2010–2019
Kutorithika kwa Kiungu
Oktoba 2018


11:58

Kutoridhika kwa Kiungu

Kutoridhika kwa kiungu kunaweza kutufanya tutende kwa imani, kufuata mialiko ya mwokozi kutenda mema, na kutoa maisha yetu Kwake kwa unyenyekevu.

Nilipokuwa katika shule ya msingi, tulitembea kwenda nyumbani kupitia kwenye mkondo uliotiwa lami ambao ulizunguka mlima. Kulikuwa na mkondo mwingine, usiotiwa lami, ulioitwa “mkondo wa wavulana” Njia ya mkondo wa wavulana ilikuwa njia ya mchanga iliyokwenda moja kwa moja juu ya mlima. Ilikuwa fupi sana lakini yenye mteremko mkali. Kama msichana mdogo, nilijua kuwa ningetembea kwenye mkondo wowote ambao wavulana wangetembea. Muhimu zaidi, nilijua niliishi katika siku za mwisho na kwamba ningehitaji kufanya mambo magumu, kama waanzilishi—na nilitaka kuwa tayari. Hivyo mara kwa mara, ningebaki nyuma ya kikundi cha rafiki zangu kwenye njia iliyotengenezwa, na kuvua viatu na kutembea bila viatu kwenye mkondo wa wavulana Nilikuwa najaribu kuikomaza miguu yangu.

Kama msichana mdogo wa Msingi, hilo ndilo nilidhani ningeweza kufanya ili kujitayarisha. Sasa ninajua tofauti! Badala ya kutembea bila viatu kwenye njia za juu mlimani, ninajua ninaweza kutayarisha miguu yangu kutembea kwenye njia ya agano kwa kuitikia mialiko ya Roho Mtakatifu. Kwani Bwana, kupitia nabii Wake, anatuita kila mmoja wetu kuishi na kujali katika njia “ya juu na takatifu” na “kuchukua hatua ya juu.”1

Miito hii ya kinabii ili kutenda, pamoja na hisia yetu ya asili kwamba tunaweza kufanya zaidi na kuwa zaidi, wakati mwingine huunda ndani yetu kile ambacho Mzee Neal A. Maxwell alikiita “kutoridhika kwa kiungu.”2 Kutoridhika kwa Kiungu hutokea wakati tunapojifananisha “kile tulicho sasa, na kile tulicho na nguvu za kuwa.”3 Kila mmoja wetu, tukiwa wakweli, huhisi mwanya kati ya pale tulipo na kile tulicho, na pale na kile tunachotaka kuwa. Tunakuwa na hamu ya uwezo mkubwa wa kibinafsi. Tuna hisia hizi kwa sababu sisi ni mabinti na wana wa Mungu, tuliozaliwa na Nuru ya Kristo na hali tukiishi kwenye ulimwengu ulioanguka. Hisia hizi tumepewa na Mungu na zinaleta umuhimu wa kutenda.

Tunapaswa kukaribisha hisia za kutoridhika kwa kiungu zinazotuita kwenye njia ya juu, huku tukitambua na kuepuka ulaghai wa Shetani—wa kukatisha tamaa na kufadhaisha. Hii ni sehemu ya thamani ambapo shetani ana hamu kubwa kurukia. Tunaweza kuchagua njia iliyo juu inayotuongoza kwenye kumtafuta Mungu na amani Yake na neema, au tunaweza kumsikiliza Shetani anayetushambulia na jumbe kwamba kamwe hatutatosha: matajiri vya kutosha, werevu vya kutosha, warembo vya kutosha, chochote cha kutosha. Kutoridhika kwetu kunaweza kuwa kwa kiungu—au kwa kuangamiza.

