Mafundisho na Maagano 2021
Novemba 28. Ni Kwa Jinsi Gani Joseph Smith Alisaidia Kutimiza Mpango wa Baba wa Mbinguni? Mafundisho na Maagano 135–136


“Novemba 28. Ni Kwa Jinsi Gani Joseph Smith Alisaidia Kutimiza Mpango wa Baba wa Mbinguni? Mafundisho na Maagano 135–136,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Novemba 28. Ni Kwa Jinsi Gani Joseph Smith Alisaidia Kutimiza Mpango wa Baba wa Mbinguni?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

mchoro wa Joseph Smith

Kaka Joseph, na David Lindsley

Novemba 28

Ni Kwa Jinsi Gani Joseph Smith Alisaidia Kutimiza Mpango wa Baba wa Mbinguni?

Mafundisho na Maagano 135–136

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Tunaweza kufanya nini ili kujenga umoja miongoni mwa akidi au washiriki wa darasa? Je, ni malengo gani tunahitaji kuyashughulikia pamoja?

  • Wajibu wetu au majukumu. Tunafanya nini ili kushiriki injili? Ni uzoefu upi tumeupata kwa kufanya kazi ya hekalu na historia ya familia?

  • Maisha yetu. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu? Ni nini kimetutia moyo katika kujifunza kwetu maandiko wiki hii?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

“Joseph Smith, Nabii na Mwonaji wa Bwana, amefanya mengi, isipokuwa Yesu peke yake, kwa ajili ya wokovu wa wanadamu katika ulimwengu huu, kuliko mwanadamu mwingine yeyote aliyewahi kuishi ndani yake” (Mafundisho na Maagano 135:3). Hii ni kauli ya ujasiri kuhusu jukumu la Joseph Smith. Je, umewahi kufikiria kuhusu maana ya kauli hii katika maisha yako? Ni kwa jinsi gani maisha yako yangekuwa ya tofauti kama injili ya Yesu Kristo isingerejeshwa? Ni kipi unaweza kukifanya kuwasaidia washiriki wa akidi yako au darasa lako kuimarisha shuhuda zao kuhusu misheni ya Joseph Smith?

Unapojiandaa kufundisha, kwa kuongezea kwenye kusoma Mafundisho na Maagano 135, fikiria kurejea “Joseph Smith” katika True to the Faith ([2004], 89–90) na ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Joseph Smith” (Liahona, Nov. 2014, 28–31).

msichana na mvulana wakisoma Kitabu cha Mormoni

Maisha yetu yamebarikiwa kwa kweli zilizorejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuanza mjadala kuhusu jinsi Joseph Smith alivyosaidia kutimiza mpango wa Baba wa Mbinguni, unaweza kuanza kwa kurejea kile ambacho washiriki wa akidi au darasa wamejifunza kuhusu Nabii kwa kusoma Mafundisho na Maagano 135 wiki hii. Kwa mfano, wangeweza kuandaa orodha ya kweli wanazozijua kuhusu Mwokozi na injili Yake kwa sababu ya Joseph Smith. Kwa nini kila moja ya kweli hizi ni muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni? Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuelewa vyema jukumu la Joseph Smith katika mpango wa wokovu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kujiandaa kwa ajili ya kuwasaidia wengine kuelewa umuhimu wa Nabii Joseph, wangeweza kusoma “The Restoration of the Gospel of Jesus Christ through Joseph Smith” katika sura ya 3 ya Preach My Gospel ([2019], 36–38). Wakifanya kazi katika jozi au katika makundi madogo, wanaweza kutafuta pointi zinazoonekana za muhimu kwa ajili ya kushiriki na wengine. Kisha wanaweza kufanya zoezi la kushiriki uzoefu wa Joseph Smith wao kwa wao katika maneno yao wenyewe. Waombe wafikirie ni nini watafanya ili kushiriki ujumbe wa Urejesho. Labda wanaweza kumfikiria mtu mahsusi ambaye watashiriki nae ujumbe huu. Wanaweza pia kuwa radhi kushiriki uzoefu kuhusu wakati walipomsaidia mtu kujifunza kuhusu Joseph Smith.

  • Waombe washiriki wa akidi au darasa kupiga taswira ya kwamba mmoja wa marafiki zao kanisani anasema “sina uhakika kama nina ushuhuda wa Joseph Smith. Umewezaje kujua kuwa ni nabii? Je, tutajibu vipi? Tunajifunza nini kutoka katika uzoefu wa Joseph Smith mwenyewe katika Joseph Smith—Historia ya 1:8–19 kuhusu jinsi ya kupata au kuimarisha shuhuda zetu? Waombe washiriki wa akidi au darasa kuandaa orodha ya njia za kuimarisha shuhuda zao za Nabii Joseph Smith na kila mmoja achague kitu kimoja ambacho watapenda kufanya wiki hii.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuelewa vyema kazi ambayo Mungu aliikamilisha kupitia Joseph Smith, unaweza kuwaalika wasome kurasa 48–53 za Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinkely (2016) au kutazama video moja au zaidi katika “Nyenzo Saidizi.” Wanaweza kuteua fundisho moja au zaidi na mazoezi yatolewayo katika nyenzo hizi ambayo yana umuhimu sana kwao. Wanaweza kuelezea kwa nini wana shukrani kwamba Bwana amerejesha vitu hivi kupitia Joseph Smith. Wanaweza pia wakafurahia kuandika maneno machache wakionyesha shukrani zao za jinsi ambavyo kazi ya Joseph Smith imesaidia kuwaleta karibu na Mwokozi. Wanaweza pia kutafakari kile wanachoweza kufanya ili kuwa na fursa kubwa ya kupokea baraka zaidi ambazo Bwana amefanya zipatikane kupitia Joseph Smith.

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

  • Mafundisho na Maagano 35:17–18 (Kwa kupitia Nabii Joseph Smith, Bwana amerejesha utimilifu wa injili)

  • Russell M. Nelson, “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuaje Bila Hicho?Liahona, Nov. 2017, 60–63

  • Video “Teachings of Joseph Smith: The Nature of God,” “Ministry of Joseph Smith: The Book of Mormon,” “Ministry of Joseph Smith: The Organization of the Church,” “Ministry of Joseph Smith: The Restoration of Priesthood Authority,” “Ministry of Joseph Smith: Temples,” ChurchofJesusChrist.org

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi alifokasi katika kuwasaidia wafuasi wake kuishi injili kwa mioyo yao yote. Je, unawezaje kuwasaidia wale unaowafundisha kuona ni kwa jinsi gani shuhuda zao kuhusu Joseph Smith zinapaswa kuathiri maisha yao ya kila siku?