Mafundisho na Maagano 2021
Desemba 26. Kwa nini Familia Ni za Muhimu? “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu”


“Desemba 26. Kwa nini Familia Ni za Muhimu? ‘Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021 (2020)

“Desemba 26. Kwa nini Familia Ni za Muhimu?” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2021

Picha
kijana akikumbatiwa

Desemba 26

Kwa nini Familia Ni za Muhimu?

Familia: Tangazo kwa Ulimwengu

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni au Dhima ya Wasichana. Kisha ongoza majadiliano kuhusu vitu kama vifuatavyo, na panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadiliana (mnaweza kuamua katika mkutano wa urais ni vitu gani vya kujadili):

  • Akidi au darasa letu. Je, nani ni mgeni katika kata yetu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia kuhisi wamekaribishwa? Nini tunafanya ili kufanya muda wetu katika mikutano ya akidi au madarasa kuwa wa maana?

  • Wajibu wetu au majukumu. Ni yapi baadhi ya majukumu na wajibu tulionao kama wavulana na wasichana? Tunawezaje kuyatimiza vyema?

  • Maisha yetu. Nini tunafanya ili kuwa zaidi kama Yesu Kristo na kupokea nguvu Zake katika maisha yetu? Tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja Kwake?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kila familia ni tofauti, na hakuna familia iliyo kamilifu. Lakini sote tunao Wazazi wa Mbinguni ambao ni wakamilifu, wanaotutaka tupokee baraka ya kuishi kwa furaha kama familia za milele. Katika kutusaidia kufikia hili, Mungu amewavuvia manabii na mitume kutangaza kweli za milele katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org).

Wakati ukijiandaa kufundisha kuhusu umuhimu wa familia, fikiria kuhusu kwa nini familia yako ni muhimu kwako. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo amesaidia katika familia yako kupata furaha? Unapojiandaa kufundisha, unaweza kusoma “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist.org), “Familia” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ([2011], 14–15), na ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Kwa nini Ndoa, Kwa nini Familia” (Liahona, Mei 2015, 50–53). Ni kanuni zipi kutoka katika nyenzo hizi unahisi zitakuwa za muhimu zaidi kwa wale unaowafundisha?

Picha
familia ikipanda mlima

Familia ni kitovu cha mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu.

Jifunzeni Pamoja

Kwa kuanza majadiliano kuhusu umuhimu wa familia, unaweza kuuliza akidi au darasa ni kipi wamejifunza kuhusu furaha katika maisha ya familia wakati waliposoma “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” nyumbani. Je, walijifunza nini ambacho kingeweza kuwasaidia wao kuimarisha familia zao? Kisha chagua shughuli moja au zaidi zilizopo hapa chini ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuwa na uelewa wa kina wa kwa nini familia ni muhimu katika mpango wa Baba wa Mbinguni.

  • Maandiko katika “Nyenzo Saidizi” yanaunga mkono kanuni zenye uvuvio katika tangazo kwa familia. Huenda ukampa kazi kila mshiriki wa akidi au darasa kusoma mojawapo ya maandiko haya na kisha kutafuta kutoka katika tangazo la familia kifungu ambacho kinahusiana na andiko lake. Kila mshiriki wa akidi au darasa anaweza kushiriki kile alichokipata.

  • Kuishi mafundisho ya Yesu Kristo huongoza kwenye furaha ya kweli na isiyo na mwisho ndani ya familia zetu. Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kuelewa hili, unaweza kumualika kila mtu kuchagua sifa kama ya Kristo (ona “How Do I Develop Christlike Attributes?” Sura ya 6 katika Preach My Gospel [2019], 121–29) na kisha kutafuta andiko au kauli ya kinabii inayofundisha kuhusu sifa hiyo. Washiriki wa akidi au darasa wanapokuwa wakishiriki kile walichokipata, wanaweza kujibu mojawapo au zaidi ya maswali yafuatayo: Je, ni kwa jinsi gani kuiishi sifa hii kama ya Kristo kikamilifu zaidi kutaathiri familia yangu? Ninajifunza nini kutoka katika mfano wa Mwokozi kuhusu jinsi ya kuitumia sifa hii katika familia yangu?

  • Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Adui anaongeza mashambulizi yake kwenye imani na juu yetu na familia zetu kwa kiwango kikubwa sana” (“Maneno ya Ufunguzi,” Liahona, Nov. 2018, 7). Ili kuwasaidia washiriki wa akidi au darasa kujilinda dhidi ya mashambulizi haya, unaweza kuwaalika kuorodhesha ubaoni sifa kadhaa na tabia ambazo Shetani anaziunga mkono ili kudhoofisha familia. Kwa nini vitu hivi ni hatarishi kwa familia? Washiriki wa akidi au darasa kisha wanaweza kutafuta kutoka aya ya saba ya tangazo la familia ili kupata mitazamo na tabia ambazo zinaweza kukabiliana na mashambulizi ya Shetani. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutafuta msaada wa Mwokozi katika kukuza mitazamo na tabia hizi? Kama sehemu ya majadiliano haya, unaweza kuonyesha video ya “Proclamation” (ChurchofJesusChrist.org). Tunajifunza nini kuhusu jinsi ya kuzikinga familia zetu kutokana na ushawishi wa Shetani?

Tenda kwa Imani

Wahimize washiriki wa akidi au darasa kutafakari na kuandika kile watakachokifanya ili kutenda juu ya misukumo ambayo wameipokea leo. Ni kwa jinsi gani somo la leo linahusiana na malengo binafsi ambayo wameyaweka? Kama watapenda, washiriki wa akidi au darasa wanaweza kushiriki mawazo yao.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Mwokozi aliwaalika wanafunzi Wake kushuhudia, na walipofanya hivyo, Roho aligusa mioyo yao. Wakati unapofundisha, alika washiriki wa akidi au darasa kushiriki shuhuda zao za umuhimu wa familia katika mpango wa Mungu.

Chapisha