“Desemba 11. Je, Mimi Ninaweka Mambo ya Mungu Kwanza katika Maisha Yangu? Hagai; Zekaria 1–3; 7–14,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022 (2021)
“Desemba 11. Je, Mimi Ninaweka Mambo ya Mungu Kwanza katika Maisha Yangu? Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2022
Desemba 11
Je, Mimi Ninaweka Mambo ya Mungu Kwanza katika Maisha Yangu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa akidi au wa darasa; dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhamira ya Wasichana au Dhamira ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona General Handbook, 10.2, 11.2, ChurchofJesusChrist.org). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni mada gani uaskofu umejadili katika mikutano ya baraza la vijana la kata yenu? Ni hatua gani tunaweza kuchukua kulingana na mjadala huo?
-
Utunzaji wa wale walio na mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafikia watu katika njia za kama Kristo wakati tunaona hitaji na hatujui cha kusema?
-
Waalike wote kuipokea injili. Je, tumepata nini kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambacho hutuletea shangwe? Je, tunawezaje kushiriki upendo Wake na wengine?
-
Unganisha familia milele. Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kupata majina ya mababu zao?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Ikiongozwa na mtu mzima au kijana; dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Maisha yamejaa vitu muhimu vya kufanya. Kama hatutakuwa makini, shughuli nyingi za maisha zinaweza kutufanya tusahau madhumuni ya maisha. Tunajua kwamba Mwokozi na injili Yake inapaswa kuwa kipaumbele chetu, lakini vitu vingine kiurahisi vinaweza kutuchanganya. Labda hiyo ndiyo sababu maandiko yanatushauri sisi “Ulisawazishe pito la mguu wako” (Mithali 4:26), “Zitafakarini njia zenu” (Hagai 1:5), na “jijaribuni wenyewe kama mmekuwa katika imani” (2 Wakorintho 13:5).
Waisraeli walioishi nyakati za Hagai walihitaji aina hii ya mwaliko. Katika juhudi zao za kufaa za kuijenga tena Yerusalemu, iliwabidi waache kujenga tena nyumba ya Bwana. Fikiria jinsi gani maonyo ya Bwana katika Hagai 1 yanaweza kutumika kwetu leo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwatia moyo wale unaowafundisha kutathimini sharti la kuweka vitu vya Mungu kwanza katika maisha yao? Unaweza kupitia tena ujumbe wa Mzee Dake G. Renland “Msimamo Thabiti kwa Yesu Kristo” (Liahona, Nov. 2019, 22–25) au Mafundisho ya Rais Ezra Taft Benson katika “The Great Commandment—Love the Lord” (katika Teachings of Presidents of the Church: Ezra Taft Benson [2014], 37–45).
Jifunzeni Pamoja
Ungeweza kuanzisha mjadala kwa kuandika virai kutoka katika Hagai 1:6 ubaoni. Ni nini tunachoweza kujifunza kutoka kwa mawazo haya—kupanda mbegu na kamwe kutovuna, kula na kamwe kutoshiba, au kuchuma fedha lakini kuziweka kwenye mkoba ulio na mashimo—kuhusu kutumia muda na vitu vingine badala ya vile Bwana anatutaka tufanye? Wakati Bwana hatuombi kufokasi juu ya kujenga hekalu, ni nini Yeye anatuomba kuvifokasi? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya vitu hivyo kuwa kipaumbele kikuu katika maisha yetu? Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia vijana kutathimini sharti lao la kuweka vitu vya Mungu kuwa kwanza katika maisha yao.
-
Kushiriki sakramenti ni nafasi bora sana ya kila wiki ya kutathimini sharti letu kwa Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia sakramenti kuchunguza kama tunakuwa zaidi kama Mwokozi? Pengine vijana wangeweza kushiriki jinsi wanavyofanya hivyo. Wangeweza pia kutengeneza orodha ya maswali wangeweza kujiuliza wenyewe wakati wa sakramenti. Waalike kutafakari moja au zaidi ya maadiko, jumbe, au nyenzo zingine katika “Nyenzo Saidizi” wanapotengeneza orodha zao.
-
Rais Dieter F. Uchtdorf, katika ujumbe wake “Juu ya Vitu Vilivyo Muhimu Sana” (Liahona, Nov. 2010, 19–22), alishiriki ushauri ambao ungeweza kuwasaidia vijana “kutafakari njia [zao]” (Hagai 1:5). Unaweza kuwaalika watu binafsi au vikundi vidogo kusoma sehemu tatu za mwisho za hutoba (kuanzia na sehemu “Nguvu za Msingi”), wakitafuta kile inachomaanisha kufokasi maisha yetu kwa Mwokozi. Wangeweza kushiriki kitu fulani wanachohisi kuwavutia kukifanya ili kuimarisha sharti lao kwa Yesu Kristo.
-
Wengi wetu tunafanya shughuli nyingi mzuri. Lakini daima si vitu bora. Fikiria kushiriki kauli kutoka katika sehemu ya kwanza ya ujumbe wa Dallin H. Oaks “Nzuri, Bora, Bora Sana” (Liahona, Nov. 2007, 104–8) ambayo inaweza kuwasaidia vijana kuelewa kanuni hii. Unaweza pia kuwaalika kutengeneza orodha ya shughuli zao za kila siku. Waombe wao wajitathimini kibinafsi kama kila shughuli ni “nzuri,” “bora,” au “bora sana.” Ni nini kinachoifanya shughuli kuwa “bora sana”? Wahimize vijana kushiriki mmoja na mwingine kile wanachojifunza kutokana na hii tathimini binafsi.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wao wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Yoshua 24:14–15; Mathayo 6:19–34; 22:36–40; Mark 10:17–22; 1 Wakorintho 11:23–28; 2 Wakaorintho 13:5; Wakosai 3:1–2 (Tunapaswa kuviweka vitu vya Mungu kwanza katika maisha yetu)
-
Scott D. Whiting, “Kuwa Kama Yeye,” Liahona, Nov. 2020, 12–15
-
“As Now We Take the Sacrament,” Hymns, no. 169