambua maelezo ya Mwokozi ya Anguko na jinsi tunavyookolewa kutokana nalo. Ni kwa jinsi gani ulipata ushuhuda wa Yesu Kristo na jukumu lake kama Mwokozi na Mkombozi wako? Fikiria kuhusu jinsi kuimarisha ushuhuda wa washiriki wa akidi au darasa kuhusu Yeye kutakavyowabadili. Unapojiandaa, fikiria kusoma “Agency and the Fall of Adam and Eve,” “The Atonement of Jesus Christ,” na “The Divine Mission of Jesus Christ” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel ([2019], 49–52, 60–61).
Jifunzeni Pamoja
Ili kutambulisha mjadala wa leo, unaweza kuwaalika wale unaowafundisha kuorodhesha ubaoni kitu chochote wanachojua kuhusiana na Anguko la Adamu na Eva. Kwa mfano, wanajifunza nini kuhusu Anguko kutoka kwenye Mafundisho na Maagano 29:36–50? Ni ushahidi gani wa Anguko tunaouona miongoni mwetu? Shughuli zifuatazo hapa chini zitaisaidia akidi yako au darasa lako kugundua jinsi upatanisho wa Yesu Kristo unavyotusaidia kushinda matokeo ya Anguko.
-
Ili kuelewa vyema anguko la Adamu na Eva, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kusoma “Fall” katika True to the Faith (56–59) au “Agency and the Fall of Adam and Eve” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel (49–50). Waalike wafikirie kwamba rafiki aliwauliza, “Kwa nini ninamhitaji Yesu Kristo?” Waalike wafundishane wao kwa wao katika jozi kuhusu jinsi watakavyojibu swali hilo kulingana na kile walichojifunza kutoka kwenye usomaji wao.
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kujifunza kutoka katika maandiko juu ya kwa nini wanahitaji Upatanisho wa Yesu Kristo? Njia mojawapo ni kuandika ubaoni baadhi ya marejeleo ya maandiko kutoka kwenye “Nyenzo Saidizi” na kisha andika kauli fupi za marejeleo hayo katika vipande vya karatasi. Mpatie kila mshiriki wa akidi au darasa kipande kimoja cha karatasi. Waalike wasome marejeleo ya maandiko yaliyoandikwa ubaoni na kutafuta mojawapo linaloendana na kauli zao fupi. (Baadhi ya kauli zinarejelea andiko zaidi ya moja.) Mwalike kila mshiriki wa akidi au darasa kusoma kwa sauti kifungu cha andiko ambacho kimefanana na kauli yao na kushiriki kile walichojifunza kuhusu kwa nini tunahitaji Upatanisho wa Mwokozi.
-
Waalike washiriki wa akidi au darasa kwa faragha kujibu maswali kama yafuatayo: Ni kwa jinsi gani nimebarikiwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo? Je, Mwokozi anahitaji nibadili nini ili niweze kupokea kikamilifu baraka za Upatanisho Wake? Kisha waombe wajadili swali la kwanza kwa pamoja. Wanaweza kurejea “The Atonement of Jesus Christ” na “The Divine Mission of Jesus Christ” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel (51–52, 60–61) na video moja au zaidi katika “Nyenzo Saidizi.” Waalike kushiriki kile walichojifunza.
Tenda kwa Imani
Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.
Nyenzo Saidizi
-
Mafundisho na Maagano 19:16–19 (Yesu Kristo alilipa deni la dhambi zetu ili kwamba tusiteseke kama tutatubu)
-
2 Nefi 9:6–16; Alma 42:6–9 (Yesu Kristo hutuokoa kutoka kifo na jehanamu)
-
2 Nefi 2:5–10; Helamani 14:15–17 (Tunaweza kurudi kwa Mungu kupitia kwa Yesu Kristo pekee)
-
Mosia 3:7; Alma 7:11–13 (Kwa sababu Kristo alijichukulia juu Yake masumbuko na dhambi zetu, Anajua jinsi ya kutusaidia)
-
Musa 5:10–12 (Kwa sababu Kristo alitukomboa kutoka kwenye Anguko, tunaweza kupata shangwe)
-
Walter F. González, “Mguso wa Mwokozi,” Liahona, Nov. 2019, 90–92
-
(Video) “Where Justice, Love, and Mercy Meet,” “Why We Need a Savior,” “The Atonement Enables Us”, ChurchofJesusChrist.org