Kujivika juu yetu jina la Yesu Kristo.
Na kwa uaminifu tujivike juu yetu jina la Yesu Kristo—kwa kuona kama Yeye anavyoona, kwa kutumikia kama Yeye alivyotumikia, na kwa kuamini kwamba neema Yake yatosha.
Ndugu zangu akina kaka na akina dada, hivi karibuni, nilipokuwa nikitafakari wito wa Rais Nelson kuliita Kanisa kwa jina lake sahihi, nilielekea kule mwokozi alipowafundisha Wanefi kuhusu jina la Kanisa.1 Wakati nilipokuwa nasoma maneno ya Mwokozi, Niliguswa kwa jinsi alivyowaambia pia watu kwamba “lazima mjivike juu yenu jina la Kristo.”2 Hii ilisababisha mimi kujitafakari na kujiuliza, “je mimi najivika juu yangu jina la Mwokozi kama ambavyo Angependa nifanye?”3 Leo ningependa kushiriki baadhi ya misukumo niliyopokea kama jibu kwa swali langu.
Kwanza, kujivika juu yetu jina la Kristo inamaanisha kwa uaminifu tunajitahidi kuona kama Mungu anavyoona.4 Je Mungu anaonaje? Joseph Smith alisema, “Wakati sehemu moja ya jamii ya binadamu ni kuhukumu na kulaani wengine bila huruma, Mzazi Mkuu wa ulimwengu anaona jamii yote ya familia ya binadamu kwa ulinzi na heshima ya kibaba” kwani “Upendo Wake hauelezeki.”5
Miaka michache iliyopita dada yangu mkubwa alifariki. Alikuwa na maisha yenye changamoto. Alihangaika na injili na hakuwa mwenye kushiriki kimamilifu. Mume wake aliiacha ndoa yao na akamwacha na watoto wadogo wanne kuwalea. Jioni ya siku aliyofariki, nikiwa chumbani na watoto wake wakiwepo, Nilimpa baraka ya amani kurudi nyumbani. Wakati ule nilitambua nami pia mara nyingi nimeelezea maisha ya dada yangu katika hali ya changamoto na kutoshiriki kikamilifu. Nilipo weka mikono yangu juu ya kichwa chake jioni ile, Nilipokea karipio kali kutoka kwa Roho. Nilifanywa nitambue dhahiri juu ya uzuri wake na kuruhusiwa kumwona yeye kama Mungu alivyomuona— si kama mtu ambaye alihangaika na injili na maisha, bali mtu aliyetakiwa kushughulikia changamaoto ambazo sikuwa nazo. Nilimwona yeye kama mama mzuri ambaye, licha ya vikwazo vikubwa, amelea watoto wanne wazuri na wa kupendeza. Nilimwona yeye kama rafiki wa mama yetu aliyechukua muda kumlinda na kuwa mwenza wake baada ya baba yetu kufariki.
Wakati wa jioni ile ya mwisho pamoja na dada yangu, Nina amini Mungu alikuwa akiniuliza, “Je huoni kila akuzungukaye ni mtu mtakatifu?”
Brigham Young alifundisha:
“Ningetamani kusisitiza juu ya Watakatifu … kuwaelewa wanaume na wanawake kama walivyo na sio kuwaelewa kama mlivyo.”6
Jinsi gani mara nyingi inasemwa—‘Mtu kama huyo amefanya makosa na hawezi kuwa Mtakatifu.’… Tunasikia baadhi wakiapa na kudangaya … [au] kutoitii Siku ya Sabato. … Msiwahukumu watu kama hao, kwani hamjui mpango wa Bwana kuhusu wao … [Badala yake,] wavumilieni.”7
Je, kuna yoyote anayeweza kufikiria mwokozi wetu kuwaacha nyinyi na mizigo yenu kupita bila Yeye kuwaona? Mwokozi alimwangalia Msamaria, mzinzi, mtoza ushuru, mwenye ukoma, mlemavu wa akili, na mwenye dhambi kwa macho yaleyale. Wote walikuwa watoto wa Baba Yake. Wote waliwezekana kukombolewa.
