2010–2019
Kuweka Msingi wa Kazi Kubwa
Oktoba 2018


11:3

Kuweka Msingi wa Kazi Kubwa

Masomo yaliyofundishwa kupitia desturi zilizoanzishwa katika nyumba zetu, ingawa ni kidogo na rahisi, ni muhimu sana katika ulimwengu wa leo.

Kama wazazi katika Sayuni, tuna wajibu mtakatifu kuamsha shauku ndani ya watoto wetu na kujitolea kwa furaha, mwanga na ukweli wa injili ya Yesu Kristo. Tukiwa tunawalea watoto wetu, tulianzisha desturi katika nyumba yetu na tukaweka taratibu za mawasiliano na tabia ndani ya mahusiano yetu ya kifamilia. Kwa kufanya hivyo, desturi tulizozianzisha inabidi zitopee tabia thabiti, zizoyumba katika watoto wetu ambazo zitawatia moyo katika kukabiliana na changamoto za maisha.

Kwa miaka mingi familia yetu ilifurahia desturi za kila mwaka za kuweka kambi katika Milima ya Uintah kaskazini mashariki mwa Utah. Tunasafiri kwa maili (kilomita 32 ) juu ya njia ya mchanga na mawe ili kufika sehemu nzuri yenye uwanda wa kijani, kwenye mnara wa kuta za korongo na humo hutiririka mto wenye maji baridi, mazuri. Kila mwaka, tukitumaini kuimarisha thamani ya mafundisho na matendo ya injili katika mioyo ya watoto na wajukuu wetu, Susan nami tunawauliza kila mmoja wa watoto wetu sita na familia zao kuandaa ujumbe mfupi kwenye mada wanayoona ni jambo muhimu katika msingi wa maisha ya Kristo nyumbani. Kisha tunakusanyika kwa ibada ya familia kwenye sehemu iliyotengwa, na kila mmoja hutoa ujumbe wao.

Ujumbe ulioandikwa juu ya mawe

Mwaka huu, wajukuu wetu waliandika mada ya ujumbe wao kwenye mawe, na kisha, mmoja baada ya mwingine, walifukia karibu na mwingine, ikimaanisha msingi halisi ambao maisha ya furaha huanzishwa. Miongoni mwa jumbe zao zote sita kulikuwa na ukweli wa milele usiobadilika kwamba Yesu Kristo ni jiwe kuu la pembeni la msingi huo.

Katika maneno ya Isaya, “Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe la msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la thamani la pembeni, msingi imara.”1 Yesu Kristo ndiye jiwe la pembeni katika msingi wa Sayuni. Yeye ndiye aliyefunua kwa Nabii Joseph Smith: “Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu.”2

Masomo yaliyofundishwa kupitia desturi zilizoanzishwa katika nyumba zetu, ingawa ni kidogo na rahisi, ni muhimu sana katika ulimwengu wa leo. Je, ni mambo gani madogo na rahisi ambayo, yakianzishwa, yatafanya kazi nzuri katika maisha ya watoto wetu?

Rais Russell M. Nelson hivi karibuni alihutubia kusanyiko kubwa huko Toronto, Canada, na kwa uchungu aliwakumbusha wazazi juu ya majukumu matakatifu tuliyonayo ya kuwafundisha watoto wetu. Miongoni mwa majukumu muhimu yaliyoainishwa, Rais Nelson alisisitiza kazi ambazo tunazo kama wazazi ni kuwafundisha watoto wetu kuelewa kwa nini tunapokea sakramenti, umuhimu wa kuzaliwa katika maagano, na umuhimu wa kujiandaa na kupokea baraka za baba mkuu na, yeye aliwahimiza wazazi wake kuongoza katika kusoma maandiko pamoja kama familia.3. Kwa juhudi hizi, nabii wetu mpendwa ametuomba tufanye nyumba zetu kuwa “kimbilio la imani.”4

Katika Kitabu cha Mormoni, Enoshi anaandika juu ya shukrani nyingi alizohisi kwa ajili ya mfano wa baba yake, ambaye “alimfunnza [yeye] kwa lugha yake, na pia katika malezi na maonyo ya Bwana.” Kwa hisia kali Enoshi alitamka “Na jina la Mungu wangu libarikiwe kwa hayo.”5

Ninazitunza desturi ndogo ndogo na rahisi tulizozifuata katika nyumba yetu zaidi ya miaka 35 ya ndoa yetu. Desturi zetu nyingi ni nzuri na zina maana. Kwa mfano:

  • Wakati wa vipindi vya jioni nikiwa mbali na nyumbani, daima nilijua kwamba chini ya maelekezo ya Susan, mwana wetu mkubwa akiwepo angejichukulia juu mwenye kuiongoza familia katika kusoma maandiko na sala.6

  • Desturi ingine––hatuondoki nyumbani kwetu au kukata maongezi ya simu bila ya kusema, “Ninakupenda.”

