2010–2019
Uongofu wa kina na wa kudumu kwa Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo
Oktoba 2018


Uongofu wa kina na wa kudumu kwa Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo

Lengo letu ni kuwekea usawa uzoefu wa Kanisani na nyumbani katika njia ambayo itaongeza imani, mambo ya roho, na kuongeza uongofu.

Kama Rais Russell M. Nelson alivyotangaza kwa uzuri na kwa ufasaha, viongozi wa Kanisa wamekuwa wakifanyia kazi kwa muda mrefu mpango “unaolenga‑nyumbani na unaosaidiwa na Kanisa wa kujifunza mafundisho, kuimarisha imani, na kukuza uwezo wa kuabudu kibinafsi. Rais Nelson kisha akatangaza mabadiliko ya kufikia “usawa mpya kati ya mafunzo ya injili nyumbani na Kanisani.”1

Kutimiza malengo haya—yaliyoelezwa na chini ya maelekezo ya Rais Russell M. Nelson na kufuatia uamuzi wa Baraza la Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili—ratiba ya mkutano wa jumapili itabadilishwa katika njia zifuatazo, kuanzia Januari 2019.

Ratiba ya Mikutano ya Jumapili.

Mikutano ya Kanisa ya Jumapili itakuwa ya dakika‑60 za mkutano wa sakramenti kila Jumapili, ikimlenga Mwokozi, ibada ya sakramenti, na jumbe za kiroho. Baada ya muda wa kwenda madarasani, waumini wa Kanisa watahudhuria darasa la dakika‑50 ambalo litakuwa na mbadilishano kila Jumapili.

  • Shule ya Jumapili itafanyika Jumapili ya kwanza na ya tatu.

  • Mikutano ya akidi za Ukuhani, Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, na wasichana itafanyika Jumapili ya pili na ya nne.

  • Mikutano ya Jumapili ya tano itakuwa chini ya maelekezo ya askofu.

Msingi itafanyika kila wiki wakati wa kipindi hiki cha dakika‑50 na itajumuisha kuimba na madarasa.

Picha
Ratiba ya Jumapili.

Kuhusu ratiba ya mkutano wa Jumapili, viongozi wa juu wa Kanisa wamekuwa na ufahamu kwa miaka mingi kwamba kwa baadhi ya waumini wetu wa thamani, ratiba ya Jumapili ya masaa‑matatu kanisani inaweza kuwa ngumu. Hii ni kweli hasa kwa wazazi wenye watoto wadogo, watoto wa msingi, waumini wazee, waongofu wapya, pamoja na wengine.2

Lakini kuna mengi zaidi kwenye badiliko hili zaidi tu ya kufupisha ratiba ya jumapili kwenye nyumba ya ibada. Rais Nelson ametambua kwa shukrani kiasi kikubwa kinachofanikishwa kama matokeo ya uaminifu wenu kwa mialiko iliyotangulia. Yeye, pamoja na uongozi wote wa Kanisa wanatamani kuleta shangwe kubwa ya injili—kwa wazazi, watoto, vijana, waseja, wazee, waongofu wapya, na wale watu wanaofundishwa na wamisionari—kupitia juhudi usawa inayolenga‑nyumbani, inayosaidiwa na‑Kanisa. Malengo na baraka zinazoambatana na rekebisho hili na mabadiliko mengine ya karibuni inajumuisha yafuatayo:

  • Kuongeza uongofu kwa Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo na kuimarisha imani katika Wao.

  • Kuimarisha watu binafsi na familia kupitia mtaala unaolenga‑nyumbani, unaosaidiwa na‑Kanisa ambao unachangia kuishi injili kwa furaha.

  • Kuheshimu siku ya Sabato, kwa kuzingatia ibada ya sakramenti.

  • Kuwasaidia watoto wote wa Baba wa Mbinguni katika pande zote za pazia kupitia kazi ya umisionari na kupokea ibada na maagano na baraka za hekaluni.

