2010–2019
Mwako Wetu wa Kambi wa Imani
Oktoba 2018


Mwako Wetu wa Kambi wa Imani

Kwa wale wanaotafuta, wanaokubali, wanaoishi kwa ajili yake, alfajiri ya imani wakati mwingine pole pole, itakuja au kurejea.

Akina kaka na dada, je, si ni vyema kupokea ufunuo kutoka mbinguni kupitia kwa Rais Russel M. Nelson na viongozi wetu wa Kanisa kwa njia mpya na takatifu zaidi,1 nyumbani na kanisani, kwa mioyo yetu, akili zetu na nguvu zetu zote?

Umewahi kuwa na nafasi kufanya kitu ulichohisi kuwa hukuwa tayari au kutokiweza lakini ulibarikiwa kwa kujaribu?

Mimi pia. Hapa kuna mfano.

Miaka kadha iliyopita Mzee Richard G. Scott, mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alinialika kwa upole, “Gerrit ungependa kuchora picha nami?

Mzee Scott alisema kuchora kulimsaidia kutazama na kubuni. Ameandika: “Jaribu kuwa mbunifu, hata kama matokeo ni ya wastani. … Ubunifu unaweza kukuza moyo wa shukrani kwa ajili ya maisha na kwa kile ambacho Bwana ametengeneza kuwa asili yako. … Ukichagua vyema, haitachukua muda mrefu.”2

Rais Henry B. Eyring anaeleza kuhusu tafakari zake za kisanaa zikichochewa na “hisia ya upendo,” pamoja na upendo wa Muumba anayetarajia watoto Wake kuwa kama Alivyo Yeye—kubuni na kujenga.”3 Kazi za kisanaa za Rais Eyring zinatoa “mtazamo wa kipekee wa kiroho katika ushuhuda na imani.”4

Kazi ya kisanaa yaa Boyd K. Packer inadhihirisha ujumbe wa kimsingi wa injili: “Mungu ni Muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo ndani yake na asili yote inashuhudia hivyo maumbile na kwamba kuna uwiano mkamilifu kati ya asili, sayansi na ujumbe wa Yesu Kristo.”5

Alma alishuhudia, “vyote vinaonyesha kwamba kuna Mungu.”6 Watoto wetu wa Msingi huimba “ninaposikia wimbo wa ndege au kutazama anga ya bluu, anga ya bluu … ninafurahi kuwa ninaishi katika ulimwengu huu maridadi Baba wa Mbinguni aliuumba kwa ajili yangu”7 Mwandishi Victor Hugo anasherehekea “mahusiano ya kimiujiza baina ya watu na vitu katika ukamilifu huu usio na mwisho kutoka kwa jua hadi kwa mdudu mdogo. … Ndege wote wanaopaa wanashikilia uzi wa umilele katika kucha zao. … Wingu la jekunduni kichuguu cha nyota.”8

Na hiyo huturejesha kwenye mwaliko wa Mzee Scott.

“Mzee Scott,” nilijibu, “Ningependa kuwa mbunifu na mwenye kuchunguza zaidi. Ninasisimka kufikiria Baba wa Mbinguni hupaka rangi kwa mawingu mazito na kila rangi ya mbingu na maji. “Lakini”—hapa kulikuwa na kimya kirefu— “Mzee Scott,” Nilisema, “Sina ujuzi wowote wa kuchora. Ninawasiwasi inaweza kukuvunja moyo kujaribu kunifundisha.”

Mzee Scott akatabasamu na kupanga ili tukutane. Kwenye siku iliyochaguliwa, alitayarisha karatasi, rangi na brashi Alichora sehemu za nje na kunisaidia kuniwekea unyevu kwenya karatasi.