  • Maisha yetu yamebarikiwa kwa kutenga muda kila wakati wa kufurahia usaili binafsi na kila mmoja wa wana wetu. Wakati wa usaili mmoja nilimwuliza mwana wetu kuhusu matamanio yake na maandalizi ya kuhudumu misheni. Baada ya majadiliano kadhaa, palitokea muda wa ukimya kidogo, kisha akajisogeza mbele na huku akifikiria alisema, “Baba, kumbuka nilipokuwa mdogo na kuanza kuwa na sahili wa baba?” Nikasema, “Ndiyo.” “Vizuri,” alisema, “Nilikuahidi wakati ule kuwa ningehudumu misheni, na uliniahidi kwamba wewe na Mama mngehudumia misheni mtakapokuwa wazee.” Kisha kulikuwa na maombi mengine.” “Je, ninyi mnamatatizo ambayo yatawazuia kutohudumu—kwa sababu huenda nikasaidia?”

Desturi nzuri za familia za kila mara zinajumuisha sala, kusoma maandiko, jioni ya familia, na kuhudhuria Kanisani, japokuwa inaonekana kama mambo madogo na rahisi, hujenga utamaduni wa upendo, kuheshimiana, umoja, na ulinzi. Katika roho ambayo hujumuisha juhudi hizi, watoto wetu walilindwa dhidi ya mishale ya moto ya adui ili kuingizwa katika utamaduni wa kidunia wa siku zetu.

Tunakumbushwa kuhusu ushauri wa busara wa Helamani kwa mwanawe: “Kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu; kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndio, mishale yake kimbungani, wakati mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, hautakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha, kwa sababu ya mwamba ambako kwake mmejengwa, ambao ni msingi imara, msingi ambako watu wote wakijenga hawataanguka.”7.

Miaka iliyopita, nikiwa ninahudumu kama askofu kijana, mzee mngwana mmoja aliomba kuonana na mimi. Alielezea kuondoka kwake Kanisani na desturi njema za wazazi wake wakati akiwa kijana. Alifafanua kwa undani maumivu ya moyo aliyoyaona wakati wa maisha yake wakati akijitahidi kutafuta furaha ya kudumu, katikati ya furaha ya muda ambayo ulimwengu unatoa. Sasa, katika miaka yake ya baadaye ya maisha, alipata hisia nyororo, wakati mwingine akiwa na hisia za kurudiwarudiwa za Roho wa Mungu akiumwongoza tena kwenye masomo, mazoea, hisia, na usalama wa kiroho wa ujana wake. Alionyesha shukrani kwa desturi za wazazi wake, na maneno ya kisasa, alisikiliza tangazo la Enoshi: “Heri jina la Mungu wangu kwa ajili yake.”

Katika uzoefu wangu, kurudi kwa mtu huyu mpendwa kwenye injili ni tabia ya wengi na hujirudia mara nyingi miongoni mwa watoto wa Mungu ambao huondoka kwa muda, kisha kurudi kwenye mafundisho na mazoea ya ujana wao. Wakati huo, tunashuhudia hekima ya mwandishi wa mithali, ambaye anawahimiza wazazi, “Mlee mtoto katika njia impasayo: Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”8

Kila mzazi anakabiliwa na wakati wa kuchanganyikiwa na viwango tofauti vya uamuzi na nguvu wakati akiwalea watoto. Hata hivyo, wakati wazazi wanafanya imani kwa kuwafundisha watoto kila mara, kwa uwazi, kwa upendo na kufanya yote wanayoweza kuwasaidia njiani, wanapata tumaini kubwa zaidi kwamba mbegu zilizopandwa zitapata mizizi ndani ya mioyo na mawazo ya watoto wao.

Musa alielewa haja ya msingi ya kufundisha kila mara. Alishauri, “Nawe uwafundishe [maneno haya] watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.”9

Tunapiga magoti karibu na watoto wetu wakati wa sala ya familia, tunawajali kupitia juhudi zetu za kusoma maandiko ya familia yenye manufaa, kwa uvumilivu, tunawajali kwa upendo kama vile tunavyoshiriki katika jioni ya familia, na tunahuzunika kwa ajili yao tunapopiga magoti katikati ya sala zetu binafsi za mbinguni. Ee, jinsi tunavyotamani kwamba mbegu tunayopanda itakita mizizi ndani ya mioyo na akili za watoto wetu.

Ninaamini kuwa ni swali dogo la iwapo watoto wetu “wanaelewa” miongoni mwa mafundisho yetu, kama vile wakati wanajitahidi kusoma maandiko au kuwa na jioni ya familia nyumbani au miradi ya Kutambua ya Wasichana na mikutano mingine ya Kanisa. Ni swali dogo la iwapo katika wakati huo wanaelewa umuhimu wa shughuli hizo na zaidi ni swali la iwapo, kama wazazi, tunaonyesha imani ya kutosha kufuata ushauri wa Bwana kwa kuishi kwa bidii, kufundisha, kuhimiza, na kuweka matarajio ambayo yanaongozwa na injili ya Yesu Kristo. Ni jitihada inayotokana na imani yetu––imani yetu kuwa siku moja mbegu zilizopandwa katika ujana wao zitakita mizizi na kuanza kuota na kukua.

Mambo tunayosema, mambo tunayayohubiri na kufundisha huamua mambo ambayo yatatokea kati yetu. Tunapotengeneza desturi nzuri zinazofundisha mafundisho ya Kristo, Roho Mtakatifu anatoa ushuhuda juu ya ukweli wa ujumbe wetu na inalisha mbegu za injili zilizopandwa ndani ya mioyo ya watoto wetu kwa jitihada zetu zote njiani. Mimi nashuhudia hivyo kwa jina la Yesu Kristo, amina.