Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 26. Kwa nini Ni Muhimu Kwamba Funguo za Ukuhani Ziko Duniani Leo? Mafundisho na Maagano 106–108


“Septemba 26. Kwa nini Ni Muhimu Kwamba Funguo za Ukuhani Ziko Duniani Leo? Mafundisho na Maagano 106–108,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Septemba 26. Kwa nini Ni Muhimu Kwamba Funguo za Ukuhani Ziko Duniani Leo?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

maelezo ya sanamu ya Petro akiwa ameshikilia funguo

Septemba 26

Kwa nini Ni Muhimu Kwamba Funguo za Ukuhani Ziko Duniani Leo?

Mafundisho na Maagano 106–108

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Tunaweza kufanya nini ili kujenga umoja miongoni mwa washiriki wa akidi au darasa? Je, ni malengo gani tunahitaji kuyashughulikia kwa pamoja?

  • Wajibu wetu au majukumu. Tunafanya nini ili kushiriki injili? Ni uzoefu upi tumeupata wakati tunafanya kazi ya hekalu na historia ya familia?

  • Maisha yetu. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu? Ni nini kimetutia moyo katika kujifunza kwetu maandiko wiki hii?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

“Funguo za ukuhani,” Mzee Gary E. Stevenson alifundisha, “hufungua baraka, vipawa na nguvu za mbinguni kwa ajili [yetu]” (“Funguo na Mamlaka ya Ukuhani Viko Wapi?Liahona, Mei 2016, 32). Yesu Kristo anashikilia funguo zote za ukuhani, na Aliwapa mamlaka wajumbe wa mbinguni kumtunukia Joseph Smith funguo za ukuhani. Hivi leo washiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wanashikilia funguo hizi (ona Mafundisho na Maagano 90:3–4, 6; 107:35; 132:7). Funguo hizi ni mamlaka ambayo Mungu ameyatoa kwa viongozi wa ukuhani ili kuongoza matumizi ya ukuhani Wake hapa duniani.

Unaposoma Mafundisho na Maagano 107 wiki hii, fikiria ni jinsi gani Mungu anaweza kukubariki wewe na wale unaowafundisha kupitia ukuhani Wake. Je, ni nini unapata katika sehemu hii ambacho ni cha muhimu kwa washiriki wa akidi au darasa kukifahamu? Unapojiandaa kufundisha, unaweza kurejea ujumbe wa Mzee Gary E. Stevenson ulionukuliwa hapo juu na “Priesthood Keys” katika True to the Faith ([2004], 126–27).

mvulana akipitisha sakramenti

Baraka kuu za kiroho zipo kwa ajili yetu kupitia funguo za ukuhani.

Jifunzeni Pamoja

Mafundisho na Maagano 107 inaweza kusadia kujibu swali lisemalo “Ni baraka zipi tunazipokea kupitia ukuhani na huduma ya viongozi wa ukuhani?” Pengine washiriki wa akidi au darasa wanaweza kutafuta baadhi ya majibu katika mistari 18–23, 85–89. Ili kuwasaidia kuelewa vyema jinsi ukuhani na viongozi wa ukuhani wanavyobariki maisha yetu, tumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo.

  • Unaweza kuanza mjadala kuhusu funguo za ukuhani kwa kumualika mshiriki wa akidi au darasa kuja akiwa amejiandaa kushiriki hadithi ya Rais Spenser W. Kimball alipotembelea kanisa huko Denmark, iliyosimuliwa na Rais Boyd K. Packer katika ujumbe wake “Thenashara” (Liahona, Mei 2008, 83–87; ona pia video ya “The Restoration of Priesthood Keys” [ChurchofJesusChrist.org]). Pia unaweza kuiomba akidi yako au darasa lako kusoma kwa pamoja sehemu ya “Priesthood Keys” katika True to the Faith (kurasa 126–27). Wape muda wa kufundishana wao kwa wao katika jozi kuhusu funguo za ukuhani ni nini, kulingana na kile walichojifunza. Ni baraka zipi tumezipokea kupitia huduma ya wale wanaoshikilia funguo za ukuhani?

  • Unaweza kuhitaji kushiriki hadithi ya Mzee Gary E. Stevenson kuhusu kupoteza funguo zake kutoka katika aya sita za mwanzo za ujumbe wake “Funguo na Mamlaka ya Ukuhani Viko Wapi?” (au onyesha video ya “Where Are the Keys?” [ChurchofJesusChrist.org]). Unaweza kuonyesha baadhi ya funguo na kuwaalika akidi au darasa lako kushiriki jinsi funguo hizo zinavyofanana na funguo za ukuhani. Wale unaowafundisha wanaweza kurejea na kujadili maandiko yaliyotolewa na Mzee Stevenson (Joseph Smith—Historia ya 1:68–72; Mafundisho na Maagano 110:11–16), ambayo huelezea funguo za ukuhani zikiwa zimekabidhiwa duniani. Unaweza kuwaalika washiriki wa akidi au darasa kila mmoja kuchagua mojawapo ya maandiko yafuatayo na kushiriki kwa ufupisho wa sentensi moja kile walichojifunza kuhusu nguvu na baraka tunazopokea kupitia funguo za ukuhani: Mathayo 16:18–19; Mafundisho na Maagano 27:12; 65:2; 84:19–20. Kwa nini ni muhimu kwamba funguo za ukuhani ziko duniani leo?

    14:6
  • Unaweza kumpa kila mshiriki wa akidi au darasa lako ufunguo wa karatasi na kumpangia kila mtu kusoma sehemu ya II, III, IV, au V ya ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Funguo na Mamlaka ya Ukuhani” (Liahona, Mei 2014, 49–52). Waalike waandike katika ufunguo kile walichojifunza kuhusu ukuhani na kisha washiriki kile walichoandika. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zimechangia jinsi tunavyohisi kuhusu viongozi wetu wa akidi au darasa na majukumu tunayopokea kutoka kwao?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

  • Russell M. Nelson, “Hazina za Kiroho,” Liahona, Nov. 2019, 76–79.

  • Priesthood Keys,” katika General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 3.4.1

  • Video “Learn Your Duty,” “The Priesthood, an Opportunity to Serve,” ChurchofJesusChrist.org

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi aliwaita na kuwasimika viongozi wa kuongoza na kusimamia Kanisa Lake (ona Mathayo 10:1–5). Unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kuhisi shukrani kwa ajili ya wale walioitwa kuwatumikia na kuwasaidia?

Ona pia video “Asking Follow-up Questions” (ChurchofJesusChrist.org).