Agano la Kale 2022
Oktoba 23. Je, Injili Imeandikwa Moyoni Mwangu? Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3


“Oktoba 23. Je, Injili Imeandikwa Moyoni Mwangu? Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Oktoba 23. Je, Injili Imeandikwa Moyoni Mwangu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
kujifunza maandiko kama familia

Oktoba 23

Je, Injili Imeandikwa Moyoni Mwangu?

Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1;3

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni tena kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kushughulikia mialiko hiyo au kazi hizo?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Tunaweza kufanya nini au kusema nini ili kuwafikia wale wanaoweza kuwa wanahisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?

  • Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine kuimarisha familia zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Bwana alimwambia nabii Yeremia kwamba katika siku zinazokuja, Yeye angewakusanya Israeli na kufanya “agano jipya” na watu Wake. Yeye alitangaza, “Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; na nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (ona Yeremia 31: 31– 31). Hizo siku ni leo, na sisi ni watu wa Mungu. Mafundisho haya yanaweza kusukuma—na wale unaowafundisha—kuuliza, Inamaanisha nini kwa injili kuandikwa katika moyo wangu? Je, injili imeandikwa moyoni mwangu? Kama haijandikwa, unaweza kufanya nini kuhusu hilo?

Fikiria jinsi utakavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako au akidi kutafakari maswali haya kwa ajili yao wenyewe. Ili kujiandaa kufundisha, unaweza kutafuta jumbe za kushiriki kutoka katika Yeremia 30–33; 36; kutoka kwa ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Acheni Mungu Ashinde” (Liahona, Nov. 2020, 92–95); na kutoka kwa ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Nawe Utakapoongoka” (Liahona, May 2004, 11–13).

Picha
wasichana wakijifunza maandiko

Tunapompenda Bwana na kutafuta kujifunza juu Yake, injili itaandikwa katika mioyo yetu.

Jifunzeni Pamoja

Wahimize vijana kujadili Yeremia 31:31– 30. Ili kufanya hivi, ungeweza kuwapa wao mioyo ya karatasi iliyo na maswali kadhaa yaliyoandikwa juu yake kuhusu kile inachomaansiha kuwa na injili katika mioyo yetu, kama vile hayo yaliyoandikwa ndani ya “Jiandae Mwenyewe Kiroho.” Wakifanya kazi kibinafsi, katika jozi, au vikundi vidogo, vijana wangeweza kusoma mistari hii kutoka kwa Yeremia na kutafakari jinsi ambavyo wangejibu maswali. Waache washiriki maswali yao na majibu wanayofikiria. Hapa chini kuna mawazo zaidi ambayo yanaweza kukusaidia kuwafundisha vijana kuhusu jinsi injili inaweza kuandikwa katika mioyo yao.

  • Wakati Musa alipotoa baadhi ya mafundisho yake ya mwisho kwa Waisraeli, aliwasihi kupokea maneno ya Mungu katika mioyo yao. Pia aliwafundisha baadhi ya njia wanazoweza kufanya hivi, kama inavyoptikana katika Kumbukumbu la Torati. Kama darasa au akidi, someni mistari hii pamoja na mjadili njia zipi tunazoweza kufanya kile Musa alichoshauri. Kwa baadhi ya mawazo, darasa lako au akidi yako wanaweza kutazama video “Njoo, Unifuate: Maneno Haya” (ChurchofJesusChrist.org). Wanaweza pia kujifunza Alma 5:14, 26–35 kutafuta kile Alma alifundisha kuhusu jinsi tunaweza kuweka injili iliyoandikwa ndani ya mioyo yetu.

  • Katika ujumbe wake “Nawe Utakapoongoka,” Mzee D. Todd Christofferson alielezea nini tunaweza kufanya kuwa na injili iliyoandikwa ndani ya mioyo yetu. Tunajifunza nini kutoka katika aya nne za kwanza kuhusu kile inachomaanisha kuwa na injili iliyoandikwa ndani ya mioyo yetu? Ungeweza kumwalika kila kijana kusoma moja au zaidi ya aya zilizobakia na kutafuta kile tunachohitaji kufanya ili hii itokee. Ni jukumu gani Mwokozi analofanya? Ni jukumu gani sisi tunalofanya? Wahimize vijana kushiriki majibu yao, pamoja na umaizi mwingine walioupata. Ni uzoefu gani umetusaidia kupata injili iliyoandikwa ndani ya mioyo yetu? Ni jukumu gani kuyashika maagano yetu linafanya katika mchakato huu?

  • Rais Russell M. Nelson alielezea kwamba neno Israeli “linataja mtu ambaye yu radhi kumuacha Mungu ashinde katika maisha yake” (“Acheni Mungu Ashinde,” 92). Ungeweza kuwaalika vijana kupekua aya sita za kwanza za ujumbe wa Rais Nelson na sehemu ya mwisho ya ujumbe unaoanzia na “Swali kwa kila mmoja wetu.” Waombe watafute kitu ambacho kinawasaidia kuelewa kile inamaanisha “kuacha Mungu ashinde” katika maisha yao. Tunahisi vipi na kutenda wakati Mungu anashinda katika maisha yetu? Ni nini Rais Nelson alifundisha kuhusu jinsi kuwa na injili iliyoandikwa ndani ya maisha yetu huathiri juhudi zetu za kukusanya Israeli?

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wakipenda, wanaweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Mafundisho yanayopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho yana nguvu ya kubadilisha mioyo na kuongeza imani. Wakati wewe na wale unaowafundisha ‘wanajaribu utukufu wa uwezo wa neno la Mungu,’ utapata kwamba una ‘maelekezo makubwa ya kuongoza watu kufanya kile ambacho [ni] haki’ (Alma 31:5)” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,5).

Chapisha