Tenda kwa Imani

Njia moja ya kutambua kutoridhika kwa kiungu kutokana na ulaghai wa Shetani ni kwamba kutoridhika kwa kiungu kutatuongoza kwenye tendo la uaminifu. Kutoridhika kwa kiungu si mwaliko wa kukaa kwenye hali ya kuridhika, wala hakutatuongoza kwenye kukata tamaa. Nimejifunza kwamba ninapogaagaa kwenye mawazo ya kila kitu ambacho mimi sicho, siendelei, na ninapata ugumu zaidi kuhisi na kumfuata Roho.4

Kama kijana mdogo, Joseph Smith alipata ufahamu makini wa mapungufu yake na akawa na wasiwasi kuhusu “wema wa nafsi [yake] isiyokufa.” Kwa maneno yake, “akili yangu ilidhikishwa, kwani nilisadikishwa kuhusu dhambi zangu, na … nikahisi kuhuzunika kwa ajili ya dhambi zangu na dhambi za ulimwengu.”5 Hii ilimwongoza kwenye “tafakari na wasiwasi mkubwa”6 Haya yanasikika kama ya kawaida? Una wasi wasi au kudhikishwa na mapungufu yako?

Basi, Joseph alifanya jambo. Alishiriki, “daima nilijisemea mimi mwenyewe: Ni nini cha kufanya?”7 Joseph alitenda kwa imani. Aligeukia maandiko, akasoma mwaliko katika Yakobo 1:5, na akamgeukia Mungu kwa usaidizi. Ono lililofuata lilianzisha Urejesho. Nina shukrani jinsi gani kuwa kutoridhika kwa kiungu kwa Joseph, kipindi chake cha wasiwasi na kuchanganyikiwa, vilimchochea kwenye tendo la imani.

Fuata Ushawishi wa Kutenda Mema

Ulimwengu mara nyingi hutumia hisia ya kutoridhikia kwa kiungu kama sababu ya utekaji‑binafsi, kwa kugeuza mawazo yetu ndani na nyuma na kujikita kibinafsi kwenye mimi ni nani, kile nisicho na kile nitakacho. Kutoridhika kwa kiungu hutuhamasisha kufuata mfano wa Mwokozi, ambaye “alizunguka akitenda kazi njema”.8 Tunapotembea kwenye njia ya ufuasi, tutapokea misukumo ya kiroho kuwafikia wengine.

Hadithi niliyosikia miaka iliyopita imenisaidia kutambua na kisha kutenda kulingana na ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu. Dada Bonnie Parkin, Rais mkuu wa zamani wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alishiriki yafuatayo:

“Susan … alikuwa mshonaji hodari. Rais Kimball aliishi katika kata yake [Susan]. Jumapili moja, Susan aliona kuwa alikuwa na suti mpya. Baba wa Susan alikuwa karibuni … amemnunulia kitambaa kizuri cha hariri. Susan aliona kuwa kitambaa kile kingetengenezwa tai nzuri kuendana na suti mpya ya Rais Kimball. Kwa hivyo, Jumatatu akatengeneza tai. Aliifunga kwenye karatasi ya shashi na kwenda juu ya jengo kwenye nyumba ya Rais Kimball.

“Njiani kuelekea mlango wa mblele, ghafla alisimama na kujiuliza, ‘Mimi ni nani kumtengenezea nabii tai? Pengine anazo nyingi.’ Akiamua kuwa alikuwa amefanya makosa, aligeuka kuondoka.

Hapo ndiyo Dada Kimball “alipofungua mlango wa mbele na kusema “Ee, Susan!”

Akibabaika huku na huko, Susan alisema, ‘Nilimwona Rais Kimball akiwa na suti mpya Jumapili. Baba alininunulia hariri kutoka new york … kwa hivyo nikamtengenezea tai.’

“Kabla ya Susan kuendelea, Dada Kimball alimsitisha, akashika mabega yake, na kusama: “Susan, kamwe usididimishe wazo karimu”9

Ninayapenda hayo! “Kamwe usididimize wazo karimu.” Wakati mwingine ninapopata wazo kufanya kitu kwa ajili ya mtu, ninajiuliza kama huo ulikuwa uvuvio au mawazo yangu tu. Lakini ninakumbushwa, “Kile kilicho cha Mungu hukaribisha na hushawishi kufanya mema siku zote; kwa hivyo, kila kitu kinachokaribisha na kushawishi kufanya mema, na kumpenda Mungu, na kumtumikia, kinaongozwa na Mungu.”10

Bila kujali ni uvuvio wa moja kwa moja au hamu ya kusaidia, tendo jema kamwe si hasara; kwani “hisani haikosi kufaulu kamwe”11—na kamwe si mwitikio hasi.

