2010–2019
Wote Sharti Wajichukulie juu Yao Jina Lilitolewa na Baba
Oktoba 2018


Wote Sharti Wajichukulie juu Yao Jina Lilitolewa na Baba

Jina la Mwokozi lina uwezo wa kipekee na muhimu. Ni jina pekee ambalo kupitia kwake wokovu unawezekana.

Wiki kadhaa zilizopita, nilishiriki katika ubatizo wa watoto kadhaa waliofikisha umri wa miaka nane. Walikuwa wameanza kujifunza injili ya Yesu Kristo kutoka kwa wazazi na walimu wao. Mbegu ya imani yao ndani Yake ilikuwa imeanza kukua. Na sasa walitaka kumfuata katika maji ya ubatizo ili wawe waumini wa Kanisa Lake la urejesho. Nilipokuwa nikitazama kutarajia kwao, niliwaza ni kiasi gani walielewa kuhusu mojawapo ya kipengele muhimu cha agano lao la ubatizo: kujitolea kwao kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo.

Kuanzia mwanzo, Mungu ametangaza umuhimu wa jina la Yesu Kristo katika mpango Wake kwetu sisi. Malaika alimfundisha baba yetu wa kwanza, Adamu, “Nawe utafanya yale yote uyafanyayo katika jina la Mwana, nawe utatubu na kumlingana Mungu katika jina la Mwana milele yote.”1

Nabii katika Kitabu cha Mormoni Mfalme Benyamini alifundisha watu wake, “Hakuna jina lingine litatolewa wala njia ingine wala mbinu yoyote ambayo wokovu utawashukia.”2

Bwana alirudia kusema ukweli huu kwa Nabii Joseph Smith: “Tazama, Yesu Kristo ndilo jina ambalo limetolewa na Baba, na hakuna jina lingine lililotolewa ambalo kwa hilo mwanadamu aweza kuokolewa.”3

Katika siku zetu, Rais Dallin H. Oaks amefundisha ya kwamba “wale ambao watakuwa na imani katika jina takatifu la Yesu Kristo na kuingia katika agano lake … wanaweza wakadai dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo.”4

Baba yetu wa Mbinguni anataka kuliweka hilo wazi kabisa kwamba jina la Mwana Wake, Yesu Kristo, sio tu jina moja miongoni mwa mengi. Jina la Mwokozi lina uwezo wa kipekee na muhimu. Ni jina pekee ambalo kupitia kwake wokovu unawezekana. Kwa kusisitiza ukweli katika kila maongozi ya Mungu, Baba Yetu mpendwa anawahakikishia watoto Wake wote kwamba kuna njia ya kurejea Kwake. Lakini kuwa na njia hakika haimanishi ya kwamba kurejea kwetu ni hakika na kutatendeka kwa kujiendesha. Mungu anatuelezea kitendo kinachohitajika: “Kwa hiyo, wanadamu wote yawalazimu kujichukulia juu yao jina ambalo limetolewa na Baba.”5

Ili kupata nguvu za kuokoa zinazokuja kupitia jina la Kristo, ni lazima “kujinyenyekeza [sisi wenyewe] mbele za Mungu … na wakija na mioyo iliyovunjika na roho zilizopondeka … na [tuwe] radhi kujichukulia juu [yetu] jina la Yesu Kristo” na hivyo basi kuhitimu, kama marafiki wangu wadogo wenye umri wa miaka minane, “wapokelewe kwa ubatizo katika kanisa lake.”6

Wale wote walio na dhamira ya kweli kujichukulia jina la Mwokozi juu yao ni lazima wastahiki na kupokea ibada ya ubatizo kama ushahidi wa kimwili kwa Mungu kuhusu uamuzi wao.7 Lakini ubatizo ni mwanzo tu.

Neno chukua si lenye kukaa tu. Ni neno la kitendo lenye maana nyingi.8 Vile vile, kujitolea kwetu ili kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo kunahitaji vitendo na vipimo vingi vya aina nyingi.

