Agano Jipya 2023
Novemba 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusogea Karibu na Yesu Kristo kupitia Ibada Takatifu na Maagano? Waebrania 7–13


“Novemba 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusogea Karibu na Yesu Kristo kupitia Ibada Takatifu na Maagano? Waebrania 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Novemba 12. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusogea Karibu na Yesu Kristo kupitia Ibada Takatifu na Maagano?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

mvulana akipitisha sakramenti

Novemba 12

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kusogea Karibu na Yesu Kristo kupitia Ibada Takatifu na Maagano?

Waebrania 7–13

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Je, ni kwa jinsi gani tumemkaribia Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani tunajaribu kuwa zaidi kama Yeye?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Ni nani amekuwa katika akili zetu karibuni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaida watu binafsi?

  • Waalike wote kuipokea injili. Je, tunaweza kujibu maswali ya marafiki zetu kuhusu Kanisa katika njia ambayo inaimarisha imani yao katika Mwokozi?

  • Unganisha familia milele. Ni njia zipi tunazoweza kuunganika vyema na wanafamilia wengine kama vile kina babu na binamu zetu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Kwa karne nyingi, watoto wa Israeli, wakati mwingine waliitwa Waebrania, walikuwa wamekuwa na bidii kushiriki katika ibada zilizohusiana na tabenakulo na sheria ya Musa. Na bado wengi wao hawakutambua kuwa mambo haya yalikuwa “mambo yaliyo mbinguni”—”kivuli cha mema yatakayokuja” (Waebrania 9:23; 10:1). Ibada zilikusudiwa kuwafundisha wao kuhusu Yesu Kristo. Hiki ndicho Paulo alielezea katika Waraka wake kwa Waebrania. Ujumbe wake pia ni muhimu kwetu leo kwa sababu sisi pia tuna ibada takatifu kwa dhumuni hilo hilo. Kwa hiyo kuna maana ya kujiuliza wenyewe maswali haya: Ibada hizi zitatusaidia kumkumbuka Yesu Kristo? Kuna kingine zaidi tungeweza kufanya ili kupata nguvu ya Yesu Kristo kupitia ibada za injili? Au sisi, tupo kama Waebrania wa kale, wakikosa umuhimu wao wa kina?

Tafakari maswali haya unaposoma Waebrania 7–13 na unapojiandaa kufundisha kuhusu jinsi ibada na maagano hutuleta karibu na Yesu Kristo. Ungeweza pia kujifunza baadhi ya jumbe za mkutano mkuu zilizotajwa katika muhtasari huu.

Jifunzeni Pamoja

Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuona jinsi wanavyoweza kumsogelea Yesu Kristo kupitia ibada na maagano ya injili Yake, ungeweza kuwaalika waorodheshe baadhi ya ibada za injili na maagano yake husika ubaoni (ona Mada za Injili, “Ibada,” “Agano,” topics.ChurchofJesusChrist.org). Ni nini ibada hizi na maagano haya yanatufundisha kuhusu Kristo na Upatanisho Wake? Kauli ya Mzee David A. Bednar katika “Nyenzo Saidizi” hutoa ufafanuzi wa ibada na umaizi mwingine muhimu. Shughuli kama hii zifuatazo zinaweza kusaidia.

  • Ungeweza kuwaalika vijana kusoma Mafundisho na Maagano 84:19–22 na wajadili maswali kama haya: “Nguvu ya uungu” inamaanisha nini? Ni kwa jinsi gani ibada na maagano yalitusaidia kupata nguvu hiyo? Ibada na maagano huleta tofauti gani katika maisha yetu? Ni kwa jinsi gani hutusaida kuunganika na Mwokozi? Ili kusaidia kujibu maswali haya, vijana wangeweza kusoma aya nne za kwanza za ujumbe wa Mzee Kent F. Richards “Nguvu za Uungu” (Liahona, Mei 2016, 118) au ujumbe wa Mzee Bednar “Acheni Nyumba Hii Na Ijengwe kwa Jina Langu” (Liahona, Mei 2020, 84–87), hasa sehemu “Kutoka Nje Ndani.”

