“Juni 25. Upatanisho wa Yesu Kristo Una Maana Gani Kwangu Mimi? Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Juni 25. Upatanisho wa Yesu Kristo Una Maana Gani Kwangu Mimi?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Juni 25
Upatanisho wa Yesu Kristo Una Maana Gani Kwangu Mimi?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Je, ni kwa jinsi gani tumekaribia Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?
-
Kuwajali wenye mahitaji. Ni nani amekuwa katika akili zetu karibuni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaida watu binafsi?
-
Waalike wote kuipokea injili. Je, tunaweza kujibu maswali ya marafiki zetu kuhusu Kanisa katika njia ambayo inaimarisha imani yao katika Mwokozi?
-
Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina babu na binamu zetu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Mzee David A, Bednar alisema kwamba baadhi ya Watakatifu wa Siku za Mwisho “wanaonekana kuwa na imani katika Mwokozi, lakini hawaamini ahadi za baraka Zake zipo kwa ajili yao au zinaweza kufanya kazi katika maisha yao” (“Kama Mngenijua,” Liahona, Nov 2016, 104). Kwa maneno mengine, hata ingawa tunaamini kwamba Yesu Kristo aliteseka na kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, tungeweza kushangaa kama Yeye aliteseka na kufa mahsusi kwa ajili ya dhambi zetu. Je, ninyi kamwe mmehisi hivyo? Ni kwa jinsi gani watu katika darasa lako au akidi yako wangefaidika kutokana na kuelewa kwamba Upatanisho wa Mwokozi hutumika kwao binafsi. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia?
Tafakari maswali haya unaposoma kuhusu Kusulubiwa kwa Mwokozi wiki hii. Unapojiandaa kufundisha kuhusu asili binafsi ya Upatanisho wa Kristo, ungeweza kujifunza ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Je, Mwokozi Amaefanya Nini Kwa Ajili Yetu?” (Liahona, Mei 2021, 75–77).
Jifunzeni Pamoja
Waalike washiriki wa darasa au akidi kushiriki kitu walichojifunza wiki hii kuhusu Kusulubiwa kwa Mwokozi katika Agano Jipya na hisia zao kuhusu Mwokozi. Ili kusaidia kuwasukuma, ungeweza kuuliza swali kama “Je, Ni nini tunajifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka katika vitu Yeye alivyosema na kufanya wakati wa saa Zake za mwisho?” Kwa mfano, mngeweza kuchunguza wakati Mwokozi, huku akiteseka kwa ajili ya wote, bado aliwatazama wale waliomzunguka Yeye kwa huruma (ona, kwa mfano, Luka 23:34, 39–43; Yohana 19:25–27). Hii inaweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo ni kwa wote na pia kibinafsi. Shughuli kama hii ifuatayo inaweza kukusaidia kuendeleza kujadili Upatanisho wa Mwokozi.
-
Katika aya ya kwanza ya ujumbe wake “Je, Mwokozi Amaefanya Nini Kwa Ajili Yetu?,” Rais Dallin H, Oaks alielezea maongezi na mwanamke ambaye alikuwa hasadiki kwamba Yesu Kristo alikuwa amefanya lolote kwa ajili yake. Pengine washiriki wa darasa au akidi wangeweza kusoma aya hiyo, wakijiweka katika nafasi ya Rais Oaks. Je tungesema nini kwa mwanamke huyu? Ungeweza kupangia kila mshiriki wa darasa au akidi kusoma mmoja kati ya sehemu zilizotajwa katika ujumbe wa Rais Oaks. Kutumia kile wanajifunza, pamoja na uzoefu wao wenyewe, wangeweza kisha kushiriki majibu yao wenyewe kwa swali “Yesu Kristo amefanya nini kwa ajili yangu mimi?”
-
Ili kuwatoa mwongozo katika mjadala kuhusu jinsi Upatanisho wa Mwokozi hutuathiri binafsi, ungeweza kuandika ubaoni kirai kama Kwa sababu Yesu Kristo aliteseka na kufa kwa ajili ya watu wote … . Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kupendekeza njia za kukamilisha sentensi hizi. Kisha ungeweza kubadilisha kirai kusomeka Kwa sababu Yesu Kristo aliteseka na kufa kwa ajili yangu … na uliza mapendekezo ya ziada. Washiriki wa darasa lako au akidi wanaposoma kauli hizi, wahimize wao kusoma maandiko katika “Nyenzo Saidizi.” Maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu ushawishi wa Upatanisho wa Mwokozi katika maisha yetu binafsi?
-
Njia nyingine ya kujifunza maandiko katika “Nyenzo Saidizi” ingeweza kuwa kuwaalika vijana kubadilisha maneno katika mistari hii ili kwamba mistari iwalenge wao moja kwa moja. Ni kwa jinsi gani hii inaathiri hisia zetu kuhusu kweli katika mistari hii? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha shukrani zetu kwa ajili ya dhabihu ya Mwokozi kwa ajili yetu?
-
Muziki mtakatifu unaweza kushuhudia kwa nguvu sana juu ya Yesu Kristo. Fikiria kualika washiriki wa darasa au akidi kuja kama wamejiandaa kushiriki nyimbo za dini ambazo zinawasaidia wao kuhisi nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi katika maisha yao wenyewe. (Wangeweza kutafuta nyimbo takatifu au ingizo “Jesus Christ—Savior” katika kielezo cha mada cha Nyimbo.) Waombe washiriki wa darasa au akidi kutambua virai katika nyimbo ambavyo vinawasaidia wao kuhisi upendo wa Mwokozi kwao binafsi. Ungeweza pia kuzungumza kuhusu jinsi dhabihu ya Mwokozi inaathiri maisha yetu ya kila siku. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani hii inashawishi chaguzi tunazofanya?
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
1 Wakorintho 15:20–22; 2 Wakorintho 12:7–9; Alma 7:11–12; 3 Nefi 11:10–11
-
Tad R. Callister, “Upatanisho wa Yesu Kristo,” Liahona, Mei 2019, 85–87