Kwa mfano, maana moja ya neno chukua ni kushiriki au kupokea ndani ya mwili wa mtu fulani, kama vile wakati tunapokunywa kinywaji. Kwa kujichukulia juu yetu jina la Kristo, tunajitolea kuchukua mafunzo Yake, tabia zake, na hatimaye upendo Wake ndani ya nafsi zetu ili viweze kuwa sehemu yetu. Hivyo basi, umuhimu wa mwaliko wa Rais Russell M. Nelson kwa vijana wakubwa “sali kwa nguvu [tafuta] kuelewa kile kila moja ya vyeo na majina [ya Mwokozi] inavyomaanisha kibinafsi [kwao],”9 na kwa kushiriki maneno ya Kristo katika maandiko, hasa Kitabu cha Mormoni.10

Maana nyingine ya neno chukua ni kumkubali mtu aliye katika wajibu fulani au kukubali ukweli wa dhana au kanuni. Wakati tunapojichukulia juu yetu jina la Kristo, tunamkubali kama Mwokozi wetu na kuendelea kukubali mafundisho Yake kama mwongozo wa maisha yetu. Katika kila uamuzi wa maana tunaofanya, tunaweza kuichukulia injili Yake kuwa ya kweli na kwa utiifu kuiishi kwa moyo wetu wote, uwezo, akili, na nguvu zetu zote.

Neno chukua linaweza pia maanisha kufungamana kwa mtu binafsi na jina au lengo fulani. Wengi wetu tumekuwa na uzoefu wa kuyachukua majukumu kazini au kujiunga na lengo au mabadiliko. Wakati tunapojichukulia juu yetu jina la Kristo, tunayachukua majukumu ya mfuasi wa kweli, tunatetea lengo Lake, na “kusimama kama mashahidi [Wake] nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote [sisi] tulipo.”11 Rais Nelson amesema kwa “kila msichana mkubwa na kila mvulana mkubwa … ajiunge na batalioni la vijana wa Bwana ili kusaidia kukusanya Israeli.”12 Na kila mmoja wetu ana shukrani kuitikia mwito wa kinabii wa kutumia jina la Kanisa Lake la urejesho jinsi ilivyofunuliwa na Mwokozi Mwenyewe: Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.13

Katika mchakato wa kujichukulia jina la Mwokozi juu yetu, ni lazima tuelewe kwamba njia ya Kristo na ya Kanisa Lake ni kitu kimoja. Haviwezi kutenganishwa. Vivyo hivyo, ufuasi wetu wa kibinafsi kwa Mwokozi na kushiriki kikamilifu katika Kanisa Lake pia haviwezi kutenganishwa Ikiwa tutalegea katika kujitolea kwetu kwa moja kati yake, kujitolea kwetu kwa nyingine kutafifia, hakika tu jinsi usiku unavyofuata mchana.

Baadhi wanasita kujichukulia jina la Yesu Kristo na njia Yake kwa sababu wanaiona kuwa nyembamba mno, yenye vikwazo, na kuwazuia. Kiukweli, kujichukulia juu yetu jina la Kristo kunaleta uhuru na kunapanua. Kunaamsha tamaa ambayo tulihisi wakati tulikubali mpango wa Mungu kupitia imani katika Mwokozi. Pamoja na tamaa hii mioyoni mwetu, tunaweza kugundua lengo halisi la vipaji, vipawa, uzoefu wa upendo Wake wenye kuimarisha, na kukuza ustawi wa wengine. Tunapojichukulia juu yetu jina la Mwokozi, kwa ukweli tunashikilia kila kilicho chema na kuwa kama Yeye.14

Ni muhimu kukumbuka ya kwamba kujichukulia jina la Mwokozi juu yetu ni agano na kujitolea—kuanzia agano tunalofanya wakati wa ubatizo. Rais Nelson alifundisha, “Kujitolea [Kwetu] kumfuata Mwokozi kupitia kufanya maagano Naye na kisha kuyaishi maagano hayo kutafungua mlango kwa kila baraka ya kiroho na fadhila iliyoko.”15 Mojawapo ya fadhila takatifu ya kujichukulia jina la Mwokozi juu yetu kupitia ubatizo ni fursa inayotoa kwa ibada inayofuata katika njia ya agano, kuidhinishwa kwetu. Wakati nilipomuuliza mmoja kati ya marafiki zangu wenye umri wa miaka minane kile ambacho kujichukulia jina la Kristo ilimaanisha kwake, alijibu kwa urahisi, “Inamaanisha ninaweza kuwa na Roho Mtakatifu.” Yeye alikuwa sawa.

