Agano Jipya 2023
Julai 9. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anaongoza Kanisa Lake? Matendo ya Mitume 1–5


“Julai 9. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anaongoza Kanisa Lake? Matendo ya Mitume 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Julai 9. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anaongoza Kanisa Lake?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Mtume Paulo akizungumza na umati

Baada ya Ufufuko Wake, Mwokozi aliongoza Kanisa Lake kupitia Mitume Wake akiwemo Petro.

Julai 9

Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anaongoza Kanisa Lake?

Matendo ya Mitume 1–5

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni mada gani uaskofu umejadili katika mikutano ya baraza la vijana la kata yenu? Tunaweza kufanya nini kama darasa au akidi kulingana na umuhimu wa mijadala hiyo?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafikia watu katika njia za kama Kristo wakati tunaona hitaji na hatujui cha kusema?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tumepata nini kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambacho kinatuletea shangwe? Je, tunawezaje kushiriki shangwe hiyo na wengine?

  • Unganisha familia milele. Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kupata majina ya mababu zao?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Ni kitu kimoja kujua kwamba Kanisa ni zuri, kwamba Kanisa linafudisha kanuni za kweli, au Kanisa linaweza kukusaidia kuwa mtu bora. Ni kitu kingine kujua kwamba Kanisa leo kiuhalisia ni Kanisa la Yesu Kristo, lililoanzishwa Naye na linaongozwa binafsi na kwa muendelezo Naye kupitia nabii aliye hai. Kitabu cha Matendo ya Mitume hutoa ushahidi mwingi kwamba Mwokozi kwa undani anajihusisha katika kuongoza Kanisa Lake. Unapojifunza sura ya 1–5, tafuta ushahidi huo, na tafakari jinsi unajua kwamba Yeye anaendelea kuongoza Kanisa Lake leo. Ni kwa jinsi gani elimu hii imekubariki wewe?

Je, vijana unaowafundisha wanao ushuhuda kwamba Kanisa walilo ndani yake linaongozwa na Mwokozi Mwenyewe? Ni kwa namna gani ushuhuda kama huu huwabariki? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wao kupata au kuimarisha ushuhuda huu? Kama nyongeza ya kujifunza Matendo ya Mitume 1–5, ungeweza pia kusoma ujumbe wa Mzee Quentin L. Cook “Baraka ya Ufunuo Endelevu kwa Manabii na Ufunuo Binafsi wa Kuongoza Maisha Yetu” (Liahona, Mei 2020, 96–100).

Jifunzeni Pamoja

Ili kuanza majadiliano yako, ungeweza kuandika ubaoni Yesu Kristo analiongoza Kanisa Lake kupitia ufunuo kwa Manabii Wakei. Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kushiriki kitu walichopata katika kujifunza kwao kwa Matendo ya Mitume1–5 ambacho kinaunga mkono kauli hii. (Kama inahitajika, ungeweza kuwaelekeza wao kwenye Matendo ya Mitume 1:1–8; 2:36–39; 4:1–13, 31–33.) Je, ni ushahidi gani tunaouona kwamba Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake katika njia hiyo hiyo leo? Shughuli kama zifuatazo pia zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuimarisha imani yao katika ukweli huu muhimu.

  • Ungeweza kuandaa maswali kadhaa kama haya: Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo Anaongoza Kanisa Lake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuongeza imani yetu kwamba Yesu Kristo anaongoza Kanisa Lake? Kwa nini tunawaamini manabii na mitume wa Bwana? Mpe kila mshiriki wa darasa au akidi mojawapo ya maswali, na waalike wao kutafakari swali hili na kufikiria maandiko ambayo yangeweza kuwasaidia kulijibu (kama inahitajika, ona “Nyenzo Saidizi” kwa ajili ya baadhi ya mawazo). Kisha mpe kila mmoja muda wa kushiriki na kujadili kile wamejifunza.

  • Ili kusaidia darasa au akidi kuona jinsi Bwana huongoza Kanisa Lake, ungeweza kuwaalika kupitia tena sehemu ya kwanza ya ujumbe wa Mzee Quentin L. Cook “Baraka ya Ufunuo Endelevu kwa Manabii na Ufunuo Binafsi wa Kuongoza Maisha Yetu.” Pengine kila mshiriki wa darasa au akidi angeweza kushiriki kitu fulani kutoka katika ujumbe huu ambacho huwasaidia wao kujua kwamba Yesu Kristo analiongoza binafsi Kanisa Lake Ni umaizi gani mwingine tunapata katika maandiko katika “Nyenzo Saidizi”?

  • Ingeweza pia kuwa msaada kwa vijana kujifunza zaidi kuhusu jinsi Bwana anaongoza kata yako. Ungeweza kuwaomba vijana kushiriki mifano ya jinsi Bwana anavyowaongoza viongozi binafsi wa kata, ikijumuisha rais wa darasa au akidi. Wakati wa wiki kabla ya darasa, ungeweza kuwaomba baadhi ya viongozi wa kata kushiriki—ana kwa ana au kieletroniki kile kinaonyesha jinsi Bwana anawaongoza. Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kupata mifano ya ziada katika ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Bwana Huongoza Kanisa Lake” (Liahona, Mei 2017, 81–84). Kwa nini ni muhimu kuwa na imani kwamba Bwana anawapatia mwongozo viongozi wake wa kata?

  • Baadhi ya watu uhisi kwamba kama sisi tu watu wazuri na kufanya mambo mazuri, hatuhitaji kanisa. Ungeweza kuwauliza vijana jinsi wangehisi kujibu hivi. Katika ujumbe wake “Haja ya Kanisa” (Liahona, Nov 2021, 24–26), Rais Dallin H. Oaks alitoa sababu kadhaa kwa nini makanisa, ikijumuisha Kanisa la Bwana lililorejeshwa, ni muhimu. Vijana wangeweza kupekua ujumbe huu katika majozi, makundi madogo, au kama darasa au akidi na kushiriki kile wanachopata.

Picha
vijana wakikutana

Bwana analiongoza Kanisa Lake kupitia ufunuo, ikijumuisha urais wa darasa au akidi.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kumwalika Roho Mtakatifu katika kufundisha kwako, wahimize wengine kushiriki ushuhuda wao binafsi juu ya kweli unazojadili.

Chapisha