“Septemba 24. Je, Ni kwa Jinsi Gani Nitafuata Mfano wa Mwokozi katika Kuwasaidia Wale Walio na Uhitaji? 2 Wakorintho 8–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Septemba 24. Je, Ni kwa Jinsi Gani Nitafuata Mfano wa Mwokozi katika Kuwasaidia Wale Walio na Uhitaji?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Septemba 24
Je, Ni kwa Jinsi Gani Nitafuata Mfano wa Mwokozi katika Kuwasaidia Wale Walio na Uhitaji?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Tulijadili nini wakati uliopita, na ni mialiko gani au kazi gani zilitolewa? Tumefanya nini kushughulikia mialiko hiyo au kazi hizo?
-
Kuwajali wenye mahitaji. Tunaweza kufanya nini au kusema nini ili kuwafikia wale wanaoweza kuwa wanahisi kuwa wapweke au wako mbali na Baba wa Mbinguni?
-
Waalike wote kuipokea injili. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Yesu Kristo?
-
Unganisha familia milele. Ni mawazo gani tunaweza kushiriki mmoja na mwingine kuimarisha familia zetu?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Ni fursa zipi wewe na washiriki wa darasa au akidi mnazo za kuwahudumia wale walio na uhitaji wanaokuzunguka? Wakati ule Watakatifu katika Yerusalemu walikuwa wanateseka na walihitaji msaada, Paulo aliwaandikia Wakorintho kuwahimiza kutoa kwa ukarimu, “si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.” Yeye aliahidi kwamba kama watafanya hivyo, Mungu aweza “kuwajaza kila neema [wao], ili kwamba “mpate kuzidi sana katika kila tendo jema” (2 Wakorintho 9:7–8).
Paulo pia alilenga mfano wa Yesu Kristo, ambaye “ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake” (2 Wakorintho 8:9). Mwokozi kwa hiari aliuacha utajiri wa mbinguni ili kwamba Yeye angeweza kuhudumia na kutufanya matajiri milele. Fikiria mifano kutoka katika maisha Yake wakati Yeye aliwafikia kuwahudumia wale waliomzunguka Yeye. Katika nyongeza ya kusoma 2 Wakorintho 8–9 unapojiandaa kufundisha, fikiria kusoma ujumbe wa Dada Michelle D. Craig “Macho ya Kuona” (Liahona, Nov 2020, 15–17).
Jifunzeni Pamoja
Ili kuanza mjadala wako, omba darasa au akidi kutengeneza orodha ya baadhi ya sababu za kwa nini mtu yaweza hasiwahudumia wengine walio uhitaji. Tunajifunza nini kutoka kwa mafundisho ya Paulo katika 2 Wakorintho 8:9; 9:7–9 ambacho kinatupa mwongozo kufanya zaidi ili kuwahudumia wale walio na uhitaji? Shughuli zifuatazo zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vyema jinsi ya kuwatunza wale wanaotuzunguka.
-
Mara kadhaa katika maandiko, Bwana jinsi Yeye anahisi kuhusu kuwatunza maskini na walio na mahitaji. Baadhi ya mifano inayoorodheshwa katika “Nyenzo Saidizi.” Njia moja ya kupitia tena mafundisho haya ni kugawa darasa lako au akidi yako katika majozi na kuomba kila jozi kujifunza baadhi ya maandiko. Waombe wajadili kile vifungu hivi vinafundisha kuhusu kuwatunza maskini na wenye shida. Kwa nini unafikiria kutunza maskini na wenye mahitaji ni muhimu sana kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Waalike vijana kupanga njia wanazoweza kuwasaidia wale walio na uhitaji.
-
Wakati mwingine tunakuwa na shughuli nyingi za mambo yetu wenyewe kwamba tunashindwa kutambua mahitaji ya wale wanaotuzunguka. Katika ujumbe wake “Macho ya Kuona,” Dada Michelle D. Craig alipitia tena simulizi ya Mungu akifumbua macho ya kijana (ona 2 Wafalme 6:15–17). Tunajifunza nini kutoka kwenye simulizi hii? Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa simulizi zingine alizoshiriki kuhusu kutambua mahitaji ya wengine na kuwafikia? (Ona pia video “Pray for Eyes to See as He Sees” katika ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa pia wangeweza kushiriki uzoefu wao ambapo mtu alitambua mahitaji yao na kuwahudumia. Ni lini tulitambua mahitaji ya wengine na kuwahudumia? Ni kwa jinsi gani tunahisi tunapopokea au kutoa huhudumiaji kama huo?
-
Je, washiriki wa darasa au akidi wanaelewa jinsi ya kutimiza wajibu wao wa kusaidia kuwatunza wale walio na uhitaji? Fikiria kujadiliana pamoja Mosia 4:16–21 na 18:8–10, vile vile sehemu husika za Kitabu cha Maelezo ya Jumla (10.2.2 kwa ajili ya akidi za Ukuhani wa Haruni au 11.2.2 kwa ajili ya wasichana). Je, unahisi kupata mwongozo kufanya nini kama matokeo ya kujifunza nyenzo hizi? Fikiria kupanga njia mnazoweza kufanya kazi pamoja ili kuwafikia wale walio na mahitaji katika darasa lako au akidi yako, kata, au jamii. Video katika “Nyenzo Saidizi” zinaweza kutoa baadhi ya mawazo. Kwa ajili ya fursa za huduma katika eneo lako, ona JustServe.org.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Mathayo 25:31–45; Yakobo 1:27; Mosia 2:17; Alma 34:27–28; Mormoni 8:35–39; Mafindisho na Maagano 104:14–18 (Umuhimu wa kuwatunza maskini na walio na uhitaji)
-
Jeffrey R. Holland, “Si Sisi Sote Tu Waombaji?,” Liahona, Nov. 2014, 40–42
-
“Michelle’s Story,” “Caring for the Poor and Needy,” “I Was a Stranger: Love One Another,” “Fast Offerings: Are We Not All Beggars” (videos), ChurchofJesusChrist.org