Picha
Kambi Moto Wakati wa Machweo

Tulitumia kama mfano mchoro wake maridadi ulioitwa Mwako wa moto Wakati wa Machweo. Wakati tukichora, tulizingumzia kuhusu imani—jinsi tunavopata mwanga na joto la mwako wa moto, tunaacha giza na shaka nyuma yetu—jinsi gani wakati mwingine usiku mrefu, wenye upweke, mwako wetu wa imani unaweza kutupa matumaini na hakikisho. Na alfariji huja. Mwako wetu wa imani— kumbukumbu zetu, uzoefu, na urithi wa imani kwa wema wa Mungu na rehema ororo maishani mwetu—vimetuimarisha usiku kucha.

Ushuhuda wangu ni—kwa wale wanaotafuta, wanaokubali, wanaoishi kwa ajili yake—alfajiri ya imani, wakati mwingine pole pole, itakuja au inaweza kurejea. Mwanga utakuja tunapotamani na kuutafuta, tukiwa na subira na watiifu kwa amri za Mungu, tunapokuwa wawazi kwa neema ya Mungu, uponyaji, na maagano.

Tulipoanza kuchora, Mzee Scott alihimiza, “Gerrit, hata kwa somo moja utachora kitu utakachotaka kuweka na kukumbuka.” Mzee Scott alikuwa sahihi. Ninathamini mchoro rangi za maji wa mwako wa moto moto ambao Mzee Scott alinisaidia kuchora. Uwezo wangu wa kisanaa ulikuwa, na umebaki kuwa wenye mipaka, lakini kumbukumbu ya mwako wetu wa imani inaweza kututia moyo kwa njia tano.

Kwanza, mwako wetu wa imani unaweza kututia moyo kupata shangwe katika ubunifu.

Kuna shangwe katika kufikiri, kujifunza na kufanya mambo mapya ya thamani. Hii hasa ni kweli tunapokita kwa kina imani na kuamini katika Baba wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo. Hatuwezi kujipenda wenyewe vya kutosha kujiokoa wenyewe. Lakini Baba wa Mbinguni anatupenda zaidi na hutujua kuliko jinsi tunavyojijua. Tunaweza kumwamini Bwana na kutotegemea ufahamu wetu wenyewe.9

Umewahi kuwa pekee ambaye hujaalikwa kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mtu fulani ?

Umewahi kuchaguliwa wa mwisho, au kutochaguliwa, wakati timu zinapochaguliwa?

Umewahi kujitayarisha kwa ajili ya mtihani, mahojiano ya kazi, fursa uliyotaka sana—na ukahisi kuwa umeshindwa?

Umewahi kusali kwa ajili ya uhusiano ambao, kwa sababu zozote zile, hakuweza kuendelea?

Umewahi kukabiliwa na ugaonjwa wa muda mrefu, kuachwa na mwenzi, kuteseka kwa ajili ya familia?

Mwokozi wetu anafahamu hali zetu. Tunapotumia uhuru wa kuchagua tuliopewa na Mungu na kuhusisha uwezo wetu wote kwa unyenyekkevu na imani, Mwokozi wetu, Yesu Kristo, anaweza kutusaidia kukabiliana na changamoto za kimaisha na shangwe. Imani hujumuisha hamu na uchaguzi wa kuamini. Imani pia huja kwa kutii amri za Mungu, tulizopewa kutubariki, wakati tukifuata njia Yake ya agano.

Wakati tumehisi au wanaohisi shaka, upweke, kuudhiwa, kukasirishwa, kuvunjwa moyo, kukatishwa tamaa, au kutengwa kutoka kwa Mungu na Kanisa Lake lililorejeshwa, inaweza kuchukua juhudi za ziada na imani kuingia tena katika njia yake na ahadi. Lakini inafaa! Tafadhali njoo, au njoo tena kwake, kwa Bwana Yesu Kristo! Upendo wa Mungu ni imara zaidi kuliko kamba za mauti—ya kimwili au kiroho.10 Upatanisho wa Mwokozi wetu hauna mwisho na ni wa milele. Kila mmoja wetu hupotoka na kupungukiwa. Tunaweza, kwa muda, kupotea njia. Mungu kwa upendo anatuhakikishia kwamba, licha ya pale tulipo au kile tulichokifanya, hakuna mahali hatuwezi kurudi. Anasubiri, tayari kutukumbatia.11

Pili, mwako wetu wa imani unaweza kututia moyo kuhudumu upya, katika ubunifu wa kiroho, na katika njia takatifu za Kiroho zaidi.

