“Oktoba 22. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kubaki Imara katika Sharti Langu kwa Yesu Kristo? 1 na 2 Wathesalonike,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Oktoba 22. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kubaki Imara katika Sharti Langu kwa Yesu Kristo?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Oktoba 22
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kubaki Imara katika Sharti Langu kwa Yesu Kristo?
1 na 2 Wathesalonike
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Je, ni uzoefu gani ya hivi karibuni umeimarisha shuhuda zetu?
-
Kuwajali wenye mahitaji. Je, ni akina nani wanahitaji msaada wetu na sala zetu? Je, ni nini tunahisi kuvutiwa kukifanya ili kuwasaidia?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa wanafamilia au marafiki ambao hawashiriki imani yetu?
-
Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha upendo zaidi na ufadhili kwa familia zetu na kuleta tofauti chanya katika nyumba zetu.
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Wengi wetu wanamjua mtu fulani wakati mmoja alionekana kuwa na sharti kamili kwa Yesu Kristo lakini tena alishaanguka kutoka kwa imani yao. Ni kawaida kushangaa, “Ni nini ambacho kingenitokea?” Paulo aliwasifu Watakatifu Wathesalonike kwa sababu ya uaminifu wao lakini alihisi kushawishika kuwaonya wao kuhusu mafundisho ya uongo na athari zingine ambazo zingedhoofisha imani yao. Bila kujali jinsi sharti lako kwa Mwokozi lilivyo sawa sasa, daima kuna mengi tunaweza kufanya ili “kuyatengeneza mapungufu ya imani [yetu]” (1 Wathesalonike 3:10).
Unaposali kuhusu watu katika darasa lako au akidi yako, sikiliza mnong’ono ambao Bwana anakutumia. Unahisi ni nini kingewasaidia wao kubaki waaminifu kwa Mwokozi bila kujali upinzani watakaokabiliana nao? Ni nini kimekusaidia wewe? Unapojiandaa kufundisha, ungeweza kupitia tena ujumbe wa Mzee Dale G. Renlund “Msimamo Thabiti kwa Yesu Kristo” (Liahona, Nov. 2019, 22–25) katika nyongeza ya 1 na 2 Wathesalonike.
Jifunzeni Pamoja
Ili kuwasaidia vijana kupitia tena kile walichosoma katika 1 na 2 Wathesalonike na kutambulisha mada ya kubaki imara katika sharti langu kwa Mwokozi, mngeweza kusoma pamoja 2 Wathesalonike 2:1–3. Jadilini kile neno “kuanguka” lingemaanisha. Hasa, inamaanisha nini kwa mtu kuanguka kutoka kwa Yesu Kristo? Ungeweza kulinganisha neno hili na virai vingine alivyotumia Paulo , “mnasimama imara katika Bwana” (1 Wathesalonike 3:8) na “msikate tamaa katika kutenda mema” (2 Wathesalonike 3:13). Ungeweza kisha kupitia tena 1 Wathesalonike 5:15–23. Ni kwa jinsi gani ushauri wa Paulo katika mistari hii hutusaidia kutuzuia kutoanguka kutoka kwa imani yetu katika Yesu Kristo—hata wakati tunapokabiliana na upinzani? Tumia shughuli kama zifuatazo kuwasaidia washiriki wa darasa au akidi kubaki imara katika sharti lao kwa Mwokozi.
-
Inaweza kuwa mwongozo kujifunza kutokana na mifano ya wengine ambao wamekuwa thabiti katika sharti lao kwa Kristo. Kwa mfano, mngeweza kujifunza pamoja mfano wa Anti-Nefi-Lehi, ambao walikuwa wamekuwa “watu wakaidi na wagumu na wakali” lakini “hawakuanguka kamwe” baada ya “kuongoka kwa Bwana” (Alma 17:14; 23:6–8) Ni nini Alma 24: 8–18 inapendekeza kuhusu kwa nini walibakia waaminifu? Ni chaguo gani muhimu waliyafanya? Ni kwa jinsi gani Mwokozi aliwasaidia? Mifano ya ziada inaweza kupatikana katika ujumbe wa Mzee Dale G. Renlund “Msimamo Thabiti kwa Yesu Kristo.” Pengine vijana wangeweza kusoma baadhi ya mifano hii na kushiriki kile wanachojifunza kuhusu kubakia mkweli kwa Kristo. Ni kwa jinsi gani tumebaki na sharti kwa Bwana licha ya mapungufu yetu?
-
Katika juhudi zetu za kuimarisha imani yetu, itakuwa msaada kuwa macho juu ya nguvu ambazo zinatafuta kuidhoofisha. Ono la Lehi la mti wa uzima linaelezea baadhi ya nguvu hizi. Pengine ungeweza kuonyesha picha ya ono (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, [2009], na. 69), na mpitie tena pamoja utendeti, unaopatikana katika 1 Nefi 8:10–34. Katika ono, ni kitu gani kiliwazuia watu kula tunda la mti? Ni nini kiliwasaidia watu kufikia mti na kubaki pale? Ni nini vitu hivi vinaashiria katika maisha yetu?
-
Katika ujumbe wake “Nguvu za Kushinda Adui” (Liahona, Nov 2019, 110–12), Mzee Peter M Johnson aliorodhesha njia tatu Shetani hujaribu kutudhoofisha. Ungeweza kumpangia kila kijana kusoma kuhusu mojawapo ya hizi na kushiriki na darasa au akidi mifano ya jinsi Shetani hutumia chombo hiki dhidi ya vijana leo. Kisha wangeweza kusoma mojawapo ya mapendekezo manne ya Mzee Johnson ya kushinda mbinu za adui na kushiriki kile walichojifunza.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Jeffrey R. Holland, “Bwana, Ninaamini,” Liahona, Mei 2013, 93–95
-
Neil L. Andersen, “Usimwache Kamwe,” Liahona, Nov. 2010, 39–42
-
Becky Craven, “Makini dhidi ya Kawaida,” Liahona, Mei 2019, 9–11