Kujifunza Injili Kunakosaidiwa na Kanisa, Kunakolenga Nyumbani

Ratiba hii ya Jumapili inatoa muda zaidi kwa jioni ya nyumbani na kujifunza injili nyumbani Jumapili, au hata wakati mwingine kama watu binafsi na familia wanavyoweza kuchagua. Shughuli ya usiku ya familia inaweza kufanyika Jumatatu au nyakati zingine. Kwa hitimisho hili, viongozi wanapaswa kuendelea kuacha huru jioni za Jumatatu kutoka kwenye mikutano na shughuli za Kanisa. Hata hivyo, muda unaotumika katika jioni ya nyumbani, kujifunza injili na shughuli za watu binafsi na familia zinaweza kupangwa kulingana na hali zao za kibinafsi.

Picha
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Kujifunza injili kibinafsi na kifamilia nyumbani kutakuwa kumeongezewa maana na mtaala unaolingana na [nyenzo] mpya ya Njoo, Unifuate Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ambayo inawiana na kile kinachofundishwa katika Shule ya Jumapili na Msingi.3 Mnamo Januari, madarasa ya Kanisa ya Shule ya Jumapili ya vijana na watu wazima na ya Msingi yatakuwa yakijifunza Agano Jipya. [Nyenzo] mpya ya kujifunza nyumbani ya Njoo, Unifuate kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia—pia ikijumuisha Agano Jipya—imekusudia kuwasaidia waumini kujifunza injili nyumbani. Inaelezea: “Nyenzo hii ni kwa ajili ya kila mtu binafsi na familia katika Kanisa. Imetengenezwa ili kutusaidia [vizuri zaidi] kujifunza injili—iwe peke [yetu] au na familia [zetu]. … Mihutasari katika nyenzo hii [mpya] imepangwa kulingana na ratiba ya … kila wiki.”4

Masomo mapya ya Msingi ya Njoo, Unifuate yanayofundishwa kanisani yatafuata ratiba inayofanana ya kila wiki. Madarasa ya Shule ya Jumapili ya watu wazima na vijana ya Jumapili ya kwanza na ya tatu yatawianishwa ili kwamba yaweze kuunga mkono nyenzo mpya ya nyumbani ya Njoo, Unifuate. Katika Jumapili ya pili na ya nne, watu wazima katika Ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wataendelea kujifunza mafundisho ya viongozi wa Kanisa, kwa msisitizo kwenye jumbe za sasa za manabii wa leo.5 Wasichana na wavulana wa Ukuhani wa Haruni watajifunza mada za injili katika Jumapili hizo.

Nyenzo mpya ya kujifunza nyumbani inatoa “Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.”6 Mihutasari kwa ajili ya kila wiki ina mawazo ya kujifunza yenye msaada na shughuli kwa ajili ya watu binafsi na familia. [Nyenzo] ya Njoo, Unifuate Kwa ajili ya watu binafsi na familia pia ina vielelezo vingi ambavyo vitasaidia kuongeza kujifunza kwa mtu binafsi na familia, hasa kwa watoto.7 Nyenzo hii mpya itatolewa kwa kila nyumba kufikia Disemba ya mwaka huu.

Rais Nelson, kutoka kwenye hotuba yake ya mwanzo kwa waumini wa Kanisa mnamo Januari, ametusihi kujiandaa kwa Ujio wa Pili wa Yesu Kristo kwa kutembea njia ya agano.8

Hali za ulimwenguni zinahitaji zaidi kuongeza uongofu binafsi kwa na kuimarisha imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo pamoja na Upatanisho Wake. Bwana ametuandaa sisi, mstari juu ya mstari, kwa nyakati hatari ambazo sasa tunazikabili. Katika miaka ya karibuni, Bwana ametuongoza kuzungumzia mambo ya muhimu yanayohusiana nazo ikijumuisha:

  • Kuiheshimu siku ya Sabato na ibada takatifu ya sakramenti ambavyo tena vimesisitizwa kwa miaka mitatu iliyopita.

  • Chini ya maelekezo ya askofu, akidi za wazee zilizoimarishwa na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama zimezingatia lengo na majukumu matakatifu yaliyoteuliwa ya Kanisa9 na kuwasaidia waumini kufanya na kutunza maagano matakatifu.

  • Kuhudumu katika “njia ya juu na takatifu zaidi” kumekubaliwa kwa furaha.