  • Fikiria kuwauliza wale unaowafundisha jinsi wangeelezea ibada ya sakramenti kwa mtu ambaye hajui lolote kuihusu. Sehemu “Uzoefu na Ushuhuda” katika ujumbe wa Mzee Taniela B. Wakolo “Ibada za Kuokoa Zitatuletea Nuru ya Ajabu” (Liahona, Mei 2018, 39–41) hutoa mfano. Vijana pia wanaweza kupata mafundisho muhimu katika video “Always Remember Him” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani sakramenti hutuleta karibu na Yesu Kristo? Je, Ni fursa gani tunazo za kuwafundisha wengine kuhusu hili?

  • Kupitia tena mapendekezo matano katika ujumbe wa Mzee Peter F. Meur “Sakramenti Inaweza Kutusaidia Kuwa Watakatifu” (Liahona, Nov. 2016, 85–87) kungeweza kuwasaidia vijana kuelewa jinsi ya kujiandaa vyema kwa ajili ya sakramenti. Au, kama una vijana wanaojiandaa kupokea endaumenti yao, pitia tena pamoja nao sehemu yenye kichwa cha “Kuhusu Endaumenti ya Hekaluni” katika temples.ChurchofJesusChrist.org. Jadili jinsi ibada hizi takatifu na maagano yake husika yanaweza kutuleta karibu na Mwokozi.

  • Fikiria kuandika maneno Sakramenti, Ubatizo, na Hekalu ubaoni. Chini ya kila moja, waalike vijana waorodheshe maagano tunayofanya. Marejeo katika “Nyenzo Saidizi” yanaweza kusaidia. Jadilini pamoja jinsi maagano haya hutusaidia kumkaribia Yesu Kristo.

  • Ungeweza kugawa darasa lako au akidi yako katika vikundi na kukipangia kila kikundi kupitia tena sehemu ya ujumbe wa Mzee Ronald A. Rasband “Kusimamia Ahadi na Maagano Yetu” (Liahona, Nov. 2019, 53–56) au ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Kwa Nini Njia ya Agano” (Liahona, Mei 2021, 116–19). Wahimize wao kushiriki kile walichojifunza kuhusu jinsi kushika maagano yao huimarisha uhusiano wao na Yesu Kristo.

wasichana wakitembea nje ya hekalu

Ibada takatifu za injili huleta “nguvu za kiungu” katika maisha yetu (ona Mafundisho na Maagano 84: 19–22).

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

  • Mosia 18:8–10 (Agano la Ubatizo)

  • Moroni 4–5 (Agano la Sakramenti)

  • Mzee David A. Bednar alifundisha; “Ibada takatifu ni muhimu katika injili ya Mwokozi na katika mchakato wa kuja Kwake na kutafuta kuzaliwa upya kiroho. Ibada ni matendo matakatifu ambayo yana kusudi la kiroho, umuhimu wa milele, na yana uhusiano na sheria na amri za Mungu.

    “Ibada za wokovu na kuinuliwa zinazoendeshwa katika Kanisa la urejesho la Bwana ni zaidi ya kaida za kidini au utendaji wa kiishara. Bali, zina mikondo iliyoidhinishwa ambayo kwayo baraka na nguvu za mbinguni zinaweza kutiririka kwenye maisha yetu binafsi.

    “Ibada zilizopokelewa na kuheshimiwa kwa uadilifu ni muhimu kwa kupata nguvu ya ucha mungu na baraka zote zilizopatikana kupitia Upatanisho wa Mwokozi” (“Daima Bakiza Ondoleo la Dhambi Zetu,” Liahona, Mei 2016, 59–60).

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kadiri unavyowaalika wale unaowafundisha kutenda kulingana na mafundisho ya kweli, unawasaidia kuendeleza uzoefu wa kujifunza nyumbani mwao na katika maisha yao.