Mafundisho na Maagano 2021
Septemba 12. Tunawezaje Kukabiliana na Dhiki kwa Imani? Mafundisho na Maagano 98–101


“Septemba 12. Tunawezaje Kukabiliana na Dhiki kwa Imani? Mafundisho na Maagano 98–101,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Septemba 12. Tunawezaje Kukabiliana na Dhiki kwa Imani?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
Watakatifu wakikimbia kundi la wavamizi

C. C. A. Christensen (1831–1912), Watakatifu Wakifukuzwa kutoka Wilaya ya Jackson Missouri, c. 1878, tempera kwenye kitambaa cha pamba, inchi 77 ¼ × 113. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, zawadi ya wajukuu wa C. C. A. Christensen, 1970

Septemba 12

Tunawezaje Kukabiliana na Dhiki kwa Imani?

Mafundisho na Maagano 98–101

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, ni nani huhitaji usaidizi wetu na sala zetu? Je, tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia? Je, ni nani tumualike katika shughuli ijayo?

  • Wajibu wetu au majukumu. Je, ni majukumu gani tumeshayatimiza? Je, ni majukumu gani tunahitaji kuyatoa? Je, ni kwa namna gani tumewaalika wengine kuja kwa Kristo, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaalika wengine hivi sasa?

  • Maisha yetu. Je, ni uzoefu gani wa hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu? Je, ni nini kinatokea katika maisha yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Maneno ya Mungu katika Mafundisho na Maagano 98 na 101 yalitoa faraja kwa Watakatifu ambao walikuwa wanapitia majaribu makali huko Missouri katika miaka ya 1830. Wakati majaribu yetu yanaweza kuwa tofauti na yale ya waumini wa mwanzo wa Kanisa, sote tunapitia dhiki wakati wa maisha haya ya kifo, na kukabiliana na dhiki kwa uaminifu kunaweza kutusaidia kukua kiroho na kuwa zaidi kama Yesu Kristo.

Ni kwa jinsi gani kumgeukia Bwana nyakati za dhiki kumekuimarisha na kukuza mahusiano yako na Yesu Kristo? Ni changamoto zipi na majaribu gani ambayo washiriki wa akidi au darasa lako wanayapitia, na ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kupata nguvu kwa Mwokozi? Kukusaidia katika kujiandaa kufundisha kuhusu dhiki, unaweza kurejea ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Kujeruhiwa” (Liahona, Nov. 2018, 83–86) na “Adversity” katika True to the Faith ([2004], 8–11).

Picha
mvulana akiwa nje

Tunaweza kupata amani katika nyakati za dhiki kwa kumgeukia Mwokozi.

Jifunzeni Pamoja

Kila mshiriki wa akidi au darasa lako anakabiliana na changamoto zake mwenyewe. Ni Faraja gani unahisi wanaweza kuipata katika Mafundisho na Maagano 98:1–3? Unaweza kutumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo kuwasaidia kuelewa jinsi ya kuvumilia dhiki wakiwa na imani kwa Bwana.

  • Maandiko yamejaa mifano mingi ya watu ambao kwa imani walivumilia majaribu. Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kujifunza jinsi ya kuvumilia dhiki kwa kusoma baadhi ya mifano hii (ona baadhi katika “Nyenzo Saidizi”). Kila mmoja anaweza kuchagua mojawapo ya kifungu cha maandiko na kufupisha uzoefu wa mtu huyo kwa ajili ya akidi au darasa. Je, ni utambuzi gani tunaupata kuhusu kwa nini tunapata dhiki? Je, tunajifunza nini kuhusu jinsi ya kuvumilia dhiki kwa imani? Waalike washiriki wa akidi au darasa kila mmoja kuandika jaribu ambalo wao au wapendwa wao wanapitia na kutafakari jinsi wanavyoweza kupokea nguvu ya Mwokozi kuwasaidia katika majaribu haya.

  • Kujifunza kuhusu baadhi ya visababishi vya dhiki na kile tunachoweza kujifunza kutokana na majaribu yetu, mnaweza kusoma pamoja aya mbili za mwanzo kwenye “Adversity” katika True to the Faith (ukurasa wa 8). Waombe washiriki wa akidi au darasa kushiriki kile walichojifunza. Kisha kila mtu anaweza kurejea mojawapo ya sehemu tatu zilizobakia kwenye “Adversity” na kujiandaa kuwafundisha wengine kile walichojifunza, ikijumuisha jinsi Mwokozi anavyoweza kutusaidia nyakati za majaribu. Wahimize kushiriki uzoefu binafsi unaohusiana na kile walichokisoma kama wanahisi vyema kufanya hivyo.

  • Njia mojawapo ya kuanzisha mjadala kuhusu dhiki ni kwa kuchora mstari katikati ya ubao na kuandika Kwa nini tunapitia dhiki? katika upande mmoja na Ni kwa jinsi gani tunaweza kukabiliana na dhiki kwa imani? Katika upande mwingine. Kila mshiriki wa akidi yako au darasa lako anaweza kusoma mojawapo ya vipengele kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Kujeruhiwa,” akitafuta majibu ya maswali yaliyoko ubaoni. Tunajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Andersen?

  • Mzee Stanley G. Ellis alitumia mifano ya vifaranga vya kuku na vipepeo kufundisha kuhusu dhiki katika ujumbe wake “Je, Tunamwamini Yeye? Ugumu Ni Mzuri” (Liahona, Nov. 2017, 112–14). Unaweza kuonyesha picha ya kifaranga akitotolewa au kipepeo akitoka kwenye kifukofuko na kujadili kile Mzee Ellis alichofundisha. Wale unaowafundisha kisha wanaweza kufanya kazi pamoja katika jozi kurejea mahubiri ya Mzee Ellis. Kila jozi inaweza kuorodhesha kila kitu wanachoweza kupata kwenye kile alichofundisha kuhusu kwa nini tunapitia dhiki na ni kwa jinsi gani tukabiliane nayo. Ni kwa jinsi gani kuvumilia kwa uaminifu katika nyakati za dhiki kumetusaidia kuwa karibu na Mwokozi?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi kwa binafsi Aliwajua wale Aliowafundisha—na Alijua wangekuwa watu gani. Walipopitia magumu, hakuwakatia tamaa lakini aliendelea kuwapenda. Ni magumu gani ambayo vijana wanapitia? Ni kwa jinsi gani unaweza kuonyesha upendo na msaada?

Chapisha