Je mnaweza kumfikiria Yeye akigeuka mbali na mtu fulani mwenye mashaka kuhusu nafasi yake kwenye ufalme wa Mungu au kutoka kwa yoyote anayesumbuliwa kwa namna yoyote?8 Mimi siwezi. Katika macho ya Kristo, kila nafsi ni ya thamani milele. Hakuna mtu yeyote aliye pangiwa kabla kushindwa. Maisha ya milele yanawezekana kwa wote.9
Kutoka karipio la Roho pembeni mwa kitanda cha dada yangu, Nilijifunza somo kuu: kwamba tunapoona vile Aonavyo, kwetu sisi utakuwa ushindi mara mbili—ukombozi wa wale tunaowagusa na ukombozi wetu.
Pili, kujivika juu yetu wenyewe jina la Kristo, lazima tusione tu kama Mungu anavyoona, bali lazima tufanya kazi Yake na kutumikia kama alivyo tumikia. Tunaishi amri mbili kuu, tunakubali mapenzi ya Mungu, tunaikusanya Israeli, na kuacha nuru yetu “iangaze mbele ya watu.”10 Tunapokea na kuishi maagano na ibada za Kanisa lake la urejesho.11 Tunapofanya haya, Mungu hutujalia nguvu za kubariki nafsi zetu, familia zetu, na maisha ya wengine.12 Jiulize, “Je ninamjua yeyote ambaye haitaji nguvu za mbinguni katika maisha yao?”
Mungu atafanya maajabu miongoni mwetu tunapojitakasa.13 Tunajitakasa kwa kujisafisha mioyo yetu.14 Tunasafisha mioyo yetu tunapomsikiliza Yeye,15 kutubu dhambi zetu,16 kuongoka,17 na kupenda kama Anavyo penda18 Mwokozi alituuliza,“Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani?”19
Hivi karibuni nilijifunza kuhusu uzoefu katika maisha ya Mzee James E. Talmage ambao ulinisababishia mimi kutulia na kufikiria jinsi ninavyowapenda na kuwatumikia wanaonizunguka. Kama profesa kijana, kabla hajawa Mtume na katika kilele cha mlipuko wa ugonjwa wa hatari wa dondakoo mwaka 1892, Mzee Talmage aligundua familia ya watu wageni, sio waumini wa Kanisa, walioishi karibu naye ambao walishambuliwa na ugonjwa huo. Hakuna yoyote aliyetaka kujiweka hatarini kwa kuingia ndani ya nyumba yenye maambukizi. Mzee Talmage, hata hivyo, mara moja aliingia ndani ya nyumba. Aliwakuta watoto wanne: wa miaka miwili na nusu amekufa kitandani, wa miaka mitano na wa miaka kumi kwenye maumivu makali, na wa miaka kumi na tatu mdhaifu. Wazazi walikuwa wakiteseka kwa huzuni na uchovu.
Mzee Talmage aliwavisha waliokufa na waliohai, akafagia vyumba, akachukua nguo zilizo chafu, na kuchoma matambara machafu yaliyoenea ugonjwa. Alifanya kazi siku mzima na kisha alirudi asubuhi iliyofuata. Mwenye umri wa miaka kumi alifariki usiku. Alimwinua na kumbeba mwenye umri wa miaka mitano. Alikohoa kamasi ya damu kote usoni mwake na kwenye nguo zake. Aliandika, “Nisingeweza kumweka mbali nami,” na alimbeba mpaka alipokufa mikononi mwake. Alisaidia kuwazika watoto wote watatu na alipanga utaratibu wa chakula na nguo safi kwa ajili ya familia inayo omboleza. Mara alipofika nyumbani, Kaka Talmage alizitupa nguo zake, na alioga katika mchanganyiko wa zinki, akajitenga na familia yake, na akateseka kwa shambulio dogo la ugonjwa ule.20
Maisha mengi yanayotuzunguka yapo hatarini. Watakatifu wanajivika jina la Mwokozi juu yao kwa kuwa watakatifu na wahudumiaji kwa wote bila kujali ni wapi au msimamo wao—maisha yanaokolewa tunapofanya hivyo.21
Mwisho, Nina amini kwamba kujivika juu yetu jina Lake lazima tumwamini Yeye. Kwenye mkutano Niliohudhuria Jumapili moja, binti aliuliza kitu kama ifuatavyo: “Rafiki wangu wa kiume na mimi hivi karibuni tumeachana,na alichagua kuliacha Kanisa. Ananiambia kamwe hajawahi kufurahi. Hii inawezekanaje?
