Agano la Kale 2022
Oktoba 9. Kwa Nini Yesu Kristo Anapaswa Kuwa Muhimu katika Maisha Yangu? Isaya 58–66


“Oktoba 9. Kwa Nini Yesu Kristo Anapaswa Kuwa Muhimu katika Maisha Yangu? Isaya 58–66,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Oktoba 9. Kwa Nini Yesu Kristo Anapaswa Kuwa Muhimu katika Maisha Yangu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
Yesu Kristo

Oktoba 9

Kwa Nini Yesu Kristo Anapaswa Kuwa Muhimu katika Maisha Yangu?

Isaya 58–66

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha, kwa nyongeza kwenye kushauriana kuhusu mahitaji mahususi ya darasa au shughuli za akidi, mnaweza kutaka kujadili misukumo na dhamira kutoka mkutano mkuu. Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia.

  • Ni dhamira zipi au jumbe zipi zimejitokeza bayana kwetu? Ni nini kiliimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?

  • Ni nini kiliimarisha shuhuda zetu juu ya manabii walio hai? Tumehisi kushawishika kufanya nini kwa sababu ya kile tulichojifunza au kuhisi?

  • Ni nini tunahitajika kufanya kama darasa au akidi ili kutendea kazi ushauri tuliousikia katika mkutano mkuu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

“Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu,” Isaya alisema, “maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki” (Isaya 61:10). Kwa nini “unafurahia katika Bwana”? Kama vile Isaya, tunavyotambua kile Bwana alichotufanyia, tunafurahia, na tunazungumza kila mara juu ya “wema wa Bwana, na sifa za Bwana” (Isaya 63:7).

Je, wale unaowafundisha wanahisi vipi kuhusu Mwokozi? Ni nini kingeweza kuwasaidia kuhisi upendo mkuu na staha nyingi kwa ajili Yake? Je, nini kingewasaidia kuhisi upendo Wake? Unapotafakari maswali haya na kusoma Isaya 58–66, unaweza pia kupitia tena ujumbe wa Mzee Matthew S. Holland “Zawadi Nzuri Sana ya Mwana” (Liahona, Nov. 2020, 45–47) na ujumbe wa Dada Cristina B. Franco “Nguvu ya Uponyaji ya Yesu Kristo” (Liahona, Nov. 2020, 60–62).

Picha
msichana akisoma maandiko

Tunapojifunza zaidi kuhusu Mwokozi, tunavutiwa kumfanya Yeye kuwa kitovu cha maisha yetu.

Jifunzeni Pamoja

Washiriki wa darasa au akidi wanapojifunza kuhusu misheni Yesu Kristo alitumwa kutimiza, watavutiwa zaidi kumfanya Mwokozi kuwa kitovu cha maisha yao. Labda wanaweza kupekua Isaya 61:1–3 na kutengeneza orodha ubaoni ya kile Mwokozi alipakwa mafuta kufanya (ona pia Luka 4:16–20). Ni kwa jinsi gani Mwokozi alitimiza vipengele hivi vya misheni Yake? Ni kwa jinsi gani Yeye anavitimiza katika maisha yetu sasa? Mawazo hapa chini yanaweza kusaidia darasa lako au akidi kuendelea na mjadala kuhusu kwa nini Yesu Kristo anapaswa kuwa kitovu cha maisha yetu.

  • Mkutano mkuu daima una jumbe ambazo zinashuhudia juu ya Yesu Kristo. Ungeweza kuwaalika washiriki kadhaa wa darasa au akidi kushiriki kitu walichojifunza kuhusu Mwokozi wakati wa mkutano mkuu. Wahimize kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi kwa sababu ya kile walichojifunza.

  • Maandiko yanaweza kuwasaidia vijana kuelewa vizuri zaidi kwa nini Mwokozi anapaswa kuwa kitovu cha maisha yao. Unaweza kuandika ubaoni Kwa Nini Yesu Kristo Anapaswa Kuwa Muhimu katika Maisha Yangu? Waombe vijana washiriki mawazo yao. Kisha unaweza kuwaomba (binafsi au katika vikundi) kupekua maandiko ndani ya “Nyenzo Saidizi” kupata majibu ya ziada. Waalike vijana kushiriki kile wanachojifunza na kwa nini kina maana kwao.

  • Fikiria kuwauliza wale unaowafundisha kuelezea siku muhimu sana katika maisha yao. Ni ipi inaweza kuwa siku muhimu sana katika historia? Waalike wao kugundua kile Mzee Dieter F. Uchtdorf alichosema ilikuwa ndiyo siku muhimu sana kwa kupitia tena ujumbe huu “Mtazame Mtu Huyo!” (Liahona, Mei 2018, 107–10). Wahimize vijana kutafuta baraka ambazo Mzee Uchtdorf aliwaahidi wale ambao “wanamtazama” Yesu Kristo. Wangeweza pia kushiriki kile wanachofanya ili kumfanya Mwokozi kuwa kitovu cha maisha yao ya kila siku. Unaweza kuwahimiza wafikirie kile wanachoweza kufanya kusogea karibu na Yesu Kristo na kuweka lengo la kufanya hivyo.

  • Kama mtu angetuuliza kwa nini tunaamini katika Yesu Kristo, tungesema nini? Wahimize vijana kushiriki mawazo yao na kuyaandika ubaoni. Ungeweza pia kuwaalika wao wapitie tena “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (ChurchofJesusChrist.org) au “Misheni Takatifu ya Yesu Kristo” katika sura ya 3 ya Hubiri Injili Yangu ([2019], 60–61). Wahimize kutafuta kweli rahisi watakazoshiriki ili kuelezea kwa nini Mwokozi ni muhimu kwao. Wanaweza kuongeza kweli walizopata kwenye orodha ubaoni na kujadili jinsi wanaweza kushiriki kweli hizi na watu wanaowajua.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Kila mtu binafsi katika darasa lako ni chanzo kikubwa cha ushuhuda, umaizi, na uzoefu kutokana na kuishi injili. Waalike kushiriki pamoja na kuinuana” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,5).

Chapisha