Atavijumlisha Vitu Vyote Katika Kristo
Nguvu ya injili ya Mwokozi kubadilisha na kutubariki hutiririka kutoka kwenye utambuzi na kutumia uhusiano wa mafundisho, kanuni na matendo.
Kamba ni zana muhimu ambayo sote tunaitambua. Kamba zimetengenezwa kwa nyuzi, mimea, nyaya, au vitu vingine ambavyo kila kimoja hukunjwa au kusokotwa kwa pamoja. Cha kushangaza, vitu ambavyo haviwi vya kustaajabisha vinaweza kusukwa kwa pamoja na kuwa vyenye nguvu ya kustaajabisha. Hivyo, kwa kuunganisha kwa uthabiti au kufunga vitu vya kawaida kunaweza kuzalisha nyenzo imara zaidi.
Kama vile kamba ipatavyo nguvu kutoka kwenye nyuzi zilizofumwa, vivyo hivyo injili ya Yesu Kristo hutoa mtazamo mkuu wa kweli na hutoa baraka za thamani wakati tukifuata himizo la Paulo la “kuvijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo.”1 Muhimu, kusanyiko hili muhimu linajikita katika na kulenga kwa Bwana Yesu Kristo kwa sababu Yeye ni njia, kweli na uzima.”2
Ninasali kwamba Roho Mtakatifu atatuangaza kila mmoja wetu wakati tukifikiria jinsi gani kanuni ya kuvijumlisha vitu vyote katika Kristo itumikavyo katika kujifunza na kuishi injili Yake ya urejesho katika maisha yetu ya kila siku
Nyakati za Ufunuzi
Tunaishi katika nyakati zisizo na kifani na za ufunuzi wa Kanisa la Yesu Kristo. Marekebisho ya kihistoria yaliyotangazwa leo yana lengo kuu moja tu: kuimarisha imani katika Baba wa Mbinguni na Mpango Wake na katika Mwana Wake Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Ratiba ya mkutano wa Jumapili haitafupisha tu. Badala yake, sasa tuna ongezeko la fursa na majukumu kama watu binafsi na familia ya kutumia muda wetu kuiboresha Sabato kuwa furaha nyumbani na Kanisani.
Aprili iliyopita, mpangilio wa mfumo wa akidi za ukuhani haukuwa umebadilishwa tu. Badala yake, msisitizo na nguvu zilitolewa katika njia ya juu na takatifu ya kuhudumia kaka na dada zetu.
Kama vile nyuzi zilizosokotwa za kamba zinazalisha zana ya kudumu na imara, matendo yote haya yanayoshabihiana ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuweka uzingativu kiusahihi, nyenzo na kazi ya Kanisa la urejesho la Mwokozi pamoja na kazi yake ya msingi: kumsaidia Mungu katika kazi Yake ya kuleta ukombozi na kuinuliwa kwa watoto Wake. Tafadhali msizingatie kimsingi katika vipengele vya kiutendaji kama ilivyotangazwa. Ni lazima tusiruhusu maelezo ya utaratibu kutia kiza sababu kuu za kiroho mabadiliko haya sasa yanapofanywa.
Hamu yetu ni kwamba imani katika Mpango wa Baba na katika kazi ya ukombozi ya Mwokozi ingeweza kuongezeka katika dunia na kwamba agano la Mungu lisilo na mwisho lingeweza kuanzishwa.3 Malengo yetu pekee ni kusaidia mwendelezo wa uongofu katika Bwana na kupenda zaidi kikamilifu na kuwatumikia zaidi kaka na dada zetu.
Kugawanyisha na Kutenganisha.
Wakati mwingine kama waumini wa Kanisa tunagawanyisha, kutenganisha na kutumia injili katika maisha yetu kwa kutengeneza orodha ndefu ya mada binafsi za kusoma na kazi za kukamilisha. Lakini kwa njia hiyo inaweza kuzuia uelewa wetu na maono. Sisi sharti tuwe makini kwa sababu kuzingatia kifarisayo katika orodha kunaweza kututoa katika kumkaribia Bwana.