Kipawa cha Roho Mtakatifu kinapokewa kupitia kuidhinishwa baada ya sisi kupokea bada ya ubatizo. Kipawa hiki ni haki na nafasi ya kuwa na Roho Mtakatifu kwa karibu kabisa kama mwenzi wa muda wote. Ikiwa tutasikiliza na kutii sauti Yake, ndogo tulivu, atatudumisha katika njia ya agano tuliyoingia kupitia ubatizo, hutuonya wakati tunajaribiwa kuondoka kwake, na kututia moyo kutubu na kurekebisha inapohitajika. Lengo yetu baada ya ubatizo ni kuwa na Roho Mtakatifu daima nasi ili tuweze kuendelea kusonga mbele kwenye njia ya agano. Roho Mtakatifu anaweza kuwa nasi tu kwa kiasi cha kwamba tunaweka maisha yetu safi na huru kutokana na dhambi.

Kwa sababu hii, Bwana ametoa njia ambayo kupitia kwake tunaweza kujikumbusha athari ya kusafisha ya ubatizo wetu kupitia ibada nyingine—sakramenti. Kila wiki tunaweza “kushuhudia … kwamba [sisi] tuko radhi kujichukulia juu [yetu] jina [la] Mwana16 tena, kwa kunyoosha mkono na kuchukua ishara ya mwili na damu ya Bwana mikononi mwetu—mkate na maji—na kupokea ndani ya nafsi zetu hasa. Kwa upande Wake, Mwokozi anatimiza muujiza wa kusafisha tena na hivyo kutufanya wastahiki wa ushawishi unaoendelea wa Roho Mtakatifu. Je, huu si ushahidi wa rehema isiyo na kifani inayopatikana tu katika jina la Yesu Kristo? Jinsi tu tunavyojichukulia juu yetu jina Lake, Yeye huchukua dhambi zetu na masikitiko yetu juu Yake, na bado “mkono Wake wa rehema umenyoshwa”17 kutuzingira katika mikono Yake ya upendo.18

Sakramenti ni ukumbusho wa kila wiki kwamba kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo ni kujitolea kwa maisha, si tukio moja ambalo linafanyika tu mara moja katika siku yetu ya ubatizo.19 Tunaweza kuendelea na kufurahia kila mara “ile dhabihu takatifu, inayoeleweka kwa kiasi kidogo zaidi na mwanadamu, kusamehewa dhambi zetu na kupokea mwili na damu Yake.”20 Si ajabu basi kwamba wakati wowote watoto wa Mungu wanapoelewa, baraka za nguvu za kiroho ambazo zinaweza kuja kwa sababu ya kujichukulia juu yao jina la Kristo, hisia yao daima ni shangwe na tamaa yao daima ni kufanya agano na Mungu wao.21

Tunapofuata njia hii takatifu iliyopangwa kutoka mbinguni, kujitolea na juhudi zetu kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo kutatupatia nguvu “kudumisha jina [Lake] limeandikwa mioyoni [mwetu].”22 Tutampenda Mungu na majirani zetu na kuhisi tamaa ya kuwahudumia. Tutatii amri Zake na tunatamani kusonga karibu Naye kwa kufanya maagano ya ziada Naye. Na tunapojikuta tukiwa wanyonge na tusioweza kutenda kulingana na matamanio yetu ya haki, tutasali kwa ajili ya nguvu zinazokuja tu kupitia jina Lake na Atakuja kutusaidia. Tunapovumilia kwa imani, siku itakuja wakati tutamuona, na tutafahamu ya kwamba tumekuwa kama Yeye, hivyo basi kutuhitimisha sisi kurejea katika uwepo wa Baba.

