“Oktoba 24. Ninawezaje Kupata ‘Nguvu za Mbinguni’ katika Maisha Yangu? Mafundisho na Maagano 121–123,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Oktoba 24. Ninawezaje Kupata ‘Nguvu za Mbinguni’ katika Maisha Yangu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Oktoba 24
Ninawezaje Kupata “Nguvu za Mbinguni” katika Maisha Yangu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):
-
Akidi au darasa letu. Je, ni nani mgeni katika kata yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia kuhisi wamekaribishwa? Ni nini tunafanya ili kufanya muda wetu katika mikutano ya akidi au darasa kuwa wa maana?
-
Wajibu wetu au majukumu. Ni yapi baadhi ya majukumu na wajibu tulionao kama wavulana na wasichana? Tunawezaje kuyatimiza vyema?
-
Maisha yetu. Ni nini tunafanya ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo na kupokea nguvu Zake katika maisha yetu? Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja Kwake?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Mamlaka ya ukuhani na nguvu ya ukuhani sio vitu sawa. Mtu anaweza kupokea mamlaka ya ukuhani kupitia kuwekewa mikono—wanaume wanaweza kutawazwa katika ofisi ya ukuhani, na wote wanaume kwa wanawake wanaweza kusimikwa kwa ajili ya wito. Lakini nguvu za ukuhani—Nguvu za Mungu, au “nguvu za mbinguni”—zinaweza kutumika tu “kwa kanuni za haki” (Mafundisho na Maagano 121:36, na wote wanaume kwa wanawake wanaweza kutumia nguvu hii. Kama tunahitaji huduma yetu kuwa yenye nguvu kwa wengine na yenye kubadili maisha, tunahitaji kuwa wenye kustahili kwa ajili ya kualika nguvu za mbinguni.
Je, washiriki wa akidi yako au darasa wanajua jinsi ya kupata nguvu za ukuhani? Je, maisha yao na huduma yao vingekuwa na tofauti kiasi gani kama wangekuwa na uelewa huo? Tafakari maswali haya unaposoma Mafundisho na Maagano 121. Pia itakuwa vizuri kusoma jumbe mbili kutoka kwa Rais Russell M. Nelson. Ujumbe mmoja umeelekezwa kwa wenye ukuhani—“Gharama ya Nguvu za Ukuhani” (Liahona, Mei 2016, 66–69). Na mwingine umeelekezwa kwa akina dada—“Hazina za Kiroho” (Liahona, Nov. 2019, 76–79).
Jifunzeni Pamoja
Kwa kuanza mjadala kuhusu nguvu za ukuhani, unaweza kuwaomba washiriki wa akidi au darasa kushiriki kitu walichojifunza kuhusu nguvu hii kutoka kwenye usomaji wao wa Mafundisho na Maagano 121 wiki hii. Kama itasaidia, unaweza kupendekeza kwamba wapitie kwa haraka mistari 34–46 kutafuta kila mahali neno nguvu lilipotumika na kisha washiriki kile walichojifunza. Unaweza kutumia shughuli zifuatazo kuwasaidia washiriki wa akidi yako au darasa lako kuelewa vyema jinsi wanavyoweza kupata nguvu ya ukuhani wa Mungu katika maisha yao.
-
Itakuwa vyema kutofautisha jinsi “nguvu na “ushawishi” vinavyotumika katika ulimwengu na kile ambacho Bwana amefundisha katika sehemu ya 121 kuhusu nguvu za ukuhani zinavyotumika. Unaweza kuandaa jedwali lenye safu mbili ubaoni lenye vichwa vya habari Nguvu za Kiulimwengu na Nguvu za Mbinguni. Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kujaza jedwali hilo kwa maneno na vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 121:34–46. Je, ni jinsi gani uelewa wa mistari hii unaathiri jinsi tunavyotafuta kuwashawishi wengine kutenda mema, ikiwa ni pamoja na marafiki zetu, wanafamilia, na wale tunaowatumikia na kuwahudumia? Kulingana na mistari hii, ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu hutusaidia kuwashawishi wengine kwa njia ya uadilifu?
-
Kuwasaidia wenye Ukuhani wa Haruni kujifunza jinsi ya kupata nguvu katika huduma yao ya ukuhani, unaweza kuonyesha vitu mbalimbali na kuwaomba washiriki wa akidi kubashiri ni thamani kiasi gani kila kimoja kinabeba. Ni kwa nini baadhi ya vitu vina thamani kubwa kuliko vingine? Ni vitu gani katika maisha yetu vina thamani kubwa, na ni gharama kiasi gani tunapaswa “kuilipa” ili kuvipata? Washiriki wa akidi kisha wanaweza kutafuta ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Gharama ya Nguvu za Ukuhani,” wakitafuta gharama aliyosema kwamba tunapaswa kuilipa ili kupokea nguvu za ukuhani. Ni kwa jinsi gani maisha yetu na maisha ya wengine yanaathirika tunapotumikia kwa nguvu zaidi ya Mwokozi?
-
Ili kuwasaidia wasichana kuelewa jinsi ya kupata nguvu za ukuhani, unaweza kuwaomba kufikiria nyakati ambazo walihisi nguvu za Mungu katika maisha yao. Elezea kwamba nguvu ya ukuhani ni nguvu ya Mungu. Wanaweza kutafuta ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Hazina za Kiroho” juu ya kweli kuhusu wanawake na nguvu ya ukuhani. Ni kitu gani Rais Nelson amewaomba wanawake wa Kanisa kufanya ili “kwa uhuru kuvuta nguvu za Mwokozi”? (ukurasa wa 77; ona hasa aya nne zinazoanzia na “Kila mwanamke na kila mwanamume”). Ni lini tumevuta nguvu hii ili kubariki maisha yetu na maisha ya wengine? Ni kipi Mafundisho na Maagano 121:39–43 inatufundisha kuhusu jinsi ya kutenda kwa kutumia nguvu ya Bwana katika maisha yetu?
Tenda kwa Imani
Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.
Nyenzo Saidizi
-
Russell M, Nelson, “Kuvuta Nguvu ya Yesu Kristo kwenye Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2017, 39–42.
-
David A. Bednar, “Nguvu za Mbinguni,” Liahona, Mei 2012, 48–51