  • Kuanza na mwisho akilini, maagano ya hekaluni na historia ya familia vinakuwa sehemu yenye maana ya njia ya agano.

Marekebisho yaliyotangazwa asubuhi ya leo bado ni mfano mwingine wa mwongozo kwa changamoto za siku yetu.

Mtaala wa mafundisho ya Kanisa umesisitiza uzoefu wa Kanisani Jumapili. Tunajua kwamba tunapokuwa na mafundisho mazuri zaidi na washiriki wa darasa waliojiandaa zaidi kiroho, tunakuwa na uzoefu mzuri zaidi kanisani Jumapili. Tunabarikiwa kwamba daima Roho atazidisha na kuimarisha uongofu katika mazingira ya Kanisa.

Mtaala mpya unaolenga‑nyumbani na unaosaidiwa na‑Kanisa unapaswa kushawishi kwa nguvu zaidi utiifu wa kidini na tabia za familia na utiifu wa kidini na tabia za mtu binafsi. Tunajua athari ya kiroho na uongofu wa kina na wa kudumu unaoweza kupatikana katika mazingira ya nyumbani. Miaka iliyopita, utafiti ulishuhudia kwamba kwa wasichana na wavulana ushawishi wa Roho Mtakatifu mara nyingi hufuatana na usomaji binafsi wa maandiko na sala nyumbani. Lengo letu ni kuwekea usawa uzoefu wa nyumbani na Kanisani katika njia ambayo itaongeza imani, na mambo ya roho, na kuongeza uongofu kwa Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo.

Katika sehemu ya unaolenga‑nyumbani, unaosaidiwa na‑kanisa ya rekebisho hili, kuna uwezekano wa kubadilisha kwa kila mtu binafsi na familia kuamua kwa sala jinsi gani na lini utatekelezwa. Kwa mfano, kiasi kikubwa litabariki familia zote, kutegemeana na mahitaji husika, litakuwa la kufaa kabisa kwa vijana waseja, watu wazima waseja, wazazi wasio na wenza wao, familia ambazo baadhi tu ni waumini, waumini wapya,10 pamoja na wengine kukusanyika katika makundi nje ya ibada ya kawaida ya kuabudu Jumapili kufurahia ushirikiano wa injili na kuimarishwa kwa kujifunza pamoja nyenzo inayolenga‑nyumbani, inayosaidiwa na‑Kanisa. Hili lingefanikishwa nje ya utaratibu na wale ambao wanatamani kufanya hivyo.

Katika sehemu nyingi za ulimwengu, watu huchagua kubaki kwenye nyumba ya ibada baada ya ratiba ya kawaida ya Jumapili kufurahia mahusiano ya kijamii. Hakuna chochote katika badiliko hili lililotangazwa ambacho kitaingilia utamaduni huu wa kupendeza na wa thamani katika namna yoyote.

Kuwasaidia waumini kujiandaa kwa ajili ya Sabato, baadhi ya kata tayari zinatuma barua pepe yenye taarifa, arafa, au ujumbe wa mitandao ya kijamii katikati ya wiki. Katika mtazamo wa badiliko hili, kwa nguvu tunapendekeza aina hii ya mawasiliano. Mialiko itawakumbusha waumini juu ya ratiba ya mkutano wa Jumapili kwa wiki ile, ikijumuisha mada ya somo la darasa lijalo, na kuunga mkono muendelezo wa mazungumzo ya injili nyumbani. Kwa kuongezea, mkutano wa watu wazima wa Jumapili pia utatoa taarifa za kuunganisha kujifunza Kanisani na nyumbani kila wiki.

Mkutano wa sakramenti na muda wa darasa vitahitaji kufikiriwa kwa sala kuhakikisha kwamba vipaumbele vya kiroho vinasisitizwa kuliko shughuli za utawala. Kwa mfano, matangazo yanaweza kwa kiasi kikubwa kutolewa katika mwaliko wa katikati ya wiki au kwenye programu iliyochapishwa. Wakati mkutano wa sakramenti unapaswa kuwa na sala ya kufungua na kufunga, mkutano wa pili unahitaji kuwa tu na sala ya kufunga.11

Kama ilivyotajwa mwanzo, ratiba mpya ya Jumapili haitaanza mpaka Januari 2019. Kuna sababu kadhaa kwenye hili. Mbili za muhimu zaidi ni, kwanza, kuwa na muda wa kusambaza [nyenzo] ya Njoo, Unifuate Kwa ajili ya watu binafsi na familia na, pili, kutoa muda kwa marais wa vigingi na maaskofu kupanga ratiba za mikutano kwa lengo la kuwa na kata zaidi kukutana mapema katika siku.