Mara nyingi wakati si wa kufaa, na kwa nadra tunafahamu athari ya matendo yetu madogo ya huduma. Lakini mara moja moja, tutatambua kuwa tumekuwa vifaa kwenye mikono ya Mungu na tutakuwa wenye shukrani kujua kwamba Roho Mtakatifu anayefanya kazi kupitia sisi ni onyesho la ukubali wa Mungu.

Akina dada, mimi na ninyi tunaweza kuomba Roho Mtakatifu kutuonyesha “Vitu vyote tunavyostahili kutenda,”12 hata kama ratiba yetu ya vitu vya kufanya inaonekana kujaa. Tunapovuviwa, tunaweza kuacha vyombo kwenye sinki au sanduku lililojaa changamoto zinazohitaji umakini wetu ili kumsomea mtoto, kutembelea rafiki, kulea watoto wa jirani, au kuhudumu hekaluni. Msinielewa vibaya—mimi ni mtengeneza orodha, ninapenda kukamilisha mambo. Lakini amani huja kwa kujua kwamba kuwa zaidi si lazima kuwe sawa na kufanya zaidi. Kujibu kutoridhika kwa kuamua kufuata uvuvio hubadilisha jinsi ninavyofikiria kuhusu “muda wangu,” na ninawaona watu, si kama usumbufu, bali kama lengo la maisha yangu.

Kutoridhika kwa Kiungu Hutuelekeza kwa Kristo

Kutoridhika kwa Kiungu huongoza kwenye unyenyekevu, si kwenye kujihurumia wala kuvunjika moyo kunakokuja kutokana na ulinganishi ambapo kila mara sisi hupungukiwa. Wanawake wanaoweka maagano huja kwa kila umbo na ukubwa, familia zao, uzoefu wa maisha yao na hali zao ni tofauti

Bila shaka sote tumepungukiwa na uwezo wetu wa kiungu, na kuna ukweli fulani katika uelewa kwamba sisi peke yetu hatutoshi. Lakini habari njema ya injili ni kuwa kwa neema ya Mungu tunatosha. Kwa usaidizi wa Kristo, tunaweza kufanya mambo yote.13 Maandiko yanaahidi kwamba tutapata “neema wakati wa haja.”14

Ukweli wa kustajabisha ni kwamba kwa upungufu wetu unaweza kuwa nguvu yetu unapotunyenyekeza na kutugeuza kwake Kristo.15 Kutoridhika huwa kwa kiungu pale kwa unyenyekevu tunapomwendea Yesu Kristo na mahitaji yetu, badala ya kusita katika kujihurumia.

Kwa hakika, miujiza ya Yesu mara nyingi huanza na utambuzi wa hitaji, hamu, kuanguka au kupungukiwa. Mnakumbuka mikate na samaki? Kila mwandishi wa injili anasimulia jinsi Yesu kimiujiza aliwalisha maelfu waliomfuata.16 Lakini hadithi inaanza na wafuasi kutambua haja yao wakagundua walikuwa na “mikate mitano tu ya shayiri, na samaki wawili: lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?”17 Wafuasi walikuwa sahihi: hawakuwa na chakula cha kutosha, lakini walitoa kile walichokuwanacho kwa Yesu naye akawapa muujiza.

Je, umewahi kuhisi kwamba talanta zako zilikuwa ndogo sana kwa kazi iliyo mbele? Mimi pia. Lakini wewe na mimi tunaweza kutoa tulichonacho kwa Kristo, naye atazidisha juhudi zetu. Kile unachoweza kutoa ni zaidi ya kutosha—hata pamoja na kasoro na mapungufu yako ya kibinadamu—ukitegemea neema ya Mungu.

