Agano la Kale 2022
Septemba 25. Majukumu Yetu ni Yapi katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa? Isaya 40–49


“Septemba 25. Majukumu Yetu ni Yapi katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa? Isaya 40–49,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Septemba 25. Majukumu Yetu ni Yapi katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
kijana amesimama nje ya hekalu

Septemba 25

Majukumu Yetu ni Yapi katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa?

Isaya 40–49

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa wa akidi au urais wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kushughulikia mialiko hiyo au kazi hizo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Tunaweza kusema nini au kufanya nini ili kuwafikia wale wanaoweza kuwa wanahisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?

  • Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine kuimarisha familia zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Ni wazi kutoka katika maandiko kwamba kusaidia katika kazi ya Bwana si kazi ya watu wazima pekee. Samweli alikuwa mvulana mdogo wakati Bwana alipozungumza naye mara ya kwanza. Mariamu vile vile alikuwa msichana mdogo wakati malaika alipomtembelea, kutangaza kwamba yeye angekuwa mama ya Mwokozi. Na Joseph Smith alikuwa na umri wa miaka 14 wakati Bwana alipomwita kurejesha injili. Hivi karibuni kabisa, Rais Russell M. Nelson aliwaalika vijana wote “wajiunge na batalioni ya vijana ya Bwana ili kusaidia kukusanya Israeli (“Tumaini la Israeli” [ibada ya vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018], ChurchofJesusChrist.org). Kwa Hakika, wakati Bwana aliposema, “Nawe, Israeli, ni mtumishi wangu” (Isaya 41:8), hii ilijumuisha watu Wake wote wa agano, ikijumuisha wale katika darasa lako au akidi.

Hata hivyo sisi sote tulifanya agano kumtumikia Mungu tulipobatizwa, si vijana wote wanajiona kama watumishi wa Bwana. Wanaweza wasitambue njia za kipekee wanazoweza kusaidia katika kazi Yake. Tafuta vifungu katika Isaya 41–44 na sehemu ya 1.2 ya General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints ambavyo vinaweza kuwasaidia vijana kuelewa kile inamaanisha kuwa watumishi wa Bwana.

Picha
wasichana nje ya hekalu

Kila kijana anaweza kuchangia kwa njia ya kipekee katika kazi ya wokovu na kuinuliwa.

Jifunzeni Pamoja

Isaya 41:44 inaweza kuwasaidia vijana kuelewa maana ya kuwa mtumishi wa Mungu? Ili kuanzisha mjadala, unaweza kuandika marejeo kama haya ubaoni: Isaya 41:8–10; 42:6–7; 43:9–12; 44:21. Kila mtu anaweza kuchagua kifungu, na kukisoma, na kushiriki kile yeye amejifunza kuhusu inamaanisha ni kuwa mtumishi wa Bwana. Ni kwa njia gani sisi ni watumishi wa Bwana? Ni baraka zipi huja wakati tunapokuwa katika huduma Yake? Hapa kuna njia zingine za kuwasaidia wale unaowafundisha kuwaleta watu kwa Kristo kama washiriki hai katika kazi Yake.

  • Je, wale unaowafundisha wanaelewa “kazi ya wokovu na kuinuliwa” ni nini? Ili kuwasaidia, unaweza kuwapa kazi ya kujifunza (binfasi au katika vikundi vidogo) mojawapo ya sehemu ndogo nne za sehemu ya 1.2 ya General Handbook. Kila sehemu ndogo inaelezea kipengele cha kazi hii. Muombe kijana kutafakari maswali kama haya: Ni vitu gani mahususi mtu wa umri wangu angefanya ili kushiriki katika kipengele hiki cha kazi ya wokovu? Ni nini darasa letu au akidi yetu inaweza kufanya? Kila mtu au kikundi kingeweza kushiriki kile walichojifunza, pamoja na majibu kwa maswali.

  • Wale unaowafundisha wanaweza kunufaika kwa kujifunza zaidi kuhusu vipengele vinne vya kazi ya wokovu na kuinuliwa—kuishi injili ya Yesu Kristo, kuwatunza wale walio na mahitaji, kuwaalika wote kuipokea injili. na kuunganisha familia milele. Wangeweza kuchagua kipengele ambacho wanakipenda na kuchunguza baadhi ya vitu vinavyohusiana navyo katika “Nyenzo Saidizi.” Waache vijana washiriki kile walichopata ambacho kinawavutia kuwa waongofu zaidi kwa Bwana na kuwasaidia wengine kufanya vivyo hivyo. Kisha wanaweza kufanya mipango ya kufanya kitu ambacho husaidia kutimiza kazi hii. Rais wa darasa au akidi angeweza kuongoza mjadala.

  • Kuwasaidia vijana kutafakari jinsi wanaweza kutumia talanta zao kuzileta nafsi kwa Kristo, ungeweza kuomba kila mmoja wao kujifunza sehemu ya ujumbe wa Mzee John C. Pingree Jr. “Na Ninayo Kazi kwa Ajili Yako” (Liahona, Nov. 2017, 32–35). Wanaweza kushiriki jinsi kile walichojifunza kingeweza kumsaidia mtu ambaye hana uhakika kwamba anaweza kusaidia katika kazi ya Bwana. Mnaweza pia kupitia tena pamoja sehemu “Kugundua na kukuza Vipawa vya Kiroho” katika ujumbe wa Pingree. Ni kwa jinsi gani Bwana hutusaidia kugundua na kukuza talanta zetu?

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Ikiwa vijana watahisi kwamba unawaamini, imani yao katika uwezo wao mtakatifu itakua” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 28).

Chapisha