Viongozi walipotafuta ufunuo, mwongozo uliopatikana kwa miaka michache iliyopita ni kuimarisha mkutano wa sakramenti, kuheshimu siku ya Sabato, na kuwahimiza na kuwasaidia wazazi na watu binafsi kuzifanya nyumba zao chanzo cha nguvu ya kiroho na ongezeko la imani—mahala pa shangwe na furaha.

Baraka za Ajabu Sana

Ni nini marekebisho haya yamaanisha kwa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho? Tuna ujasiri kwamba waumini watabarikiwa katika njia za kipekee. Jumapili inaweza kuwa siku ya kujifunza injili na kufundisha kanisani na nyumbani. Pale watu binafsi na familia wanaposhiriki katika mabaraza ya familia, historia ya familia, kuhudumu, kutumikia, ibada binafsi, na wakati wa shangwe wa familia, siku ya Sabato hakika itakuwa ya kupendeza sana.

Picha
Familia ya Carvalho

Familia moja kutoka Brazil ni washiriki wa kigingi ambacho nyenzo mpya ya nyumbani ya Njoo, Unifuate ilifanyiwa majaribio. Baba, Fernando, mmisionari aliyerudi, ambaye pamoja na mke wake, Nancy, ni wazazi wa watoto wadogo wanne, aliripoti: “Wakati programu ya Njoo, Unifuate ilipotambulishwa kwenye kigingi chetu, nilikuwa na furaha sana, na niliwaza ‘jinsi tunavyojifunza maandiko nyumbani kutabadilika.’ Ilitokea kweli nyumbani kwangu, na kama kiongozi wa Kanisa niliona kwamba ilitokea kwenye nyumba zingine. … Ilitusaidia hasa kujadili maandiko nyumbani kwetu. Mke wangu na mimi tulikuwa na uelewa wa kina kuhusu mada tuliyojifunza. … Ilitusaidia … kuongeza uelewa wetu wa injili, na kuongeza imani na ushuhuda wetu. … Ninatoa ushuhuda wangu … kwamba ninajua ilikuwa imefunuliwa na Bwana ili kwamba masomo endelevu na yenye ufanisi wa kanuni na mafundisho yaliyomo katika maandiko hulete imani zaidi, ushuhuda, na nuru kwenye familia … katika dunia inayozidi kuanguka.”12

Katika majaribio ya vigingi pande zote ulimwenguni, kulikuwa na majibu yenye kufaa kwenye nyenzo mpya ya nyumbani ya Njoo, Unifuate. Wengi walitoa taarifa kwamba walikua kutoka kwenye kusoma maandiko kwenda kwenye kujifunza kweli maandiko. Ilikuwa pia hisia ya wote uzoefu ulikuwa wa kukuza imani na ulikuwa na matokeo ya kupendeza kwa kata.13

Uongofu wa Kina na wa Kudumu

Lengo la mabadiliko haya ni kupata uongofu wa kina na wa kudumu wa watu wazima na kizazi kinachochipukia. Ukurasa wa kwanza wa nyenzo ya mtu binafsi na familia inaeleza: “Lengo la vyote kujifunza na kufundisha injili ni kuongeza uongofu wetu na kutusaidia kuwa zaidi kama Yesu Kristo. … Hii inamaanisha kumtegemea Kristo ili abadili mioyo yetu.”14 Hii inasaidiwa na kufika “zaidi ya darasani mpaka kwenye moyo na nyumba ya mtu binafsi. Inahitaji uthabiti, juhudi za kila siku kuelewa na kuishi injili. Uongofu wa kweli unahitaji ushawishi wa Roho Mtakatifu.”15

Lengo muhimu zaidi na baraka ya juu ya uongofu wa kina na wa kudumu ni kupokea kwa kustahili maagano na ibada za njia ya agano.16

Tunawaamini ninyi kushauriana pamoja na kutafuta ufunuo kwa ajili ya kutekeleza mabadiliko haya—wakati mkitazama si zaidi ya alama au kujaribu kushurutisha watu binafsi na familia. Taarifa zaidi zitatolewa kwenye mawasiliano yajayo, ikijumuisha barua ya Barua ya Urais wa Kwanza na kiambato.