Kwa maana ahadi ya Mwokozi ni imara: wale “wanaoamini kwa jina la Yesu Kristo, na kumwabudu Baba katika jina lake, na kuvumilia katika imani kwa jina lake hadi mwisho”23 wataokolewa katika ufalme wa Mungu. Pamoja nanyi, ninafurahia ya kwamba baraka hizi ambazo hazina kifani zinawezekana kwa kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo, ambaye na ni katika jina lake ninashuhudia, amina.

Muhtasari

  1. Musa 5:8

  2. Mosia 3:17.

  3. Mafundisho na Maagano 18:23.

  4. Dallin H. Oaks, “Kujichukulia juu Yetu Jina la Yesu Kristo,” Ensign, Mei 1985, 82.

  5. Mafundisho na Maagano 18:24; mkazo umeongezewa.

  6. Doctrine and Covenants 20:37; emphasis added.

  7. Rais Dallin H. Oaks alifundisha: “Tunajichukulia juu yetu Jina la Mwokozi wetu wakati tunapokuwa washiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. … Kama waumini wa kweli katika Kristo, kama Wakristo, tumejichukulia jina lake juu yetu kwa furaha” (“Kujichukulia juu Yetu Jina la Yesu Kristo,” 80).

  8. Kamusi ya mtandaoni ya Merriam-Webster, inaorodhesha fafanuzi 20 za muundo elekezi wa kitenzi chukua, ambao ni muundo ambao kwao kitenzi kinatumika katika kirai “kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo.” (merriam-webster.com/dictionary/take).

  9. Russell M. Nelson, “Manabii, Uongozi, na Sheria Takatifu” (worldwide devotional for young adults, Jan. 8, 2017), broadcasts.lds.org.

  10. Russell M. Nelson, “Kitabu cha Mormoni: Maisha Yako Yangekuaje Bila Hicho? Liahona, Nov. 2017, 60–63.

  11. Mosia 18:9

  12. Russell M. Nelson, “Hope of Israel” (worldwide youth devotional, June 3, 2018), hopeofisrael.lds.org.

  13. Bwana alivutia akili yangu umuhimu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Tuna kazi mbele yetu ya kutuleta kwenye uwiano na mapenzi Yake” (Russell M. Nelson, katika “Jina la Kanisa” [official statement, Aug. 16, 2018], mormonnewsroom.org).

  14. Ona Moroni 7:19.

  15. Russell M. Nelson, “As We Go Forward Together,” Liahona, Apr. 2018, 7.

  16. Mafundisho na Maagano 20:77; mkazo umeongezewa.

  17. 3 Nefi 9:14 AM; ona pia Alma 27:-34.

  18. Ona 2 Nefi 1:15.

  19. “Tunaposhuhudia utayari wetu kujichukulia juu Yetu jina la Yesu Kristo, tunaonyesha kujitolea kwetu kufanya kila tunachoweza ili kufanikiwa kufanikiwa kupata maisha ya milele katika ufalme wa Baba. Tunaonyesha ugombeaji wetu—kujitolea kwetu kujitahidi kwa ajili ya—kuinuliwa katika ufalme wa selestia. …

    “… Kile tunachoshuhudia si kwamba tunajichukulia juu yetu jina lake lakini kwamba tuko tayari kufanya hivyo. Kwa namna hii, ushahidi wetu unahusiana na tukio fulani katika siku za usoni au hali ambayo kupatikana kwake si kupitia kujisadiki, lakini inategemea mamlaka au ari ya Mwokozi mwenyewe” (Dallin H. Oaks, “Kujichukulia juu Yetu Jina la Yesu Kristo,” 8283).

  20. “O God, the Eternal Father,” Nyimbo, na. 175.

  21. Ona Mosia 5; 6; 18; 3 Nefi 19.

  22. Mosia 5:12.

  23. Mafundisho na Maagano 20:29.

Chapisha