Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 14. Kwa nini Ndoa ya Milele Ni ya Muhimu? Mafundisho na Maagano 129–132


“Novemba 14. Kwa nini Ndoa ya Milele Ni ya Muhimu? Mafundisho na Maagano 129–132,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Novemba 14. Kwa nini Ndoa ya Milele Ni ya Muhimu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

wanandoa wapya wakiwa mbele ya hekalu

Novemba 14

Kwa nini Ndoa ya Milele Ni ya Muhimu?

Mafundisho na Maagano 129–132

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, akina nani wanahitaji usaidizi wetu na sala zetu? Je, ni kipi tunaweza kufanya ili kuwasaidia? Je, ni nani tunaweza kumualika katika shughuli ijayo?

  • Wajibu wetu au majukumu. Je, ni majukumu gani tumeyatimiza? Je, ni majukumu gani tunahitaji kuyatoa? Je, ni kwa jinsi gani tumewaalika wengine kuja kwa Kristo, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaalika wengine hivi sasa?

  • Maisha yetu. Je, ni uzoefu gani wa hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu? Je, ni nini kinatokea katika maisha yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana?

Kama itafaa, tamatisha somo kwa kufanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Wakati washiriki wa akidi yako au darasa lako wanapopata shuhuda za ndoa ya hekaluni wakati wakiwa wadogo, watakuwa ni wenye hamu kubwa na kujiandaa kwa baraka hii kuu. Katika mpango wa furaha wa Baba yetu wa Mbinguni, agano la milele la ndoa ni la muhimu kwa ajili ya kuinuliwa (ona Mafundisho na Maagano 131:1–4). Lakini ndoa ya hekaluni sio tu kuhusu kile tutakachopokea katika maisha yajayo—lakini pia inaweza kuleta baraka kuu katika maisha haya. Kwa mfano, maagano matakatifu na Mungu yanaweza kushawishi jinsi mume au mke wanavyoyachukulia mahusiano yao. Na mwanamume na mwanamke waliounganishwa pamoja katika maisha haya na milele zote wana uhakika kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, mahusiano yao yataendelea milele kama watabakia wakweli katika maagano yao.

Unawezaje kuwasaidia washiriki wa akidi yako au darasa lako kuhisi hamu kubwa ya kuunganishwa hekaluni? Ili kujiandaa kwa ajili ya kufundisha kuhusu ndoa ya hekaluni, unaweza kuchunguza makala “About a Temple Sealing” kwenye temples.ChurchofJesusChrist.org au soma “Marriage” katika True to the Faith ([2004], 97–101).

wazazi wakiwa wamewabeba watoto wao

Familia zinaweza kuunganishwa milele kupitia ibada za hekaluni.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwapatia washiriki wa akidi au darasa fursa ya kushiriki kile ambacho wamekuwa wakijifunza katika maandiko wiki hii, unaweza kuandika ubaoni swali kama Kwa nini ndoa ya milele katika hekalu la Mungu ni ya Muhimu? Washiriki wa akidi au darasa kisha wanaweza kutafuta rejeleo la mstari wanaosoma katika Mafundisho na Maagano 129–32 ambalo linaweza kusaidia kujibu swali na kuandika rejeleo mbele ya swali. (Kama itasaidia, unaweza kuwaelekeza kwenye Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:13–19.) Someni pamoja baadhi ya marejeleo, na jadilini ni nini yanafundisha. Unaweza kutumia shughuli yoyote kati ya zifuatazo kuwasaidia vijana kuelewa vyema umuhimu wa ndoa ya hekaluni.

