Agano Jipya 2023
Julai 23. Inamaanisha Nini Kuwa Mwanafunzi wa Yesu Kristo? Matendo ya Mitume 10–15.


“Julai 23. Inamaanisha Nini Kuwa Mwanafunzi wa Yesu Kristo? Matendo ya Mitume 10–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Julai 23. Inamaanisha Nini Kuwa Mwanafunzi wa Yesu Kristo?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Yesu na wafuasi

Yesu na Wanafunzi Wake, © Balage Balogh/Art Resource, NY

Julai 23

Inamaanisha Nini Kuwa Mwanafunzi wa Yesu Kristo?

Matendo ya Mitume 10–15.

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayopitia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia tekinolojia kama chombo cha kushiriki injili?

  • Unganisha familia milele. Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja kwa Kristo?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Sura ya 11 ya Matendo ya Mitume inasema kwamba kwa mara ya kwanza “wanafunzi waliitwa Wakristo” (mstari wa 26). Ni fursa na ni wajibu mtakatifu kujulikana kama mmoja wa wanafunzi wa Kristo na kuitwa kwa jina Lake. Kama Rais M. Russell Ballard alisema: “Je, tunafahamu jinsi tumebarikiwa kujichukulia juu yetu jina la Mwana wa Mungu wa Mpendwa wa Pekee? Je, tunaelewa jinsi hiyo ilivyo muhimu? Jina la Mwokozi ndilo jina la pekee chini ya mbingu ambalo kwalo mtu anaweza kuokolewa” (“Umuhimu wa Jina,”,” Liahona, Nov 2011, 79).

Inamaanisha nini kuwa Mkristo—mwanafunzi wa Yesu Kristo? Je, inamaanisha nini kwa washiriki wa darasa lako au akidi yako? Ni kwa jinsi gani kujichukulia jina Lake juu yako mwenyewe kunakushawishi? Ungeweza kufikiria pia nyakati ambapo wewe ulipata mwongozo na mfano wa mtu fulani ambaye alitenda kama mwanafunzi wa kweli wa Kristo.

Unapojiandaa kufundisha, kama nyongeza ya kusoma Matendo ya Mitume 10–15, fikiria kusoma ujumbe mmoja au zaidi ya mkutano mkuu unaopatikana katika “Nyenzo Saidizi.”

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kuelewa kile inamaanisha kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo, ungeweza kuwaalika wao kukamilisha kauli hii: “Mwanafunzi wa Yesu Kristo ni mtu ambaye …” Wanaweza kupitia tena Matendo ya Mitume 11:19–26, wakitafuta umaizi katika mstari wa 21, 23–24, 26 kuhusu jinsi hawa waumini wa Kanisa walionyesha kwamba wao ni wanafunzi. Ni kwa jinsi gani kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo hushawishi mawazo na tabia zetu? Shughuli kama hizi zinaweza kuongeza katika majadiliano haya.

  • Ingeweza kuwa msaada kujadili mwanafunzi wa Yesu Kristo yuko vipi (ona kauli ya Mzee Robert D, Hales katika “Nyenzo Saidizi”). Ungeweza kuwaomba vijana kushiriki baadhi ya mafundisho ya Yesu Kristo ambayo yanawaongoza wao na baadhi ya vitu walivyojifunza kutoka kwa mfano Wake. Wangeweza kupekua maandiko katika “Nyenzo Saidizi,” au wengine wanawajua, kwa mawazo. Wangeweza kuorodhesha ubaoni kile walichojifunza kuhusu Mwokozi kutoka kwenye vifungu hivi. Wangeweza kisha kuongea kuhusu njia wanaweza kwa dhati kufuata mafundisho na mifano ubaoni.

  • Waombe washiriki wa darasa au akidi kufikiria kuhusu kile inamaanisha kuwa Mkristo. Wangeweza kutengeneza orodha ya sifa wangetarajia kupata katika maisha ya mtu ambaye humfuata Yesu Kristo (ona, kwa mifano, Yohana 13:34–35). Ungeweza kuwagawa vijana katika vikundi viwili na kuomba kila kikundi kusoma mojawapo wa vifungu vifuatavyo kwa ajili ya sifa za ziada wangeongeza katika orodha yao: Mzee Terence M. Vinson, “Wauasi wa Kweli wa Mwokozi” (Liahona, Nov. 2019, 9–11) na Mzee Massimo De Feo, “Upendo Msafi: Ni Ishara ya Kweli ya Mfuasi Halisi wa Yesu Kristo” (Liahona, Mei 2018, 81–83). Waalike vijana kutafakari kitu fulani kwenye orodha wangependa kuboresha.

  • Ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa au akidi kile inamaanisha kwao kuitwa na jina la Yesu Kristo. Pengine wangeweza kushiriki uzoefu walioupata wakati mtu fulani alijua wao ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Je, ni kwa jinsi gani tunahisi kuhusu kujulikana kama wafuasi wa Yesu Kristo na ni wa Kanisa Lake? Vijana wangeweza pia kuchunguza maandiko kadhaa au mojawapo ya ujumbe katika “Nyenzo Saidizi,” wakitafuta umaizi ambao unawapa mwongozo kuishi kiwango cha jina la Yesu Kristo, ambalo tunajichukulia juu yetu wenyewe. Je, ni kwa jinsi gani kuitwa kwa jina la Yesu Kristo kunathiri chaguzi tunazofanya?

wasichana wakitembea

Kama waumini wa Kanisa la Kristo, sisi ni wanafunzi Wake na tunaitwa kwa jina Lake.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kama mwalimu, unaweza kuhimiza majadiliano ya kuinua yaliyopambwa na uzoefu na ushuhuda wa wanafunzi.