Mwokozi alijibu swali hili wakati aliposema kwa wanefi, “Lakini ikiwa [maisha yenu] haya kujengwa juu ya injili yangu, na yamejengwa juu ya kazi za wanadamu au kazi za ibilisi, amin, nawaambia nyinyi [mtakuwa] na furaha katika kazi [zenu] kwa muda, na baadae mwisho utakuja”22 Kiufupi hakuna furaha ya kudumu nje ya injili ya Yesu Kristo.
Kwenye mkutano ule Nilifikiria kuhusu watu wengi wazuri Ninao wajua wanaosumbuka na mizigo mikubwa na amri ambazo huwakatisha tamaa kwa kiasi kikubwa. Nilijiuliza , “Nini kingine mwokozi angeweza kusema kwao?23 Nina amini angewauliza, “Je Mna niamini ?”24 Kwa mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu, Alisema, “Imani yako imekuponya, enenda kwa amani.”25.
Moja ya andiko ninalolipenda ni Yohana 4:4, ambalo linasomeka, “Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria.”
Kwa nini ninalipenda andiko hilo? Kwa sababu Yesu hakuhitaji kwenda Samaria. Wayahudi wa wakati Wake waliwadharau Wasamaria na walisafiri kwenye barabara inayozunguka Samaria. Lakini Yesu alichagua kwenda kule kutangaza mbele ya watu wote kwa mara ya kwanza kwamba alikuwa ni masiya aliyeahidiwa. Kwa ujumbe huu, Hakuchagua tu kundi lililotengwa na jamii, bali pia mwanamke—na siyo tu mwanamke yoyote bali mwanamke anayeishi katika dhambi—mtu aliyefikiriwa kwa wakati huo kuwa wa chini kuliko wote. Nina amini Yesu alifanya hivi ili kwamba mara zote tuweze kuelewa kwamba upendo Wake ni mkubwa zaidi kuliko woga wetu, uraibu, wasiwasi, majaribu, dhambi, familia zetu zilizovunjika, mfadhaiko na wasiwasi, magonjwa yetu ya muda mrefu, umasikini wetu, uonevu wetu, kukata tamaa kwetu, na ukiwa wetu.26 Anawataka wote kujua hakuna chochote na yoyote asiye weza kumponya na kumpa furaha ya kudumu.27
Neema yake yatosha.28 Yeye pekee aliteremka chini ya vitu vyote. Nguvu ya Upatanisho Wake ni nguvu ya kushinda mzigo wowote katika maisha yetu.29 Ujumbe wa mwanamke pale kisimani ni kwamba Anajua hali ya maisha yetu30 na kwamba mara zote tunaweza kutembea Naye bila kujali wapi tunasimama. Kwa mwanamke na kwa kila mmoja wetu, Anasema, “walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali [yatakuwa] chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.”31
Katika safari yoyote ya maisha kwa nini ugeukie mbali kutoka kwa Mwokozi pekee ambaye ana nguvu zote za kukuponya na kukuokoa? Thamani yoyote ile ambayo ni lazima ulipe kumwamini inastahili. akina kaka na dada zangu, na tuchague kuongeza imani yetu katika Baba wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo.
Kutoka kina cha ndani cha moyo wangu, ninatoa ushuhuda kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni Kanisa la Mwokozi, linaloongozwa na Kristo aliye hai kupitia nabii wa kweli. Ombi langu ni kwamba kwa uaminifu tutajivika juu yetu jina la Yesu Kristo—kwa kuona kama Yeye anavyoona, kwa kutumikia kama Yeye alivyotumikia, na kwa kuamini kwamba neema Yake yatosha kutupeleka nyumbani na kwenye furaha ya kudumu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.