“Desemba 24. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Huonyesha Upendo Wake Kwangu? “Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Desemba 24. Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Huonyesha Upendo Wake Kwangu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Desemba 24
Ni kwa Jinsi Gani Yesu Kristo Huonyesha Upendo Wake Kwangu?
Krismasi
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni kwa jinsi gani ninaweza kupata furaha kwa kumfuata Yesu Kristo?
-
Kuwajali wenye mahitaji. Nani katika kata yetu au jamii yetu anahitaji msaada wetu? Tunawezaje kuwasaidia?
-
Waalike wote kuipokea injili. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidiana kujiandaa kwa ajili ya huduma ya ummisionari?
-
Unganisha familia milele. Je, Tunaweza kuchangia vipi katika juhudi za kata za kazi ya historia ya familia na kazi ya hekaluni?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Kabla Yeye kuzaliwa, Yesu Kristo alijulikana kama Yehova mkuu. Yeye alikuwa “Mpendwa na Mteule wa Baba tangu mwanzo” (Musa 4:2), aliyejaa utukufu, neema, na ukweli (ona Yohana 17:5; Mafundisho na Maagano 93:11). Na bado wakati alipozaliwa, Mariamu “akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wagen” i (Luka 2:7). Kwa nini Yesu Kristo alikuwa radhi kukubali wajibu Wake kama Mwokozi hata ingawa ilimaanisha kuja ulimwenguni katika hali duni? Jibu rahisi ni kwamba Yeye anatupenda. Wakati Nefi alipoona kuzaliwa kwa Mwokozi katika ono, alishuhudia juu ya “upendo wa Mungu, ambao umejimimina mioyoni mwa watoto wa watu, kwa hivyo, ni wa kupendeza zaidi ya vitu vyote” (1 Nefi 11:22).
Krismasi ni wakati maalum wa kutafakari jinsi kuzaliwa kwa Mwokozi na dhabihu ya upatanisho unaonyesha upendo Wake kwa ajili yako. Unapojiandaa kuwasaidia vijana unaowafundisha kuhisi upendo wa Mwokozi, fikiria kupitia tena Luka 4:16–21; Yohana 3:16–17; 3 Nefi 27:13–16; na ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “The Love of God” (Liahona, Nov. 2021, 16–19).
Jifunzeni Pamoja
Darasa lako au akidi yako inapoelekea mwisho wa kujifunza kwenu kwa Agano Jipya mwaka huu, ungeweza kuwaomba vijana kushiriki baadhi ya hadithi pendwa za Agano Jipya ambazo kwazo Mwokozi alionyesha upendo Wake kwa ajili ya wale wanaomzunguka Yeye. Mngeweza hata kusoma baadhi ya hadithi hizi pamoja. Ni nini hadithi hizi zinatufundisha kuhusu upendo wa Mwokozi kwa ajili yetu? Ili kuwasaidia kuendeleza kujadili upendo wa Mwokozi, tumia shughuli kama zifuatazo.
-
Waalike washiriki wa darasa lako au akidi kufikiria upendo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walionao kwa ajili yetu kama shada zuri la maua (ona Russell M. Nelson, “Upendo Mtakatifu,” Ensign, Feb. 2003, 24). Fikiria kumpa kila mtu ua lililokatwa kutoka kwa karatasi na kumuomba kila mmoja kusoma mojawapo ya vifungu vya maandiko katika “Nyenzo Saidizi.” Waombe waandike juu ya maua kile wanachojifunza kuhusu upendo wa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walio nao kwa ajili yetu. Wanaposhiriki kile walichopata, wangeweza kuweka maua yao pamoja kutengeneza shada. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutambua njia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaonyesha upendo Wao kwetu?
-
Nyimbo kadhaa zinaelezea njia ambazo Mwokozi huonyesha upendo Wake kwetu (ona, kwa mfano, “I Know That My Redeemer Lives,” Nyimbo, na. 136). Washiriki wa darasa wangeweza kuchagua wimbo na kushiriki uzoefu wakati walipohisi upendo wa Mwokozi katika njia ambazo ni sawa na zile zilizoelezewa katika wimbo. Ni baadhi ya njia zipi Mwokozi ameonesha upendo Wake kwetu? Kama wafuasi wa Kristo, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo Wake?
-
Kuna mawazo mengi ya uongo duniani kuhusu upendo wa Bwana kwa ajili yetu. Kwa mfano, baadhi wangeweza kufikiria kwamba wakati watu wanapokuwa matajiri au kufanikiwa, humaanisha kwamba Mungu huwapenda wao zaidi ya wengine. Baadhi wangeweza kuhisi kwamba kama Mungu anatupenda kweli, Yeye angetukubali jinsi tulivyo na bila kutuomba tubadilike. Ni jumbe gani za uongo kuhusu upendo wa Mungu ambazo tumezisikia? Ili kukinza jumbe hizi za uongo, ungeweza kuwaomba vijana kupitia tena ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Upendo wa Mungu” au ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Upendo na Sheria” (Liahona, Nov. 2009, 26–29). Ni kweli gani tunazipata katika jumbe hizi ambazo hutusaidia kuelewa upendo wa Mungu?
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Yohana 3:16–17; 15:9–13; Warumi 8:35–39; Waebrania 12:5–6, 9–11; 1 Nefi 11:21–23; Alma 7:11–12; 3 Nefi 11:13–17; Moroni 7:45–48
-
Michael John U. Teh, “Mwokozi Wetu Binafsi,” Liahona, Mei 2021, 99–101
-
Taniela B. Wakolo, “Mungu Anawapenda Watoto Wake,” Liahona, Mei 2021, 94–96