Lengo na utakaso, furaha na shangwe, na uongofu endelevu na ulinzi ambao huja kutokana na “kumtolea Mungu mioyo [yetu]”4 na “[kupokea] mfano Wake katika nyuso [zetu]”5 hakuwezi kupatikana kwa kufanya tu na kuangalia vitu vyote vya kiroho tunavyotakiwa kufanya. Badala yake, nguvu ya injili ya Mwokozi kubadilisha na kutubariki hutiririka kutoka kwenye utambuzi na kutumia uhusiano wa mafundisho, kanuni na matendo. Ni pale tu pekee tunapovijumlisha vitu vyote katika Kristo, tukilenga juu Yake kwa uthabiti, kweli za injili zinaweza kwa pamoja kutuwezesha kuwa vile Mungu anatamani tuwe6 na kuvumilia kiujasiri mpaka mwisho.7
Kujifunza na Kuunganisha Kweli za Injili
Injili ya Yesu Kristo ni kitambaa cha kushangaza chenye kweli “kikiwekwa vizuri”8 na kusukwa kwa pamoja. Tunapojifunza na kuunganisha kwa pamoja kweli za injili zilizofunuliwa, tunabarikiwa kupokea mtazamo wenye thamani na uongezeko la uwezo wa kiroho kupitia macho ambayo yanaweza kuona ushawishi wa Bwana katika maisha yetu na masikio yanayoweza kusikia sauti Yake.9 Na kanuni ya kuvijumlisha vitu vyote—naam katika yeye Huyo inaweza kutusaidia sisi katika kubadilisha orodha iliyozoeleka kuwa iliyounganishwa, kujumuishwa na kuwa kama nzima. Acha nitoe mifano yote kimafundisho na Kikanisa ya kile ninachopendekeza.
Mfano #1. Makala ya Imani ni moja kati ya vielelezo vikuu vya kujumlisha vitu vyote katika Kristo: “Tunaamini kwamba kanuni na ibada za kwanza za Injili ni: kwanza, Imani katika Bwana Yesu Kristo; pili, Toba; tatu, Ubatizo kwa kuzamishwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi; nne, Kuwekewa mikono kwa ajili ya kipawa cha Roho Mtakatifu.”10
Imani ya kweli inalenga katika Bwana Yesu Kristo—katika Yeye kama Mwana Mtakatifu na wa Pekee wa Baba na katika yeye katika kazi ya ukombozi Aliyoitimiza. “Kwani amejibu mwisho wa sheria, na hudai wale wote ambao wana imani ndani yake; na wale ambao wana imani ndani yake watajishikilia kwa kila kitu kizuri; kwa hivyo huzungumza akipendelea watoto wa watu.”11 Kutumia imani katika Yesu Kristo ni kuamini na kuweka kujiamini kwetu katika Yeye kama Mwokozi wetu, katika jina Lake, na katika ahadi Zake.
Tukio la kwanza na la kawaida la kuamini katika Mwokozi ni kutubu na kugeuka kutoka kwenye maovu. Wakati tunapotumia imani katika Bwana, kawaida tunageuka, kuja na kutegemea katika Yeye. Hivyo, toba ni kuamini na kutegemea katika Mkombozi kutufanyia kile ambacho hatuwezi kufanya sisi wenyewe. Kila mmoja wetu sharti “[ategemee] kabisa ustahili wa yule aliye mkuu kuokoa”12 kwa sababu ni kupitia “fadhili, na rehema, na neema za Masiya”13 tunaweza kuwa viumbe wapya katika Kristo14 na hatimaye kurudi na kuishi katika uwepo wa Mungu.
Ibada ya ubatizo kwa kuzamishwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi hutuitaji sisi kumuamini Yeye, kumtegemea Yeye na kumfuata Yeye. “Najua kwamba kama mtamtii Mwana, kwa moyo wa lengo moja, bila unafiki na udanganyifu mbele yake Mungu, lakini kwa kusudi kamili, na kutubu dhambi zenu, mkishuhudia kwa Baba kwamba mnataka kujivika juu yenu jina la Kristo, kwa ubatizo—ndio, kwa kumfuata Bwana wenu na Mwokozi wenu chini majini, kulingana na neno lake, tazameni, ndipo mtapokea Roho Mtakatifu; ndio, kisha ubatizo wa moto na Roho Mtakatifu unakuja.”15
Ibada ya kuwekewa mikono kwa ajili ya kipawa cha Roho Mtakatifu hutuitaji sisi kumuamini Yeye, kumtegemea Yeye, kumfuata Yeye, na kuendelea mbele tukiwa Naye na kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Kama Nefi alivyotangaza, “Na sasa … najua kwamba bila ya mwanadamu kuvumilia hadi mwisho, kwa kufuata mfano wa Mwana wa Mungu aliye hai, hawezi kuokolewa.”16
Makala ya nne ya imani haiainishi tu kiurahisi kanuni na ibada za msingi za injili ya urejesho. Badala yake, tamko hili la msukumo wa kiungu la imani hujumlisha vitu vyote katika Kristo: kumuamini Yeye, kumtegemea Yeye, kumfuata Yeye, na kuendelea mbele pamoja Naye—hata katika Yeye.
Mfano #2. Sasa nataka kuelezea jinsi gani programu za Kanisa na mipango inavyojumlishwa katika Kristo. Vielelezo vingine vingi vya ziada vingeweza kuwasilishwa; nitatumia tu baadhi.
