Agano Jipya 2023
Desemba 10. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anafanya Mpango wa Baba wa Mbinguni Uwezekane? Ufunuo 1–5


“Desemba 10. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anafanya Mpango wa Baba wa Mbinguni Uwezekane? Ufunuo 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Desemba 10. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anafanya Mpango wa Baba wa Mbinguni Uwezekane?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
Sanamu ya Kristo

Desemba 10

Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Anafanya Mpango wa Baba wa Mbinguni Uwezekane?

Ufunuo 1–5

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja au mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani tumeuona mkono wa Bwana katika maisha yetu?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana katika mambo tunayopitia?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia tekinolojia kama chombo cha kushiriki injili?

  • Unganisha familia milele. Je, tunafanya nini ili kuzisaidia familia zetu kuja kwa Kristo?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Katika ono, Yohana Mfunuaji aliona kitabu ambacho “hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi” aliyestahili kukifungua, na hii ilimfanya alie (ona Ufunuo 5:3–4). Kitabu hiki kiliwakilisha “kazi za Mungu,” ikijumuisha mpango Wake kwa ajili ya kutokufa na uzima wa milele (ona Mafundisho na Maagano 77:6; Musa 1:39). Lakini kisha katika ono la Yohana, Mwanakondoo alipatikana “aliyestahili kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua mihuri yake” (Ufunuo 5:9). Habari hizi tukufu zilisababisha “elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu” ya malaika kuimba na kupaza sauti za shangwe (Ufunuo 5:11). Yesu Kristo, Mwanakondoo wa Mungu, “ukatukomboa sisi kwa Mungu kwa damu [Yake] (Ufunuo 5:9),

Tafakari kile Yesu Kristo amekutendea. Je, ushawahi kihisi kama wale walio katika ono la Yohana ambao “wakaanguka, wakasujudu (Ufunuo wa Yohana 5:14). Fikiria jinsi utakavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako au akidi yako kuelewa vyema kazi muhimu ya Yesu Kristo katika mpango wa Baba wa Mbinguni. Kama nyongeza ya Ufunuo 1–5, ungeweza pia kusoma 2 Nefi 9; “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (ChurchofJesusChrist.org); na ujumbe wa Mzee Ulisses Soares “Yesu Kristo: Mtunzaji wa Nafsi Yangu” (Liahona, Mei 2021, 82–84).

Jifunzeni Pamoja

Washiriki wa darasa lako au akidi yako wangeweza kufurahia wanajifanya kuwa wazalishaji wa filamu ambao wameombwa kutengeneza sinema ya ono la Yohana katika Ufunuo 5. Wapatie dakika chache kupitia tena sura hii na kuamua ni mandhari gani wangependa kwa sinema hiyo. Ni nini wangehisi kuwa nyakati za nguvu sana? Ni kwa jinsi gani filamu hii ingejenga imani katika Mwokozi? Ili kuendelea kuwasaidia washiriki wa darasa lako au akidi yako kujifunza kuhusu kazi ya Yesu Kristo katika mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni, hapa kuna mapendekezo machache.

  • Ungeweza kuandika kufuata vichwa vifuatavyo ubaoni: Maisha Kabla ya Kuzaliwa, Maisha Duniani, na Maisha baada ya Kifo. Waalike vijana kupitia tena vifungu vya maandiko chini ya “Nyenzo Saidizi” ili kujifunza jinsi misheni ya Mwokozi katika maisha Yake kabla kuzaliwa, maisha Yake duniani, na baada ya Ufufuko Wake hufanya mpango wa Baba uwezekane. Wangeweza kufanya muhtasari wa kile wanachojifunza chini ya kichwa ubaoni. Wape washiriki wa darasa lako au akidi yako nafasi ya kushiriki hisia zao kuhusu kile ambacho Yesu Kristo amewafanyia.

  • Ili kuwasaidia vijana unaowafundisha kuelewa vyema kile Yesu Kristo alilfanya ili kufanya mpango wa Baba wa Mbinguni uwezekane, chora njia ubaoni ikiwakilisha safari yetu kurudi kwa Baba yetu aliye Mbinguni. Chora vikwazo katika njia vyenye nembo kifo cha kimwili na kifo cha kiroho. (Kama inahitajika, vijana wangesoma maelezo chini ya “Kifo, Kimwili” na “Kifo, Kimwili” katika Mwongozo wa Maandiko [scriptures.ChurchofJesusChrist.org]). Ni kwa jinsi gani Mwokozi alifanya iwezekane kwetu kushinda vikwazo hivi? (ona 2 Nefi 9:7–10). Vijana wangeweza kupitia tena ujumbe wa Mzee Ulisses Soares “Yesu Kristo: Mtunzaji wa Nafsi Yangu” na kuandika sentensi kutoka kwa ujumbe karibu na njia ambayo inaonyesha jinsi Yesu hutusaidia kurudi kwa Mungu.

  • Wakati watu wengine wanapotuuliza maswali kuhusu imani yetu na chaguo tunazofanya, tunaweza kuchukua fursa hiyo kushiriki kwa nini Yesu Kristo ni muhimu kwetu. Njia moja ya kuwaandaa vijana kwa fursa kama hizo ni kuwaalika wao kupitia tena ujumbe wa Mzee Dieter F. Uchtdorf “Mtazame Mtu Huyo!” (Liahona, Mei 2018, 107–10) wakitafuta kweli za kushiriki kuhusu Yesu Kristo. Ungeweza kuorodhesha baadhi kweli hizi ubaoni. Ungeweza kisha kuwapa vijana muda wa kufanya maoezi kuelezeana kwa nini tunamhitaji Yesu Kristo na kwa jinsi gani maisha yao yamebarikiwa kwa sababu wanamjua Mwokozi.

Picha
Kusulibiwa kwa Kristo, na Louise Parker

Kusulibiwa kwa Kristo, na Louise Parker

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kila mtu katika darasa lako ni chanzo kikubwa cha ushuhuda, umaizi, na uzoefu kutokana na kuishi injili. Waalike wao kushiriki na kuinuana.

Chapisha