Uhudumiaji kama huo, huleta miujiza na baraka za Agano—ambapo tunahisi upendo wa Mungu na kutafuta kuwahudumia wengine kwa roho hiyo.

Sio muda mrefu, Dada Gong pamoja nami tulipata kumjua baba na familia iliyobarikiwa na kaka mwaminifu wa ukuhani ambaye alikwenda kwa askofu wao na kuuliza kama yeye (yule kaka wa ukuhani) angeweza kuwa mwenzi wa baba yake kuwa walimu wa nyumbani. Baba hakuwa akishiriki kikamilifu na hakuwa anapendelea ufundushaji wa nyumbani. Lakini wakati moyo wa baba ulipobadilika, yeye na yule kaka mpendwa wa ukuhani walianza kuzitembelea familia “zao’ Baada ya mojawapo ya matembezi hayo mke wake—akiwa hahudhurii kanisa—akamuuliza mumewe jinsi mambo yalivyoenda. Baba alikubali, “Ninaweza kuwa nimehisi kitu fulani”—kisha akaenda jikoni kuchukua bia.12

Lakini kitu kimoja kikafuata kingine, uzoefu ororo, huduma, mioyo kubadilika, darasa la matayarisho ya hekaluni, kuja kanisani, kufunganishwa na familia katika hekalu takatifu. Fikiria ni jinsi gani shukrani walio nayo watoto na wajukuu kwa baba na mama na kwa yule mhudumu mwenza aliyekuja kama rafiki na mwenza kushirikiana na baba yao kuwahudumia na kuwapenda wengine.

Mhimizo wa tatu wa mwako wa imani: shangwe ya injili na baraka huja tunapotafuta kumpenda Bwana na wengine kwa mioyo na nafsi zetu zote.

Maandiko yanatualika kuweka jinsi tulivyo na tunavyokuwa juu ya madhabahu ya upendo na huduma. Katika Agano la Kale, Kumbukumbu la Torati inatuhimiza “kumpenda Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, roho, na nguvu.13 Yoshua anahimiza “mpenda Bwana, Mungu wenu, … na kwenenda katika njia zake zote, … na kuzishika amri zake, … na kushikamana na yeye, na … kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.”14

Kwenye agano jipya, Mwokozi anatangaza amri mbili zilizo kuu: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, … na Mpende jirani yako kama nafsi yako.”15

Katika Kitabu cha Mormoni: Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo mfalme Benyamini, alitumikia “kwa nguvu zote za mwili wake na uwezo wa nafsi yake yote” na aliimarisha tena amani katika nchi ile.16 Katika Maagano na Mafundhso, kila mmisionari anajua, Bwana ametuamuru kumtumikia kwa “Moyo wetu wote, uwezo, akili na nguvu.”17 Watakatifu walipoingia Jackson County, Bwana aliwaamuru kuishika sabato kuwa takatifu kwa kumpenda “Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa uwezo wako wote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote; na katika jina la Yesu Kristo utamtumikia yeye.”18

Tunafarahia kwa mwaliko kujitolea nafsi zetu kutafuta njia ya juu na takatifu zaidi za kumpenda Mungu na kuwapenda wale wanaotuzunguka na kuimarisha imani yetu katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo mioyoni mwetu na nyumbani kwetu na kanisani.

