Agano la Kale 2022
Novemba 27. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kushiriki Injili? Yona; Mika


“Novemba 27. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kushiriki Injili? Yona; Mika,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni na Darasa la Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)

“Novemba 27. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kushiriki Injili? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022

Picha
wasichana wakiongea

Novemba 27

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kushiriki Injili?

Yona; Mika

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Je, ni kwa jinsi gani tumekaribia Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?

  • Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni nani amekuwa katika akili zetu karibuni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watu hawa?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kujifunza kuhusu Kanisa?

  • Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina mababu na ndugu zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa Akidi au darasa kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Fundisha Mafundisho

Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kunaweza kuwa na washiriki wa darasa lako ambao kila mara wanatafuta njia za kushiriki injili. Labda unafanya hivyo pia! Kwa watu wengi, hata hivyo, kushiriki injili ni vigumu na hata kunaogofya. Bahati nzuri, sisi wote tunaweza kuwa bora katika kushiriki imani yetu katika Yesu Kristo. Unaweza kuwa kimwili usisikie sauti ya Bwana akikuamuru kufanya kitu fulani kama vile “ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake” kama Yona alivyofanya (Yona 1:2). Lakini sauti ndogo tulivu ya Roho Mtakatifu inaweza kukupa msukumo wa “kuondoka na kwenda” kwa wanafamilia na marafiki mahususi ambao wameandaliwa kusikia ushuhuda wako. Uwe tayari kwa kile unachoweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Yona unapojifunza wiki hii, na kujiaandaa mwenyewe kushiriki kile unachojifunza pamoja na wale unaowafundisha. Unaweza pia kusoma ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Kushiriki Ujumbe wa Urejesho na Ufufuo” (Liahona, Mei 2020, 110–13).

Picha
wavulana akijifunza maandiko

Roho Mtakatifu anaweza kutupatia msukumo kushiriki injili na wale ambao wameandaliwa kusikiliza shuhuda zetu.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kushiriki misukumo yao kutokana na kujifunza juu ya Yona wiki hii, ungeweza kuonyesha picha ya Yoha (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waalike kujadili kile walichojifunza kuhusu kushiriki injili kutokana na uzoefu wa Yona. Unaweza kuwaalika kimahususi kupitia tena Yona 1 na3 na kuuliza: Ni nini tunachojifunza kuhusu kushiriki injili na wale ambao wanaweza kuonekana hawako tayari kubadilika? Tunajifunza nini kuhusu utayari wa Mungu kuwasamehe wale ambao wanatubu? Ili kuwatia moyo washiriki wa darasa lako au akidi kushiriki injili, tumia moja au zaidi ya shughuli zifuatazo au buni moja yako mwenyewe.

  • Ili kupata mawazo kuhusu jinsi ya kushiriki injili ya Mwokozi na wengine, darasa lako au akidi ingepitia tena matukio yafuatayo katika maandiko: Yohana 4:3–26; Matendo ya Mitume 16:25–33; Alma 19:14–18, 28–31. Kisha mngeweza kujadiliana pamoja maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani watu katika matukio haya walijiandaa kusikia ujumbe wa injili? Je, unaona nini kuhusu jinsi ujumbe huu ulivyoshirikiwa? Kwa nini unafikiria Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka sisi tushiriki injili? Kisha mnaweza kujadili kama darasa au akidi kile matukio haya yanatufundisha kuhusu jinsi tunaweza kushiriki injili leo.

  • Kusoma mifano inayovutia ya wengine wakishiriki injili kunaweza kuwatia moyo vijana unaowafundisha kufanya vivyo hivyo. Mzee D. Todd Christofferson alishiriki mifano kadhaa katika ujumbe wake “Kushiriki Ujumbe wa Urejesho na Ufufuo.” Katika ujumbe huu, Mzee Christofferson alifundisha kwamba vitu vitatu vilihitajika ili kuifanya mialiko yetu ya kupokea injili kuvutia sana: upendo wetu, mifano yetu, na matumizi yetu ya Kitabu cha Mormoni. Jadili mifano ya kushiriki injili katika ujumbe huu, na uwaalike wale unaowafundisha kushiriki mifano ingine, ikijumuisha uzoefu wa kibinafsi. Ni kwa jinsi gani uzoefu huu unaonyesha hivi vitu vitatu vilivyofundishwa na Mzee Christofferson?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa kwamba kushiriki injili kunaweza kuwa kwa kawaida na hakuhitaji kuogofya? Unaweza kuonyesha video katika “Nyenzo Saidizi” na kuwaomba vijana wafikirie kuhusu jinsi wanaweza kushiriki injili na mtu wanayemjua. Tunaweza kufanya nini kuwaalika wao waje na kuona? Ni fursa gani walizonazo za kuja na kusaidia? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wao kuhisi hamu ya kuja na kubakia? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kushiriki injili kuwa sehemu ya maisha yetu?

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

“Kuna uwezekano mkubwa wa watu kufanya mabadiliko ya maana katika maisha yao wakati mabadiliko hayo yanatokana na haki yao ya kujiamulia. Wakati unapotoa mialiko ya kutenda, hakikisha unaheshimu haki ya kujiamulia ya wale unaowafundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).

Chapisha