Ninashuhudia kwenu kwamba katika mashauriano ya Baraza la Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ndani ya hekalu, na baada ya nabii wetu mpendwa kumwomba Bwana kwa ajili ya ufunuo wa kusonga mbele na mabadiliko haya, uthibitisho wenye nguvu ulipokelewa na wote. Russell M. Nelson ni Rais wetu na nabii anayeishi. Matangazo yaliyotolewa leo yataleta matokeo ya baraka kuu kwa wale ambao kwa shauku wanapokea marekebisho haya na kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu. Tutakuwa karibu na Baba yetu wa Mbinguni pamoja na Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, ambaye Kwake mimi ni shahidi wa hakika. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, “Maneno ya Ufunguzi,” Liahona, Mei 2018, 8.

  2. Sote pia tunafahamu kwamba, katika jamii kwa ujumla, ukubwa wa matukio mengi kwa ajili ya taarifa, elimu, na hata burudani umekuwa ukipunguzwa maana.

  3. Mtaala huu utapatikana kidijitali na kwenye machapisho.

  4. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia(2019), vi.

  5. Ona “Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama,”Liahona, Mei 2018, 140. Badala ya Jumapili ya pili na ya tatu; jumbe za mikutano mkuu zitajadiliwa katika Jumapili ya pili na ya nne.

  6. OnaNjoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, 4. Watu binafsi na familia huamua ni kipengele gani cha kujifunza injili nyumbani, jioni ya nyumbani, na shughuli za familia zitakuwa jioni ya familia nyumbani (ambayo wengi tayari wanaita jioni ya nyumbani”). Kwa sababu watu binafsi na familia watafanya uamuzi huu, jioni ya nyumbani na jioni ya familia nyumbani zimekuwa zikitumiwa kwa kubadilishana katika mabadiliko ambayo yametangazwa.

  7. Ona Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, 29.

  8. Ona Russell M. Nelson, “Tunaposonga Mbele Pamoja,” Liahona, Apr. 2018, 7.

  9. Ona Handbook 2: Administering the Church (2010), 2.2. Majukumu matakatifu yaliyopangwa “hujumuisha kuwasaidia waumini kuishi injili Yesu Kristo, kukusanya Israeli kupitia kwa kazi ya umisionari, kuwajali maskini na wenye shida, na kuwezesha wokovu wa wafu kwa kujenga mahekalu na kufanya ibada za niaba.” Ona pia Mafundisho na Maagano 110, ambayo ina maelezo ya urejesho wa funguo muhimu.

  10. Weka umakini hasa kwa wale watoto ambao wazazi wao siyo waumini au hawahudhurii kanisani kila mara. Waseja wanaweza pia kukutana na familia kama hilo litakuwa na manufaa kwa wote wanaohusika.

  11. Mazoezi ya ufunguzi kwa kawaida hayatakuwa sehemu ya mkutano wa pili.

  12. Familia ya Fernando and Nancy de Carvalho, Brazil.

  13. Watu binafsi na familia walioshiriki kwenye majaribio kwa wastani walijifunza injili mara nyingi na walikuwa na ujifunzaji wa maandiko wenye maana zaidi na mijadala ya injili nyumbani. Waliripoti kuwa na mijadala zaidi ya injili isiyo rasmi pamoja na familia na waumini wa kata na kushukuru kujifunza sehemu sawa ya maandiko kama familia zao. Hili lilikuwa kweli hasa kwa vijana.

  14. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, v; ona pia 2 Wakorintho 5:17.

  15. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, v.

  16. Russell M. Nelson, “Tunaposonga Mbele Pamoja,” 7.

Chapisha