Nne, mwako wetu wa imani hutuimiza kujenga mitindo ya kawaida ya kuishi kwa utakatifu inayoweka kina imani na hali ya kiroho

Tabia hizi takatifu, mazoea matakatifu, au mitindo ya kimaombi inaweza kujumuisha sala; kusoma maandiko; kufunga, kumkumbuka Mwokozi wetu kupitia maagano ya sakramenti, kushiriki baraka za injili kupitia kwa wamisionari, historia ya familia na kazi za hekaluni na huduma zingine; kuandika shajara, na kadhalika.

Wakati mazoea matakatifu na hamu za kiroho zijumuikapo, wakati na umilele huja pamoja. Mwanga wa kiroho na uzima huja wakati kanuni za kidini hutuleta karibu na Baba Yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Wakati tunapompenda roho na kutii amri, vitu vya umilele vinaweza kutatonatona juu ya roho zetu kama umande utokao mbinguni.19 Kwa utiifu wa kila siku, na kwa maji yenye uhai tunapata majibu, imani, na nguvu kukabiliana na changamoto za kila siku na fursa kwa subira ya injili, mtazamo na shangwe

Tano, tunapendelea katika mazoea mema zaidi wakati ukitafuta njia mpya na takatifu zaidi za kumpenda Mungu na kutusaidia sisi na wengine kujiandaa kukutana na Yeye, mwako wetu wa imani unaweza kututia moyo kukumbuka ukamilifu katika Kristo na si katika sisi au katika ukamilifu wa kiulimwengu.

Mialiko ya Mungu imejaa upendo na uwezekano kwa sababu Yesu Kristo ni “njia kweli na uzima”20 Kwa wale wanaohisi kuwa na mizigo, Anawaalika “Njooni kwangu,” na kwa wale wanaokuja Kwake Anaahidi “Nitawapumzisha”21 “Mje kwa Kristo, na mkamilishwe ndani yake, … mpendeni Mungu na mioyo yenu, akili na nguvu zenu zote, basi neema yake inawatosha, kwamba kwa neema yake mngekamilishwa katika Kristo.”22

Kwa hakikisho hili “ kwa neema yake mkamilike katika Kristo” pia ni faraja, amani na ahadi tunaweza kendelea mbele kwa imani na hakika kwa Bwana hata wakati mambo hayaendi tunavyotumaini, kutarajia, au hata kutakiwa, kupitia kwa kosa lisilo letu, hata baada ya sisi kufanya vyema kwa uwezo wetu wote.

Kwa wakati na njia tofauti, sote tunahisi kupungukiwa, kutokuwa na hakika, na pengine kutostahili. Hata hivyo katika juhudi zetu za kumpenda Mungu na kumhudumia jirani yetu, tunaweza kuhisi Upendo wa Mungu na mwongozo wa kiungu unaohitajika kwa ajili ya maisha yetu na yao kwa njia mpya na takatifu zaidi.

Kwa huruma, Mwokozi wetu anatutia moyo na kuahidi kuwa tunaweza “kusonga mbele tukiwa na imani imara katika Kristo, tukiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote.23 Mafundisho ya Kristo, Upatanisho wa Mwokozi wetu, na kufuata kwetu kwa moyo wote njia yake ya agano kunaweza kutusaidia kufahamu kweli na kutufanya kuwa huru.24

Ninashuhudia kuwa ukimilifu wa injili Yake na Mpango wake wa furaha vimerejeshwa na kufundishwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kwenye maandiko matakatifu, na kupitia manabii kutoka kwa Joseph Smith hadi kwa Russell M. Nelson hivi leo. Ninashuhudia njia yake ya agano huongoza kwenye zawadi kuu anayoahidi Baba yetu mpendwa wa Mbinguni: “Mtapata uzima wa milele.”25

Na baraka zake na shangwe ya kudumu ziwe zetu tuitiapo joto mioyo yetu na uwajibikaji wetu katika mwako wetu wa imani, ninasali katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo. Amina.

Chapisha