Ukweli ni kuwa kila mmoja wetu ni kizazi kimoja kutoka kwa Mungu, mtoto wa Mungu.18 Na kama alivyofanya kwa wote manabii na waume kwa wake wa kawaida nyakati zote, ndivyo Baba wa Mbinguni anavyonuia kutubadilisha.

C.S Lewis alielezea nguvu ya kubadilisha namna hii: “Jifikirie wewe kama nyumba hai. Mungu anakuja kujenga upya nyumba hiyo. Mwanzoni, pengine unaweza kuelewa anachofanya. Anatengeneza mitaro na kufunika matundu kwenye paa na kadhalika; ulijua kuwa kazi hizo zilihitaji kufanyika kwa hivyo hushangai. Lakini sasa anaanza kugonga nyumba kwa njia inayoumiza sana. … [Unaona,] anajenga nyumba nyingine tofauti kabisa na ile uliyofikiria . … Ulifikiri ulikuwa ukijengwa kuwa nyumba ndogo nzuri: lakini Yeye anajenga kasri. Ananuia kuja na kuishi ndani yake Yeye mwenyewe.”19

Kwa sababu ya dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi, tunaweza kujengwa kulingana na kazi zilizo mbele. Manabii wametufunza kuwa, tunapopanda njia ya ufuasi tunaweza kutakaswa kwa neema ya Kristo. Kutoridhika kwa kiungu kunaweza kutufanya tutende kwa imani, kufuata mialiko ya mwokozi kutenda mema, na kutoa maisha yetu Kwake kwa unyenyekevu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Russell M. Nelson, katika Tad Walch, “‘Ujumbe wa Bwana Ni kwa Kila mtu’: Rais Nelson Akizungumza kuhusu Utalii wa Ulimwengu,” Deseret News, Apr. 12, 2018, deseretnews.com.

  2. Neal A. Maxwell, “Kuwa Mfuasi,” Ensign, Juni 1996; msisitizo umeongezwa.

  3. Neal A. Maxwell, “Kuwa Mfuasi,”Ensign, Juni 16; msisitizo umeongezwa.

  4. “Kuvunjika moyo kutadhoofisha imani yako. Ukishusha matarajio yako, ufanisi wako utadidimia, hamu yako kudhoofika, na utakuwa na ugumu zaidi kumfuata Roho” (“Nini Lengo Langu kama Mmisionari?Hubiri Injili Yangu: Mwongozo Katika Huduma ya Umisionari, rev. (2018), lds.org/manual/missionary.

  5. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 28.

  6. Joseph Smith—Historia ya 1:8

  7. Joseph Smith—Historia ya 1:10; msisitizo umeongezwa.

  8. Matendo ya Mitume 10:38

  9. Bonnie D. Parkin, “Huduma Binafsi: Takatifu na yenye Thamani” (Brigham Young University devotional, Feb. 13, 2007), speeches.byu.edu.

  10. Moroni 7:13.

  11. 1 Wakorintho 13:8.

  12. 2 Nefi 32:5.

  13. “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13).

  14. Waebrania 4:16 AM.

  15. “Na ikiwa watu watakuja kwangu nitawaonyesha udhaifu wao. Ninawapatia watu udhaifu ili katika udhaifu wao wawe wanyenyekevu; na neema yangu inatosha watu wote ambao hujinyenyekeza mbele yangu; kwani wakijinyenyekeza mbele yangu, na kuwa na imani ndani yangu, ndipo nitafanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu kwao” (Etheri 12:27).

  16. Ona Mathayo 2:13–21; Marko 6:31–44; Luka 9:10–17; Yohana 6:1–14.

  17. Yohana 6:9

  18. Rais Boyd K Packer alifundisha: “Haijalishi vizazi vingi katika ukoo wako wa maisha ya sasa, haijalishi utaifa wako au watu unaowawakilisha, nasaba ya roho yako inaweza kuandikwa kwenye mstari mmoja. Wewe ni Mtoto wa Mungu!” ” (“Kwa Wasichana na Wavulana,” Ensign, May 1989, 54).

  19. C. S. Lewis, Mere Christianity (1960), 160.