Mnamo 1978, Rais Spencer W. Kimball aliwaelekeza waumini wa Kanisa kuijenga nguvu ya Sayuni ulimwenguni kote. Aliwashauri watakatifu kubakia katika nchi zao za kuzaliwa na kuanzisha vigingi kwa kuikusanya familia ya Mungu na kuwafundisha njia za Bwana. Zaidi alielekeza kwamba mahekalu zaidi yangejengwa na baraka zilizoahidiwa kwa watakatifu popote walipoishi ulimwenguni.17
Wakati idadi ya vigingi ikiongezeka, uhitaji uliongezeka wa nyumba za waumini “kuwa sehemu [ambazo] wanafamilia [wangependa] kuwepo, ambapo [wengeweza] kuimarisha maisha yao na kupata upendo wa pamoja, usaidizi, kukubalika, na kutiwa moyo.”18 Kwa sababu hiyo, mnamo 1980, mikutano ya Jumapili iliunganishwa kuwa katika saa tatu ili “kusisitiza majukumu binafsi na ya kifamilia kwa ajili ya kujifunza, kuishi na kufundisha injili.”19 Msisitizo huu tena juu ya familia na nyumbani uliimarishwa katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” iliyotambulishwa na Rais Gordon B. Hinckley mnamo 1995.20
Mnamo Aprili 1998, Rais Hinckley alitangaza ujenzi wa mahekalu mengine zaidi madogo, hivyo kuleta ibada takatifu za Nyumba ya Bwana karibu na Watakatifu wa Siku za Mwisho binafsi na familia kote ulimwenguni21 Na fursa hizi kwa ajili ya uendelevu na ukuaji wa kiroho zilisaidizwa na ongezeko la kujitegemea katika mahitaji ya kimwili kupitia uanzishwaji wa Mfuko Endelevu wa Elimu mnamo 2001.22
Wakati wa uongozi wake, Rais Thomas S. Monson kwa kurudia aliwahimiza watakatifu “kwenda kuokoa” na kusisitiza kuwajali masikini na wenye uhitaji kama mojawapo ya majukumu matakatifu ya Kanisa. Akiendelea na msisitizo juu kujiandaa katika mahitaji ya kimwili, mpango wa huduma ya Kujitegemea ulianzishwa mnamo 2012.
Kwa miaka kadhaa iliyopita, kanuni muhimu kuhusu kuitunza siku ya Sabato nyumbani na Kanisani zimekuwa zikisisitizwa na kuimarishwa,23 hivyo kutuandaa kwa ajili ya mikutano ya Jumapili iliyotangazwa kwenye sehemu hii ya mkutano mkuu.
Na miezi sita iliyopita, Akidi za ukuhani wa Melkizedeki ziliimarishwa na kuwekwa katika mfungamano zaidi na vikundi saidizi ili kufikia njia ya juu na takatifu ya kuhudumu.
Ninaamini kwamba mfuatano na muda wa matendo haya kwa miongo mingi unaweza kutusaidia kuona kazi moja iliyoungana na ya kina na si tu mfuatano pekee na wa mipango ya kipekee. Mungu amefunua mfumo wa uendelevu wa kiroho kwa watu binafsi na familia kupitia ibada, kufundisha, programu, na shughuli ambazo zinazolenga nyumbani na kusaidiwa na Kanisa. Muundo wa Kanisa na programu huwepo ili kubariki watu binafsi na familia na si kwa ajili ya muundo wa kanisa au progaramu zenyewe.”24
Ninaomba kwamba tutatambua kazi ya Bwana kama kazi moja kuu ya ulimwenguni kote ambayo inakuwa yenye kujilenga zaidi nyumbani na kusaidiwa na Kanisa. Ninajua na kushuhudia kwamba Bwana anafunua na atayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu.25
Ahadi na Ushuhuda
Nilianza ujumbe wangu kwa kuonyesha nguvu ambayo huja kutokana na nyuzi kusokotwa au kusukwa kwa pamoja kuwa kamba. Katika njia sawa na hiyo, ninaahidi kwamba kuongezeka kwa mtazamo, lengo, na nguvu vitadhihirika katika kujifunza kwetu na kuishi injili ya urejesho ya Yesu Kristo wakati tukijitahidi kuvijumlisha vitu vyote katika Kristo—hata ndani Yake.
Fursa na baraka zote za matokeo ya milele huanzia na, inawezekana na zina lengo kwa sababu ya, na kuvumilia kupitia Bwana Yesu Kristo. Kama Alma alivyoshuhudia: “Hakuna njia nyingine wala gharama ambayo kwayo binadamu anaweza kuokolewa, isipokuwa kupitia kwa Kristo. Tazama, yeye ni uzima na mwangaza wa ulimwengu.”26
Kwa shangwe ninatangaza ushuhuda wa utakatifu na kuishi kwa Baba wa Milele na Mwanawe mpendwa, Yesu Kristo Katika Mwokozi wetu, tunapata shangwe Na katika Yeye tunapata uhakika wa “amani katika ulimwengu huu, na uzima wa milele katika ulimwengu ujao.”27 Ninashuhudia hivyo katika jina takatifu la Bwana Yesu Kristo, amina.