Agano Jipya 2023
Oktoba 8. Ni kwa Jinsi Gani Injili ya Yesu Kristo Inaweza Kuimarisha Familia Yangu? Waefeso


“Oktoba 8. Ni kwa Jinsi Gani Injili ya Yesu Kristo Inaweza Kuimarisha Familia Yangu? “Waefeso,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Oktoba 8. Ni kwa Jinsi Gani Injili ya Yesu Kristo Inaweza Kuimarisha Familia Yangu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

Picha
mama na mabinti wakipika

Oktoba 8

Ni kwa Jinsi Gani Injili ya Yesu Kristo Inaweza Kuimarisha Familia Yangu?

Waefeso

Picha
ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha, kwa nyongeza kwenye kushauriana kuhusu shughuli mahsusi za darasa au za akidi, mnaweza kutaka kujadili misukumo na dhima kutoka mkutano mkuu. Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia.

  • Ni dhima zipi au jumbe zipi zimejitokeza bayana kwetu? Ni nini kuliimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?

  • Ni nini kiliimarisha shuhuda zetu juu ya manabii walio hai? Ni nini tulihisi kushawishika kufanya kwa sababu ya kile tulichojifunza au kuhisi?

  • Ni nini tunahitajika kufanya kama darasa au akidi ili kukumbuka na kutendea kazi ushauri tuliousikia katika mkutano mkuu?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

Picha
ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Baadhi ya watu katika darasa lako au akidi yako wanaweza kuwa na familia imara na zenye upendo ambazo hukuza imani na roho. Wengine wanaweza kuwa peke yao katika juhudi zao za kuishi injili, na baadhi wanaweza kukumbana na ubishi na huzuni kubwa. Lakini hakuna yeyote katika darasa lako au akidi yako aliye na familia kamilifu, hasiye na changamoto. Na kila mmoja anaweza kufikia nguvu ya Yesu Kristo, ambayo inaweza kuponya na kuimarisha familia.

Mwokozi anataka kuzibariki familia. Wakati mwingine jinsi Yeye anavyofanya hivi ni kupitia upendo na mfano wa kijana ambaye alikuwa anajitahidi kumfuata Yeye na kuishi injili Yake. Unapojiandaa kuwafundisha vijana kuhusu nguvu zilizopo kwa ajili yao na familia zao kupitia Yesu Kristo, tafakari kanuni katika Waefeso ambazo zinaweza kutusaidia kuimarisha mahusiano ya familia. Unaweza pia kujifunza “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” (ChurchofJesusChrist.org).

Jifunzeni Pamoja

Baada ya kuwapa washiriki wa darasa au akidi fursa ya kushiriki kile Roho amewafundisha wiki hii walipokuwa wanajifunza Waefeso, tafuta njia za kutambulisha mada au jinsi Yesu Kristo anaweza kutusaidia kuimarisha familia zetu. Kwa mfano, ungeweza kuwaalika vijana kutafuta na kushiriki vifungu katika Waefeso ambavyo vina kanuni tunazoweza kutumia kuimarisha mahusiano ya familia. Baadhi ya mifano ingejumuisha Waefeso 2:19–22; 3:14–19; 4:1–3, 25–26, 29–32; 5:1–2; 6:1–4. Ni kwa jinsi gani ushauri katika mistari hii unabariki familia? Ni kwa jinsi gani kuwa na Mwokozi na injili Yake kumekuwa baraka katika nyumba zetu? Hapa kuna baadhi ya mawazo ya shughuli ya ziada yanayohusiana na mada hii:

  • Kama ungependa kujadili amri ya “kumheshimu baba yako na mama yako” (Waefeso 6:2), ungeweza kuanza kwa kuuliza darasa au akidi kile neno heshima humaanisha kwao. Pengine mtu angeweza kushiriki ufafanuzi kutoka katika kamusi au Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Waalike vijana kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo wao wangeweza kutumia amri hii katika maisha yao wenyewe. Ingeweza pia kuwa mvuto kuchunguza jinsi Yesu Kristo alimheshimu Baba Yake aliye Mbinguni na mama Yake, Mariamu (ona, kwa mfano, Luka 2:41–52; Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana 2:4 [katika Yohana 2:4, tanbihi a]; Yohana 8:29; 19:25–27). Nini tunaweza kujifunza kutokana na mfano wa Yesu ambacho kinaweza kuimarisha mahusiano yetu na wazazi wetu?

  • Ingeweza kuwa msaada kuzungumza kuhusu vifaa vinavyohitajika kujenda nyumba thabiti. Ni baadhi ya vitu gani ambavyo vinahitajika kujenga nyumba imara? Kama sehemu ya mjadala, ungeweza kushiriki kauli hii ya Mzee L. Whitney Clayton: “Kile chenye umuhimu zaidi ni usanifu wa ndani wa mioyo ya wakazi, si jengo lenyewe” (“Nyumba za Kupendeza,” Liahona, May 2020, 107–9). Ungeweza pia kujadili mapendekezo manne Mzee Clayton alitoa katika ujumbe wake wa jinsi ya kujenga “nyumba za kupendeza.”

  • Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” inajumuisha ahadi: “Furaha katika maisha ya familia sana sana inaweza kupatikana inapojengwa kwa mafundisho ya Bwana Yesu Kristo.” Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Mwokozi yanajenga msingi wa familia yenye furaha? Tangazo la familia na maandiko chini ya “Nyenzo Saidizi” hutoa mifano. Ni kwa jinsi gani wanafamilia wanaweza kusaidiana mmoja na mwingine kuishi mafundisho haya?

  • Pengine washiriki wa darasa wangetazama video “Through Small Things,” ambayo ndugu watatu wanazungumza kuhusu kupokea mwaliko wa askofu wao wa kufikiria njia za kufanya nyumba yao kuwa mahali patakatifu. Ni kwa jinsi gani familia katika video hii ilibarikiwa kwa sababu ya matendo ya vijana hawa? Ni nini kinaweza kuifanya nyumba yetu kuwa mahali patakatifu? Fikiria kuwaalika vijana kukubali mwaliko sawa na ule askofu alitoa. Ili kuwasaidia kufikiria kile wangeweza kufanya, mngeweza kujadili swali lililoulizwa katika video hii: “Nini uko radhi kufanya ili kuwa na Roho katika yako?”

Picha
familia ikijifunza pamoja

Mafundisho ya Yesu Kristo ni msingi kwa ajili ya furaha katika maisha ya familia.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Ikiwa vijana watahisi kwamba unawaamini, imani yao katika uwezo wao mtakatifu itakua, na watakushangaza na yale wanaweza kutimiza. Wasaidie kuona ono la kile ambacho Baba wa Mbinguni anajua wanaweza kuwa.

Chapisha