Agano la Kale 2022
Novemba 13. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupokea Mbubujiko wa Roho wa Bwana’? Hosea 1–6; 10–14; Yoeli


“Novemba 13. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupokea Mbubujiko wa Roho wa Bwana’? Hosea 1–6; 10–14; Yoeli,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Novemba 13. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupokea Mbubujiko wa Roho wa Bwana’? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

darasa la wasichana

Novemba 13

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupokea Mbubujiko wa Roho wa Bwana’?

Hosea 1–6; 10–14; Yoeli

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa akidi au urais wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni tena kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Je, ni uzoefu gani ya hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Je, ni akina nani wanahitaji usaidizi wetu na sala zetu? Je, ni nini tunahisi kuvutiwa kukifanya ili kuwasaidia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa wanafamilia au marafiki ambao hawashiriki imani yetu?

  • Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha upendo na ufadhili kwa familia zetu na kuleta tofauti chanya katika nyumba zetu.

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Hamna shaka kwamba tunaishi nyakati zisizo na uhakika na za kuogofya. Nabii wa Agano la Kale Yoeli alielezea nyakati zetu—”siku ya Bwana”— kama “siku ya giza na huzuni” na “kuu na yenye kitisha” (Yoel 2:1–2, 11). Lakini hiyo haimaanishi siku zetu hazina tumaini. Fikiria ahadi hii ya Mzee Dieter F. Uchtdorf: “Ingawa nyakati fulani tunaweza kuhisi kuzikwa na majaribu ya maisha au kuzungukwa na giza la kimhemko, upendo wa Mungu na baraka za injili ya urejesho ya Yesu Kristo zitafanya kitu kisichofikirika kuchipuka” (“Mungu Atafanya Kitu Kisichofikirika,” Liahona, Nov. 2020, 52).

Kwa hiyo unapoona giza na huzuni wa nyakati zetu, kumbuka kwamba Bwana pia ameahidi baraka kuu—hata zisizofikirika: “Nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu na mabinti zenu watatabiri” (Yoeli 2:28; ona pia Joseph Smith—Historia 1:41). Tazama ahadi mahususi ambazo Roho wa Mungu atamiminwa juu ya wavulana na wasichana. Kwa nini unahisi ni muhimu kwa wale unaowafundisha kuelewa hilo? Tafakari swali hili unaposoma Yoeli 2 na ujumbe wa Mzee Uchtdorf katika maandalizi yako ya kufundisha.

wavulana akijifunza maandiko

Bwana ameahidi kwamba katika siku za mwisho, Yeye atamimina Roho Wake, na “wana wenu, na mabinti wenu, watatabiri” (Yoeli 2:28).

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema Yoeli 2:28–29, unaweza kuweka kitu katika bakuli na kumwacha mtu mwingine amimine maji juu yake. Ni kwa jinsi gani hii inatusaidia kuelewa kile inachomaanisha “kumimina roho [Wake] juu ya wote wenye mwili”? Ni kwa jinsi gani unabii katika Yoeli 2:28–29 unatimizwa? Hapa ni baadhi mawazo ambayo yanaweza kuwasaidia vijana kuelewa jinsi Bwana anavyomimina Roho Wake leo.

  • Maandiko yameandikwa mifano mingi wakati Bwana alimimina Roho Wake juu ya watu Wake. Kupitia tena baadhi ya hizi kungeweza kuwasaidia vijana kuelewa vyema jinsi ya kupokea mmininiko wa Roho wa Mungu katika maisha yao. Fikiria kuchora ubaoni birika kubwa ikimimina maji na kuwaomba watu au vikundi vidogo kusoma moja au zaidi ya vifungu vya maandiko katika “Nyenzo Saidizi.” Wangeweza kuandika ubaoni kuzunguka birika kile watu katika kifungu cha maandiko walifanya ili Bwana aweze kumimina Roho Wake na pia zile baraka zilizofuata. Ni lini tulihisi Roho akitufariji, kutuongoza, au kututakasa?

  • Unaweza kuandika maneno haya kutoka kwa Mzee Dieter F. Uchtdorf ubaoni: “Mungu ana kitu kisichofikirika akilini kwa ajili yako binafsi na Kanisa kwa ujumla—kazi ya kushangaza na maajabu” (“Mungu Atafanya Kitu Kisichofikirika,” 53). Fikiria kuwaomba vijana kutafuta katika ujumbe wa Mzee Uchtdorf baraka zisizofikirika Mungu alizitoa kwa watu katika maandiko baada ya nyakati za magumu. Ni nini Mzee Uchtdorf alitufundisha kufanya ili tufanye maamuzi mazuri wakati tunakabiliana na magumu? Waalike vijana watengeneze orodha ya vitu “visivyofikirika” Mungu anaweza kuwa navyo akilini kwa ajili yetu. Waalike wale unaowafundisha kutafakari kile wako radhi kufanya ili kupokea baraka hizi.

  • Fikiria kuonyesha video “Rais Nelson: Msikilize Yeye—Ufunuo Binafsi” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe vijana kusikiliza kwa ajili ya umaizi kuhusu jinsi Roho huzunngumza nasi na jinsi Yeye hubariki maisha yetu. Wanaweza pia kupitia tena ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Ufunuo kwa Ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa Ajili ya Maisha Yetu” (Liahona, Mei 2018, 93–96). Waombe watafute majibu kwa maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani Rais Nelson hutafuta na kupokea minong’ono ya Roho? Tunajifunza nini kutoka kwa Joseph Smith kuhusu utayari wa Mungu kuzungumza na watoto Wake? Ni nini Rais Nelson ametusihi tufanye? Waambie vijana kuhusu wakati ambapo ulihisi Bwana akimimina Roho Wake. Waalike wao kutafakari uzoefu walioupata, kama wanahisi sawa, waushiriki.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Kwa nyongeza kuwasaidia wanaojifunza kuhisi na kumtambua Roho, wasaidie kutenda juu ya ushawishi wanaoupokea” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi 10).