Agano Jipya 2023
Novemba 26. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwasaidia Mababu Zangu Kumkaribia Yesu Kristo? 1 na 2 Petro


“Novemba 26. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwasaidia Mababu Zangu Kumkaribia Yesu Kristo? 1 na 2 Petro,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Novemba 26. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwasaidia Mababu Zangu Kumkaribia Yesu Kristo? 1 na 2 Petro,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

kisima cha maji ya ubatizo

Novemba 26

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwasaidia Mababu Zangu Kumkaribia Yesu Kristo?

1 na 2 Petro

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni mada gani uaskofu umejadili katika mikutano ya baraza la vijana la kata yenu? Tunaweza kufanya nini kama darasa au akidi kulingana mijadala hiyo?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwafikia watu katika njia za kama Kristo wakati tunaona hitaji na hatujui cha kusema?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tumepata nini kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambacho kinatuletea shangwe? Je, tunawezaje kushiriki shangwe hiyo na wengine?

  • Unganisha familia milele. Tunafanya nini ili kupata majina ya mababu zetu ambao wanahitaji ibada za hekaluni? Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kupata majina ya mababu zao?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Ni nini kitatokea kwa mamilioni ya watu ambao wamekufa bila kupata nafasi yoyote ya kusikia ujumbe wa injili ya urejesho wa Yesu Kristo au kupokea maagizo ya kuokoa? Tunaweza kupata vidokezo kwa maswali haya katika 1 Petro 3:18–20; 4:6, ambapo Petro aliongea juu ya injili ikihubiriwa kwa wafu. Kisha Mafundisho na Maagano 138 hufunua ukweli kamili—mababu zetu wanaweza kumkaribia kikamilifu kwa Kristo kama wana imani katika Yeye na kukubali injili Yake na kufanya ibada zipatikane kwao katika hekalu. Baraka hii inahitaji kwamba sisi—wazao ambao tuna injili—tutafute majina yao, kwenda hekaluni, na kupokea ibada za kuokoa kwa niaba yao.

Ni uzoefu gani umepata ambao umewasaidia mababu zako kumkaribia Kristo? Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kusisimka kuhusu historia ya familia na kazi ya hekaluni na kujiamini zaidi katika uwezo wa kufanya hivyo? Unapojiandaa, ungeweza kusoma ujumbe wa Mzee Dale G. Renlund “Historia ya Familia na Kazi ya Hekaluni: Kuunganishwa na Uponyaji” (Liahona, Mei 2018, 46–49).

Jifunzeni Pamoja

Ni kwa jinsi gani washiriki wa darasa lako au akidi yako wangemjibu mtu ambaye anashangaa jinsi watu wazuri ambao hawakupata nafasi ya kupokea injili wanaweza kuokolewa? Wanapata nini katika 1 Petro 3:18–20; 4:6 ili kusaidia kujibu swali hili? Katika video hii “Will I Do My Part?,” Mzee Enrique R. Falabella anatoa umaizi wa ziada. Unaweza kuendelea na mjadala wako kwa shughuli moja au zaidi ya zifuatazo

  • Fundisho la kuwakomboa wafu ni la kipekee kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Waalike washiriki wa akidi au darasa kujifunza Mafundisho na Maagano 138:25–39 kama watu binafsi au vikundi na kushiriki kile wanajifunza (ona “Nyenzo Saidizi” kwa ajili ya maandiko ya ziada kwenye mada hii). Mistari hii inatufundisha nini kuhusu jinsi Mungu anavyohisi kuhusu watoto Wake? Ni kwa jinsi gani ubatizo wa wafu unawasaidia mababu zetu kusogea karibu na Kristo? Ni kwa jinsi gani unatusaidia kumsogelea Kristo na kuongeza imani yetu Kwake?

  • Ni nini kingewapatia vijana mwongozo wa kuwa wanajihusisha katika kazi ya hekalu na historia ya familia? Pengine wangeweza kutazama moja au zaidi ya video zinazopatikana katika “Nyenzo Saidizi” na kutafuta njia kazi ya hekalu na historia ya familia inavyoweza kuwabariki. Wangeweza pia kutafuta baraka zilizoahidiwa katika orodha katika Mzee Dale G. Renlund “Historia ya Familia na Kazi ya Hekaluni: Kuunganishwa na Uponyaji.” Waalike kushiriki ni baraka gani zilizo na maana kwao na kwa nini. Pia ungeweza kujadili baadhi ya vikwazo ambavyo vingeweza kutuzuia kushiriki katika hekalu na historia ya familia. Ni kwa jinsi gani Mwokozi anaweza kutusaidia kushinda vikwazo hivi?

  • Kama washiriki wa darasa lako au akidi yako wanaweza kuwa na chombo cha digitali, ungeweza kuchukua muda fulani kuwaonyesha jinsi Bwana amefanya iwe rahisi kuliko wakati mwingine kuwapata mababu zetu ambao wanahitaji ibada za kuokoa (ona “Nyenzo Saidizi”). Ungeweza pia kumualika mshauri wa kata wa historia ya familia na kazi ya hekalu kuwasaidia vijana kuelewa nyenzo hizi. Ungeweza pia kuwahimiza vijana kufanya mipango ya kuchunguza nyenzo hizi nyumbani na kuripoti katika mkutano ujao.

wasichana wakiongea

Tunapotekeleza ibada takatifu katika hekalu, tunafanya baraka za injili zipatikane kwa wale waliokufa.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Wakati unapowaalika vijana kufundisha, chukua muda kuwasaidia kujiandaa ipasavyo. Elezea kile unafanya ili kujiandaa kufundisha. Katika njia hii utakuwa unawasaidia vijana sio tu kwa somo moja bali kwa kipindi cha maisha cha kufundisha injili katika njia ya Mwokozi.