  • Kwa sababu ndoa ya hekaluni ni ya kipekee katika injili iliyorejeshwa, wale unaowafundisha wanaweza kuwa na fursa za kuielezea kwa watu ambao hawaifahamu. Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kufanya hili, unaweza kuwaalika kuwa na taswira ya rafiki ambaye anajiuliza ni kwa nini Watakatifu wa Siku za Mwisho huamini kwamba ndoa ya hekaluni ni ya muhimu sana. Waombe wasome maandiko katika “Nyenzo Saidizi,” “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org), au kurasa 97–98 katika True to the Faith. Wanaweza kutafuta maneno, virai, na mawazo wanayoweza kuyajumuisha kwenye barua kwa rafiki yao wakielezea umuhimu wa ndoa ya hekaluni. Wanaweza pia kuangalia “Kwa Nini Ndoa ni Takatifu kwa Baba wa Mbinguni?” kutoka “Uso kwa Uso na Mzee na Dada Renlund” ([Matangazo ya ulimwengu wote ya vijana], Agosti. 5, 2017, FacetoFace.ChurchofJesusChrist.org). Unaweza kuwapa muda wa kuandika barua na kisha waalike kushiriki walichokiandika.

  • Kwa kuona mfano wa ndoa yenye uaminifu kunaweza kuwatia moyo wale unaowafundisha kutafuta baraka hii wao wenyewe. Njia mojawapo ya kufanya hili ni kwa kurejea sehemu za ujumbe wa Mzee L. Whitney Clayton “Ndoa: Tazama na Jifunze” (Liahona, Mei 2013, 83–85). Ni kipi ambacho washiriki wa akidi au darasa wanajifunza kutoka katika ujumbe huu kuhusu jinsi ya kujenga ndoa ya milele yenye furaha? Washiriki wa akidi au darasa wanaweza pia kurejea mawazo katika “Achieving a Happy Marriage” katika True to the Faith (kurasa 99–101). Wanaweza pia kuangalia “Ni kwa Jinsi Gani Mzee na Dada Bednar Walikutana?” kutoka kwenye “Uso kwa Uso na Mzee na Dada Bednar” ([Matangazo ya ulimwengu wote ya vijana], Mei 12, 2015, FacetoFace.ChurchofJesusChrist.org).

  • Waombe washiriki wa akidi au darasa kufikiria baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuwazuia wao wasiunganishwe hekaluni. Ni nini tunaweza kufanya sasa kuepukana na vitu hivi? Kisha wanaweza kurejea “Eternal Marriage” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel ([2019], 89) kutafuta kanuni na matendo yanayopelekea kwenye ndoa na familia zenye furaha. Wanaweza kuorodhesha baadhi ya vitu wanavyoweza kuvifanya sasa kujiandaa kwa ajili ya ndoa ya milele. Je, ni lipi jukumu la Mwokozi katika kutusaidia kujiandaa na kuifikia ndoa ya milele?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

  • Mafundisho na Maagano 49:16–17; 131:1–4; 132:13–19 (Ndoa ya milele ni ya muhimu katika mpango wa Mungu)

  • Mada za Injili, “Ndoa,” topics.ChurchofJesusChrist.org

  • Video “What Is a Temple Wedding Like?”, temples.ChurchofJesusChrist.org

  • Mzee D. Todd Christofferson alisema: “Kutangaza kweli za muhimu zihusianazo na ndoa na familia si kuangalia juu juu au kupunguza thamani ya dhabihu na mafanikio ya wale ambao kanuni hii kwa sasa sio uhalisia. … Mengi ambayo ni mazuri, mengi ambayo ni muhimu—hata wakati mwingine yote yaliyo muhimu kwa sasa—yanaweza kufikiwa katika hali ambazo ni nzuri kidogo. … Kwa ujasiri tunashuhudia kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo ulitarajia na, hatimaye, utafidia unyang’anyi wote na hasara kwa wale watakaomgeukia Yeye” (“Kwa nini Ndoa, Kwa nini Familia,” Liahona, Mei 2015, 52).

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Uliza maswali ambayo yatawahamasisha wale unaowafundisha kutafakari kwa undani kuhusu ndoa ya milele na kuhisi hamu ya kutendea kazi lengo hilo. Sikiliza kwa makini majibu yao na jibu kwa ukarimu kama utakavyoongozwa na Roho.