Mafundisho na Maagano 2021
Oktoba 10. Je, Ni Kwa Jinsi Gani Naweza Kuwa Nimeongoka kikamilifu kwa Bwana? Mafundisho na Maagano 111–114


“Oktoba 10. Je, Ni Kwa Jinsi Gani Naweza Kuwa Nimeongoka kikamilifu kwa Bwana? Mafundisho na Maagano 111–114,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Oktoba 10. Je, Ni Kwa Jinsi Gani Naweza Kuwa Nimeongoka kikamilifu kwa Bwana?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
wasichana wakitabasamu

Oktoba 10

Je, Ni Kwa Jinsi Gani Naweza Kuwa Nimeongoka kikamilifu kwa Bwana?

Mafundisho na Maagano 111–114

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha, pamoja na kushauriana kuhusu shughuli maalumu ya akidi au darasa, mnaweza kutaka kujadili misukumo na dhima kutoka kwenye mkutano mkuu. Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia.

  • Ni dhima zipi au jumbe zipi zimejitokeza bayana kwetu?

  • Tumehisi kushawishika kufanya nini kwa sababu ya kile tulichojifunza au kuhisi?

  • Tunahitaji kufanya nini kama akidi au darasa ili kuufanyia kazi ushauri tuliousikia katika mkutano mkuu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Ili kuongoka kikamilifu kwa Yesu Kristo, lazima tumuamini Yeye na kutii amri Zake—hata wakati changamoto ngumu zinapojaribu uongofu wetu. Mwaka 1837, baadhi ya waumini wa Kanisa, wakiwemo baadhi ya washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, walipoteza shuhuda zao na wakageuka dhidi ya Nabii Joseph Smith. Thomas B. Marsh alikuwa Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kwa wakati huo. Wakati wewe na familia yako mnaposoma Mafundisho na Maagano 112 wiki hii, mnaweza kugundua ushauri ambao Bwana aliutoa kumsaidia Thomas B. Marsh kuimarisha uongofu wake (ona hasa mistari 10–26). Je, ushauri huu unakufundisha nini kuhusu kuwa mwongofu zaidi kwa Mwokozi?

Unawezaje kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kupokea ahadi ya Mwokozi kwamba “wataongolewa, nami nitawaponya”? (Mafundisho na Maagano 112:13). Ni uzoefu gani unaweza kuushiriki? Unapotafakari maswali haya, fikiria kurejea ujumbe wa Rais Bonnie H. Cordon “Amini katika Bwana na Wala Usitegemee Njia Zako” (Liahona, Mei 2017, 6–9) na “Conversion” katika True to the Faith ([2004], 40–43).

Picha
mvulana akisoma maandiko

Maandiko ni nguvu kuu pale tunapotafuta kuwa waongofu kikamilifu.

Jifunzeni Pamoja

Je, washiriki wa akidi au darasa lako wanajua inamaanisha nini kuwa muongofu kwa Yesu Kristo? Je, wanajua jinsi ya kuwa waongofu kikamilifu? Waalike kutafakari maswali haya wanaporejea Mafundisho na Maagano 112:10–26. Je, tunawezaje kubakia waongofu kwa Yesu Kristo hata katika hali zenye changamoto? Unaweza kutumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo kusaidia akidi yako au darasa lako kuimarisha uongofu wao kwa Mwokozi.

  • Alma 32:27–43 inaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa jinsi ya kuimarisha imani yao na kuwa waongofu kikamilifu kwenye injili ya Yesu Kristo. Na huenda unaweza kuwagawanya washiriki wa akidi au darasa katika makundi na kuliomba kila kundi kusoma mistari hii na kujadili inafundisha nini kuhusu imani na uongofu. Omba kila kikundi kushiriki kile walichojifunza. Unaweza kuhimiza majadiliano kwa kuuliza maswali kama haya: Kwa nini mbegu inayokua hadi kuwa mti ni kielelezo kizuri cha uongofu? Inamaanisha nini “kujaribu juu ya maneno ya [Mungu]”? (mstari wa 27). Inamaanisha nini “kulisha mti”? (mstari wa 41). Na tutatambua vipi kwamba mbegu ya uongofu “imevimba, na kumea, na kuanza kukua” ndani yetu? (mstari wa 30). Wape washiriki wa akidi au darasa muda wa kutafakari kile wanachotakiwa kufanya ili kulisha uongofu wao wenyewe kwa Yesu Kristo.

  • Kuna nguvu nyingi katika ulimwengu ambazo zinapinga uongofu wetu kwa Yesu Kristo. Kusoma Helamani 5:12 kunaweza kuwafundisha washiriki wa akidi au darasa jinsi ya kubakia imara bila kujali upinzani. Inamaanisha nini “kujenga msingi wako” juu ya mwamba wa Yesu Kristo? Unaweza kumpangia kila mtu sehemu ya ujumbe wa Mzee Quentin L. Cook “Misingi ya Imani” (Liahona, Mei 2017, 127–31) na kuwaomba watafute mifano na ushauri ambao utawasaidia kujenga msingi wao kwa Mwokozi.

  • Je, unaweza kufikiria njia ya kibunifu ili kuonyesha kwa mfano kanuni iliyofundishwa na Rais Bonnie H. Cordon katika ujumbe wake “Amini katika Bwana na Wala Usitegemee Njia Zako”? Kwa mfano, unaweza kuigawa akidi yako au darasa lako katika makundi na kulipa kila kundi changamoto ya kujenga jengo refu juu ya uso ulio tenge kwa kutumia matofali au vitu vingine. Kisha Jadili jinsi hili linavyohusiana na ujumbe wa Rais Cordon. Akidi au darasa kisha wanaweza kuuchunguza ujumbe kwa ajili ya mapendekezo ya jinsi ya kuweka maisha yetu yakiwa yamelenga juu ya Yesu Kristo. Ni uzoefu gani tunaoweza kuushiriki wa wakati tulipotegemea uelewa wetu sisi wenyewe au pale tulipomwamini Mwokozi?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi alisema, “Mafundisho yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka” (Yohana 7:16). Alifundisha mafundisho ambayo Alijifunza kutoka kwa Baba Yake. Ni kwa jinsi gani utahakikisha kwamba unafundisha mafundisho ya kweli? (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi [2016], 20–21.)

Chapisha