“Desemba 12. Nitapataje Majibu ya Maswali Yangu? Makala za Imani na Matamko Rasmi 1 na 2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)
“Desemba 12. Nitapataje Majibu ya Maswali Yangu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021
Desemba 12
Nitapataje Majibu ya Maswali Yangu?
Makala za Imani na Matamko Rasmi 1 na 2
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):
-
Akidi au darasa letu. Je, ni shughuli gani tumezifanya hivi karibuni? Je, zilifanikiwa? Ni nini kilifanyika vizuri, na ni jinsi gani tunaweza kuboresha?
-
Wajibu wetu au majukumu. Ni nani anahitaji usaidizi wetu? Tunawezaje kuwasaidia?
-
Maisha yetu. Ni malengo gani tunayashughulikia kibinafsi? Ni uzoefu gani tunaweza kuushiriki? Ni baraka zipi tumepokea?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Ni kawaida kuwa na maswali. Tunashangaa kuhusu mambo yajayo na ulimwengu unaotuzunguka. Pia tuna maswali kuhusu Mungu na Mpango Wake kwetu. Unaposoma Matamko Rasmi 1 na 2 wiki hii, gundua kile manabii na mitume walichofanya kutafuta majibu ya maswali yao (muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaweza kuwa wenye msaada). Ni kwa jinsi gani kutafuta majibu ya maswali kumekusaidia katika kujifunza kwako injili? Ni kipi unaweza kukifanya kuwahimiza washiriki wa akidi yako au darasa lako kutafuta majibu ya maswali yao ya injili katika njia ya uaminifu? Unapojiandaa kufundisha, fikiria kurejea Mafundisho na Maagano 6:14–15; 9:7–9 na “Acquiring Spiritual Knowledge” katika Doctrinal Mastery Core Document ([2018], 3–5).
Jifunzeni Pamoja
Wakati washiriki wa akidi yako au darasa lako walipojifunza Matamko Rasmi 1 na 2 wiki hii, wanaweza wakawa wamegundua kanuni zihusianazo na kupokea majibu ya maswali yahusuyo injili. Wapatie dakika chache kurejea matamko na kushiriki walichojifunza kuhusu kupokea ufunuo. Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema jinsi ya kutafuta majibu ya maswali yao ya injili.
-
Mafungu yafuatayo hufundisha kanuni zihusianazo na kuuliza maswali na kupokea majibu: Mathayo 7:7; Mafundisho na Maagano 6:14–15; 9:7–9. Akidi yako au darasa lako wanaweza kusoma vifungu hivi kwa pamoja na kuandaa orodha ubaoni ya kanuni walizozipata. Kwa nini si mara zote Baba wa Mbinguni hujibu maswali yetu kikamilifu au kwa wakati huohuo? Tunawezaje kuendelea kuonyesha imani yetu wakati tunaposubiria majibu? (Ona Mafundisho na Maagano19:23; 78:18). Fikiria kushiriki uzoefu wa wakati ulipokuwa na swali kuhusu injili na ukapokea jibu. Waombe washiriki wa akidi au darasa kushiriki uzoefu sawa na huo.
-
Je, washiriki wa akidi yako au darasa lako wanaweza kuwafikiria watu katika maandiko waliouliza maswali yaliyopelekea kupata ufunuo? (Kama itahitajika, unaweza kuwarejesha kwenye maandiko yapatikanayo kwenye “Nyenzo Saidizi.”) Washiriki wa akidi au darasa wanaweza kusoma kuhusu watu hawa katika maandiko na kutafuta ni maswali gani waliuliza, jinsi walivyotafuta majibu, na majibu waliyopokea. Tunajifunza nini kutoka katika mifano hii? Tunawezaje kutumia kile tulichojifunza wakati tunapoendelea kutafuta majibu ya maswali yetu wenyewe? Kama sehemu ya shughuli hii, unaweza pia kuonyesha “Ninawezaje Kuishi Viwango vya Injili Vizuri Zaidi?” kutoka kwenye “Uso kwa Uso na Mzee na Dada Bednar” ([Matangazo ya ulimwengu wote ya vijana], Mei 12, 2015, FacetoFace.ChurchofJesusChrist.org).
-
Ujumbe wa Mzee W. Mark Bassett “Kwa Ajili ya Maendeleo Yetu ya Kiroho na Kujifunza” (Liahona, Nov. 2016, 52–54) hutoa mapendekezo ya jinsi ya kutafuta majibu ya maswali ya kiroho. Akidi yako au darasa lako wanaweza kusoma kwa pamoja aya nne za ujumbe wake wakianzia na “Ili kuelewa siri za Mungu.” Kisha waalike washiriki wa akidi au darasa kusoma 1 Nefi 2:16, 19–20; 10:17–19; 11:1 na kutafuta ni nini Nefi alifanya kutafuta majibu ya maswali yake. Waalike washiriki wa akidi au darasa kufikiria kuhusu nini watafanya ili kufuata mfano wa Nefi wakati wanapokuwa na maswali yahusuyo injili.
-
Hadithi katika Marko 9:14–27 inaweza kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa wanapokabiliana na maswali au wasiwasi. Kabla ya kipindi, mwalike mshiriki wa akidi au darasa lako aje akiwa amejiandaa kushiriki hadithi. Kisha, igawe akidi yako au darasa lako katika makundi matatu, na kuwapangia kila kikundi kusoma mojawapo ya mawazo ambayo Mzee Jeffrey R. Holland aliyatoa kuhusu hadithi katika ujumbe wake usemao “Bwana, Naamini” (Liahona, Mei 2013, 93–95). Tunawezaje kuyatumia mawazo ya Mzee Holland wakati sisi au mtu mwingine tumjuaye anapokuwa na maswali au wasiwasi kuhusu injili?
Tenda kwa Imani
Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.
Nyenzo Saidizi
-
Enoshi 1:1–8; Alma 5:43–47; 40:3–5; Etheri 2:18–23; Mafundisho na Maagano 138:1–4, 11; Joseph Smith—Historia ya 1:10–18 (Mifano ya watu wakitafuta majibu ya maswali yao)
-
James B. Martino, “Mgeukie Yeye na Majibu Yatakuja,” Liahona, Nov. 2015, 58–60
-
Mada za Injili, “Kujibu Maswali ya Injili,” topics.ChurchofJesusChrist.org